DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,344
2,000
Hatari sana
Yaani ni shida jamani, unafungua bomba maji yanatoka meusi kabisa, huwezi kuyatumia kwa namna yoyote ile, na inaweza kuchukua hata masaa matano ndio yanaanza kutoka masafi

Umeona eeh, sisi wakati mwingine tunashindaga siku nzima maji yanatoka machafu, tunauliza hapa wako kimya tu
 

Ndongi

New Member
May 21, 2020
3
45
Ushauri wangu kwa Dawasa
Wawe wanaangalia mabomba yanayopasuka na kuyazibiti mapema
 

kidumba

Member
Aug 16, 2013
56
125
DAWASA KIMARA MWISHO NJIA YA KWENDA BONYOKWA HAPA KABLA YA DARAJA HATUNA MAJI SIKU YA TATU LEO,BOMBA LIMEPASUKA HAPA KWA MZEE MGWAO MAARUFU MZEE WA MA DCM WAMEKUJA WATU WENU WAMELIKUNJA WAKAONDOKA HIYO NDO HUDUMA YA ISO?SIKU TATU HAMNA REPAIR?
 
Apr 27, 2019
6
45
TATIZO LA KUVUJA KWA MAJI.
Eneo la Mbagala Kiburugwa kuna visima vya Maji vilichimbwa na Dawasa kikiwemo kisima namba 1.Pamoja na kupata Maji ya kutosha lakini kuna tatizo la mabomba kuvujisha Maji na tatizo hili siyo la mwezi mmoja ila ni miezi mingi bila kupata ufumbuzi. Ukitoka mashine namba 1 mpaka Njia Panda shule Kiislamu eneo lote hilo ni kero. Wahusika Dawasa Temeke akiwemo meneja Temeke AMBOKILE 0736/0717312028 anajua pamoja na aliyepewa jukumu la kuangalia eneo hilo MKAMA 0714958040 taarifa anayo. Mafundi wanaonekana wakiwa kwenye mashine namba 1 wanapiga soga tu. Engineer LUHEMEJA ulijizolea sifa sana ukiwa Kilimanjaro kwani nami Nilikuwa huko, ebu jaribu wakumbushe watu wako wasifanye Kazi kwa mazoea, hii ni AWAMU ya tano ya Mhe. JOHN POMBE MAGUFULI watu ambao hawatatui kero za wananchi hawana nafasi.
 
Apr 27, 2019
6
45
Mbona hatuoni majibu ya Dawasa humu? Au ndo kusema shirika ili la umma halina mpango na wananchi? Ilani ya CCM kweli itatekelezeka kama watendaji ndo hawa?
 

Gibeath-Elohimu

JF-Expert Member
Jan 5, 2014
372
500
DAWASA naomba kuwauliza sisi wakazi wa Kimara Bucha/Baruti mna mpango gani na sisi kwa kutukosesha maji leo inaingia siku ya pili bila taarifa yoyote ile juu ya katizo la maji....mnataka tuishije??????
 

Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
2,176
2,000
DAWASA vipi mnasema hamna mita za maji wakati mita zimejaa Kariakoo! Kwanini msiruhusu mtu anunue mita yake nyie mje mconnect if mnashindwa kuzipata kwa wakati.
 

BONTABOY

Member
Nov 20, 2015
25
45
Dawasco dawasco mmenikwaza sana tokea niwaambie tatizo langu ...
Mimi ni mteja wenu niko Kibaha misugusugu Vitendo tangu niunganishiwe maji yametoka miezi miwili na mpaka leo hakuna maji sijui tatizo na bili wanatuma sijazilipa kwakuwa mita haitumiki sijui bili wanaitoa wapi naomba kuwasilisha
 

BONTABOY

Member
Nov 20, 2015
25
45
Mimi ni mteja wenu niko Kibaha misugusugu Vitendo tangu niunganishiwe maji yametoka miezi miwili na mpaka leo hakuna maji sijui tatizo na bili wanatuma sijazilipa kwakuwa mita haitumiki sijui bili wanaitoa wapi naomba kuwasilisha
Mbona sijibiwi au hii ni mfu
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
2,573
2,000
gharama za kuunganishiwa zipo juu sana!!
punguzeni ili kila mtu aweza kumudu kulipia gharama, watu wengi mpaka leo wameshindwa kulipia gharama za kuunganishiwa maji, wizara iangalie utaratibu wa kuwaongezea muda wale wanao daiwa gharama za kuunganishiwa huduma badala ya kuwakatia maji.
mfano mradi ulio fanywa na wahindi ktk maeneo ya Chalinze, kibaha, kiluvya, kibamba n.k.
lengo lisiwe kuwakatia huduma wateja bali lengo liwe ni kusaidia namana ya kuweza kukamilisha gharama za kuunganishiwa huduma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Gibeath-Elohimu

JF-Expert Member
Jan 5, 2014
372
500
Yaani DAWASA mnashindwa hata kutia maji dawa,leo ni siku ya tatu wakazi wa Kimara tunapata maji machafu kama vile yanatoka mtoni au kwenye kidimbwi....shida ni nini.
 

Jinikashkash

JF-Expert Member
Nov 27, 2020
457
1,000
DAWASA
Pamoja na kero ya umeme sasa nanyi mnatuumiza
Hakuna maji Manzese Darajani leo siku ya nne huku kila siku naletewa SMS za kudai malipo
Tufungulieni maji kwani mnadhani tutafua na kuoga na maji ya Bakhressa ya chupa?
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,009
2,000
AISEE KUWENI SERIOUS MAJI YANAKATIKA WEEKEND TUTAFUA SAA NGAPI. MNAYAFUNGUA J3 HAPO SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 8.
 

radavi

Senior Member
Oct 17, 2014
176
225
Hivi hamjawahi japo kufikira kuwapelekea maji wakazi wa kisopwa wakati bomba limepita karibu yao?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom