DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA TUNAOMBA KUFAHAMISHWA KIMARA BONYOKWA TUMERUDI KWENYE MGAO WA MAJI ?MAANA MLIJIGAMBA HAKUNA TENA SHIDA YA MAJI KIMARA TUMEKUWA NA KUKATIKA KATIKA KWA MAJI WIKI YA TATU SASA NA HIVI NINAVYOANDIKA TANGU JUMAMOSI HATUNA MAJI SASA SIJUI KUNA SHIDA GANI NA HATUTANGAZIWI, MUWE MNATOA TAARIFA BASI TUJUE KAMA NI MGAO AU KUNA HITILAFU MAHALI TUJUE.
Dawasco Kimara mnakwama wapi? Mbezi kwa Msuguli eneo la Nguzo hatuna maji leo Ni siku ya nne na hakuna taarifa tatizo ni ni nini? Ndo nimeanza kulipa deni sasa na maji hakuna si bora nisilipe sasa.Huu ni upumbavu mnafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti DAWASA kule maeneo ya Mbezi juu wananchi wanasema kwanini mnafungulia maji usiku wa manane na kuyafunga alfajiri?
Lengo lenu hapo linakuwa ni nini?
Kwamba watu wasilale wakeshe wakichota maji na kujaza vyombo?
Au mnataka washindwe kuchota maji ili wateseke na kununua maji yenu ya ulanguzi ?
Pia wanauliza ni siku ipi au zipi hasa katika wiki maji huwa mnayafungulia ?

Kwa nini mnafungulia maji kwa kuvizia watu wakiwa wamelala usiku wa manane?

Wamesema niwaulizie.

Nahitaji majibu.

Na salamu hizi zimfikie Meneja wa DAWASA -Kawe


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi inakuaje kwako unakosa maji miezi takribani miwili pengine kwa kosa la Bomba kukatika na umetoa taarifa ofisini... Alafu msoma mita akija bado anaandika Deni lile lile na unapaswa ulilipe?!
 
Ila nilishangaa siku Moja nafika ofisini kwenu (Dawasco) kwa lengo la kuripoti tatizo yule mtu wa mapokezi ananipa namba ya simu niongee (nimueleze shida yangu) kwa simu na mtu aliekua pale pale ofisini ndani.

Nikamuuliza nini maana ya mimi kufika pale ofisini kwao? Kama ningetaka kupiga simu si ningepiga nikiwa nyumbani kwangu!

Mnafanya kazi nzuri sana lakin wachache wanataka kuharibu taswira ya taasisi hii muhimu
 
Ila nilishangaa siku Moja nafika ofisini kwenu (Dawasco) kwa lengo la kuripoti tatizo yule mtu wa mapokezi ananipa namba ya simu niongee (nimueleze shida yangu) kwa simu na mtu aliekua pale pale ofisini ndani. Nikamuuliza nini maana ya mimi kufika pale ofisini kwao? Kama ningetaka kupiga simu si ningepiga nikiwa nyumbani kwangu!..
Mnafanya kazi nzuri sana lakin wachache wanataka kuharibu taswira ya taasisi hii muhimu


Je kama simu ingekuwa haina hela ingekuwaje?

Hiyo tabia naona inataka kuzoeleka maana hata Tanesco Tegeta kuna baadhi ya huduma mtu akienda anaambiwa na mlinzi wa geti apige simu akiwa nje ya geti.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nawapongeza DAWASCO HQ, simu zao zinapatika kiurahisi na unaisema shida yako na unapata majibu, ila hizi simu za huku sijui ndo wanaita branch( Kawe, Kimara etc) mara nyingi huwa hazipatikani.

Ni aibu mimi mteja wa Boko (Boko limetumika kama mfano) nipige simu HQ kueleza shida yangu wakati eneo langu la Boko kuna ofisi na simu hazipatikani.
 
Ila nilishangaa siku Moja nafika ofisini kwenu (Dawasco) kwa lengo la kuripoti tatizo yule mtu wa mapokezi ananipa namba ya simu niongee (nimueleze shida yangu) kwa simu na mtu aliekua pale pale ofisini ndani. Nikamuuliza nini maana ya mimi kufika pale ofisini kwao? Kama ningetaka kupiga simu si ningepiga nikiwa nyumbani kwangu!..
Mnafanya kazi nzuri sana lakin wachache wanataka kuharibu taswira ya taasisi hii muhimu

Pole mkuu
 
DAWASA, KWA NINI MAJI YENU SIKU HIZI MARA NYINGI NI MACHAFU SANA? Machafu sana yaani utadhani tope. Kulikoni?

Naongelea wilaya ya Kinondoni, kawe, Mwenge, Mbezi, ,kunduchi, ununio etc.
sijui kwengine!
DAWASA.
 
Wakuu samahani nataka kujua Bei ya unit moja ya maji ni shilingi ngapi ?
 
Dawasa mkifanya kazi kwa mazoea, maji salama kwa kila kaya itakuwa ndoto.Nendeni mitaani mlikoweka miundombinu yenu ongea na wateja wenu iwapo wanapata huduma ya maji au la.

Kisha mrudi maofisini kuja na majibu. Inakuwaje hapa kinyerezi zimbili hatupati maji Mara kwa Mara huku mnakuja na sababu zizile?

Mara pampu mbovu, Mara ujenzi was barabara ya morgoro, Mara mitambo ya Ruvu. Wananchi wanajua wizara yenu ni miongoni mwa wizara zinazopata bajeti kubwa sn
WAKUU DAWASA KUNA MRAFI WA MAJI UMEJENGWA PALE TEGETA WAZO KWA AJILI YA KUPELEKA MAJI MADALE JE UTAANZA LIN????


Sent using Jamii Forums mobile app
 
sawasco kimara sio wasikivu kwenye huduma za maji yanayomwagika barabarani ovyo kwa kiweka mipora isiyo na ubora na kina cha uifashi bomba mabomna kiwa juu ya ardhi kwa uzembe wa wachimbaji na wao hawajiusishi tena kwa zaidi ya kidai bili na kukata maji
mfano mie bomba linapasuliwa aifiki mwezi linakanyagwa na kupasuliwa nawaambia wanibadilishie laini hawataki sikia anadai tuu mnakera sana napata hasara ya kila mwezi 20000 nani atanilipa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
DAWASCO, maji mengi sana yanapotea mitaani kwa kumwagika kutokana na mabomba yaliyo pasuka. Je, hamna kitengo Cha kuzungukia mitaa kubaini maji yanayo mwagika ovyo na kusabishia shirika hasara? Hizi Ni hela za wananchi. Wanaosoma mita hata wakiona wanapita tu.
 
Tumeletewa bill ya maji. B/f haifanani na bili ya mwezi uliopita. Mwezi uliopita majitaka bill ni 16,000 na mwezi huu bill ya maji taka ni 4,000. Naishi Mwenge. Mnatufanyia sana wizi kwenye department ya Accounts
 
Habari za mchana wadau sisi wakazi wa mtaa wa serenge kata ya mbagala manispaa ya Temeke, Dawasa walichukuwa mradi wa kisima cha maji kilichokuwa kinasimamiwa na kamati ya maji tangu mwaka 2005, chanzo cha maji ni ya chumvi kwa kutumia kwa kunywa hayafai, ila wamefunga mita kwa kila mteja na bei yao unit moja 1563/=.wateja wenu inabidi kununua maji kwa ajili ya kunywa kwa gharama nyingine, tunaomba maji ya baridi kutoka katika vyanzo vyenu vya mtoni na hata mbagala nzasa. Kwani mlituahidi kutuletea maji hayo.
 
Habari za asubuhi wadau? Kuna tatizo Mbezi Luis, mtaa wa Muhimbili, sijajua linasababishwa na nini? Kumewekwa mabomba muda sasa yapata mwaka mpaka sasa maji hayatoki.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Ununio Boko hakuna maji siku ya 5 leo bila taarifa yoyote.

Ni mgao au kuna tatizo gani?
 
Back
Top Bottom