DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

-Hongera Sana Rais SSH kwa Uamuzi wa kuiagiza DAWASA kuchukua jukumu la kutoa Ankara ya huduma ya maji kwa wateja.
-Huko nyuma Ankara ya huduma ya maji zilikuwa zinatolewa na kampuni moja ya Africa ya Kusini na Serikali ilikuwa inalipwa fedha nyingi kama commission.
-Uamuzi huu umetoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania wanao soma mita na kufanya matengenezo madogo madogo ya miundombinu ya maji.
-DAWASA walianza kutoa Ankara ya maji (wenye tarakimu 12 badala ya Ankara za awali ambazo zilikuwa na tarakimu 13,) kuanzia Mwezi August 2022.
-Pamoja na dhamira njema ya Rais wetu, lakini watendaji wa DAWASA au Hazina, ambao walisimamia mchakato wa kuhama kutoka kwenye mfumo wa makaburu kuja kwenye mfumo wa utoaji Ankara wa Serikali,hawakuna waangalifu au makini.
-Matokeo yake DAWASA hawawezi kuona data au Ankara za miaka ya nyuma.
-Wateja wengi hawakuingiziwa taarifa sahihi kwenye akaunti zao wakati DAWASA walipohamia kwenye mfumo mpya.
-DAWASA wanashindwa kuona (to access) bili za July 2022 kurudi miezi ya nyuma.
-Kampuni ya Africa kusini wameondoka na taarifa zetu za mapato (billing software yao).
-DAWASA kama wanataka taarifa za mapato kwa miaka ya nyuma, inabidi waombe taarifa hizo kutoka kampuni ya Africa kusini.
-Mwezi November 2022 (Kulikwa hakuna maji kwa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake lakini Wateja wamepewa Ankara kubwa Sana( mwezi huo mitambo ilizimwa).
- Mimi ninatumia wastani units 15 za maji kwa mwezi, lakini mwezi November 2022 DAWASA wametuma Ankara ya shs110,850 sawa na units 66wakati mwezi November 2022 hatukuwa na maji.
-Nimetoa taarifa DAWASA Temeke , lakini wanipatie statement of account kwa mwaka 2022 ( January 2022 mpaka December 2022), lakini wameniambia hawawezi ku-access taarifa za kuanzia January 2022 mpaka July 2022
-Best practice, whenever you want to migrate from one billing system to another billing system,the old billing information should retained for future use.
-best practice require the accounting or financial data should be retained for at least 7 years for future use.

Ushauri
1). Serikali (DAWASA) ifuatilie taarifa zetu za mapato (Billing data) toka Kampuni ya Africa kusini.
2).CAG afanye ukaguzi maalum(Special Audit to establish Over/understatement opening balance) kujua usahihi wa taarifa za mapato za miaka ya nyuma.
3). Serikali ipatiwe saver au taarifa zilizohifadhiwa kwenye server,kwa maana ni mali yetu watanzania.
-
 
TANGAZO LA DHARURA

KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU

14.04.2023

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wanaohudumiwa na Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa wastani wa saa 16 siku ya Jumamosi , Aprili 15, 2023.

Muda: Kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 4 asubuhi Jumapili

Sababu: Kuruhusu matengenezo ya bomba kubwa la inchi 36 eneo la Visiga Saheni na kutoa matoleo mawili maeneo ya Kwembe na Msigani yanayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji maeneo ya Kibamba Pangaboy na Mbezi Malamba Mawili.

Maeneo yatakayoathirika ni;
Chalinze, Chalinze Mboga, Msoga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi Magari Saba, Mbezi Kwa Yusufu, Njeteni, Msigani, Kifuru, Mbezi Inn, Mbezi Stendi ya Magufuli, Mbezi Mshikamano, Mbezi Louis, Makabe, Msakuzi, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202-121 (WhatsApp Tu)

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
 
Mkimalizana na Maji karibuni dollrubii_decors

SIsi ni wauzaji wa HomeDecors kwa bei nafuu zaidi kuliko wote karibu ujione.
KWA MAHITAJI YA
♦️PAZIA
♦️ MAUA NA MAPAMBO YA NDANI
♦️FURNITURE
♦️KITCHENWARE
TUNATUMA MIKOA YOTE🇹🇿
WHTAP|📞 0699306065
KARIBUNI SANA. FREE DELIVERY DAR

INSTAGRAM @dollrubii_decors
 
Kwanini Dawasco kibaha hawapokei simu?
Kwanini kile kimama pale reception hakina majibu mazuri. Kama kimechoka, ruksa kikalee wajukuu. Alidanganya umri Sasa miaka imeenda kazi inamshinda kufanya.
Ombi langu Ni moja tu. Dawasa kibaha pokeeni simu.
 
Mita yangu Ina ukungu, hata nikivaa miwani sioni namba, mnasomaje na kuniletea bili? Nilisharipoti Ila hamjarekebidha. Siku za nyuma mkileta bili naangalia nakuta sawa. Sasa niangalie wapi? Njooni muondoe ukungu kwenye mita. Nipo Kerege - CCM, Bagamoyo.
 
Bill inakuja kubwa kuliko matumizi.
Naomba mtueleweshe kwani unit moja sawa na kiasi gani cha maji…?? Maana bill inayokuja kila mwisho wa mwezi katika makazi yangu ni bill ya kiwanda.
 
Bill inakuja kubwa kuliko matumizi.
Naomba mtueleweshe kwani unit moja sawa na kiasi gani cha maji…?? Maana bill inayokuja kila mwisho wa mwezi katika makazi yangu ni bill ya kiwanda.
Swali muhimu lakini halikujibiwa!
Unit moja ni sawa na lita ngapi na ni bei gani?
 
Nashukuru mmerekebisha mita yangu Kerege - Ccm, Bagamoyo. Huduma ni nzuri na ninaifurahiya. Ninalipa kulingana na matumizi yangu. Big up!
 
Back
Top Bottom