Taifa_Kwanza
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 443
- 86
Ukitazama efforts zilizofanywa na "projects in hand" za umeme utakuta tunakos a umeme kwa ajili ya watendaji wachache tu na si kuwa hakuna efforts, wazembe wachache ama kwa matamanio yao ama kwa kutowajibika ipasavyo ndio wanaichafua "system" na hizo bugs lazima ziwe eliminated one way or the other.
Matatizo tulio nayo ya umeme sasa hivi, sio kuwa hatuna mitambo ya kutosha kuondosha mgao au kumaliza kabisa hili tatizo, la hasha. Tatizo ni watendaji wabovu kama huyu Jairo wa wizarani na wengine pale Tanesco. Kuna habari za kuaminika kabisa (ushahidi nnao) kuwa baada ya sheria mpya ua umeme,kuna watu wametaka kuja kuwekeza kwa fedha zao lakini wamewekewa vizingiti pale wizarani, na nani? huyo huyo Jairo. kuna wawekezaji wamemuandikia email kuhusu kuwa na nia kabisa ya kuwekeza kwenye umeme, lakini hata kuwajibu hakuwajibu na hao watu anawajua na wameshafanya kazi hapa Tanzania (in the past). Kwa nini hajawajibu? kwa sababu alikuwa anajuwa akianza mawasiliano nao atakosa ulaji. Ushahidi nnao.
Tumeishachoshwa na malalamiko kwa wasaidizi, kama haya yote mnayajua, inakuwaje Jakaya hayajui.
Tatizo ni Jakaya