Mkuu wa shule ya Green Hill tunaomba majibu yanayoeleweka

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu habari za uzima?

Leo nimerudi toka mishe mishe zangu nakutana na taarifa mbaya na za kushangaza kwa wakati mmoja.

Binafsi kipindi nataka kumpeleka shule mwanangu chaguo langu la kwanza ilikuwa ni shule ya Green Hill iliyopo pugu kona. Lakini mama yangu alinichagulia ABC mbadala wa Green hill.

Leo nimesikitishwa sana na taarifa za kuungua kwa mabweni ya shule hiyo. Taarifa zilizopo ni kwamba shule ya Green Hill iliyopo pugu kona imeungua mabweni usiku wa kuamkia Jana mida ya saa sita.

Kitu cha kushangaza watoto wawili mpaka sasa wamefariki na wengine wapo ICU kutokana na walioanza kuvuta hewa ya Moshi. Mkuu wa shule nimemsahau ni mwana mama anasema kwamba chanzo ni umeme kukatika katika hovyo, hatuwezi kubisha kama ni umeme au labda wanafunzi walikuwa na vitu vya umeme kama pasi au Laaah.....

Kitu kinachotushangaza mmiliki wa shule hajaruhusu waandishi wa habari kufika hapo na kazuia kabisa habari hizi zisirushwe.

Anadai ati yeye kama hayo magodoro na hasara zingine atalipa?!!!! Hivi huyu mmiliki tumuelewaje? Yaani watoto wamekufa, unazuia waandishi na mgambo umeweka mlangoni.
Tunataka majibu ya maswali haya.

Kwanini unazuia waandishi kufika hapo ndani na kuhoji uongozi pamoja na wanafunzi kama mashuhuda?
Kama tatizo ni Tanesco kukatika kwa umeme hovyo hovyo nini kinakufanya uzuie?

Taarifa hizi ni za jirani ambaye mtoto wake yupo ICU mpaka sasahiv na mkuu wa shule amegoma kabisa kuonyesha ushirikiano.

Wazazi ambao mpo ma watoto hapo Green Hill poleni sana ila inabidi mkuu wa shule awe responsible pamoja na mmiliki.

Mamlaka husika tunaomba mfatilie ni nini kinafichwa hapo shuleni kiasi cha mmiliki wa shule kuwa mgumu kuruhusu waandishi na uchunguzi.
 
Usingesikia watu wanalalama,wangeenda kwenye ile shule na kumaliza kwa moto, hii ndio lugha hawa ndio wanaijua, zimamoto nayo chali
 
Wakuu habari za uzima?

Leo nimerudi toka mishe mishe zangu nakutana na taarifa mbaya na za kushangaza kwa wakati mmoja.

Binafsi kipindi nataka kumpeleka shule mwanangu chaguo langu la kwanza ilikuwa ni shule ya Green Hill iliyopo pugu kona.
Lakini mama yangu alinichagulia ABC mbadala wa Green hill.
Leo nimesikitishwa sana na taarifa za kuungua kwa mabweni ya shule hiyo. Taarifa zilizopo ni kwamba shule ya Green Hill iliyopo pugu kona imeungua mabweni usiku wa kuamkia Jana mida ya saa sita.

Kitu cha kushangaza watoto wawili mpaka sasa wamefariki na wengine wapo ICU kutokana na walioanza kuvuta hewa ya Moshi. Mkuu wa shule nimemsahau ni mwana mama anasema kwamba chanzo ni umeme kukatika katika hovyo, hatuwezi kubisha kama ni umeme au labda wanafunzi walikuwa na vitu vya umeme kama pasi au Laaah.....

Kitu kinachotushangaza mmiliki wa shule hajaruhusu waandishi wa habari kufika hapo na kazuia kabisa habari hizi zisirushwe.

Anadai ati yeye kama hayo magodoro na hasara zingine atalipa?!!!! Hivi huyu mmiliki tumuelewaje? Yaani watoto wamekufa, unazuia waandishi na mgambo umeweka mlangoni.
Tunataka majibu ya maswali haya.

Kwanini unazuia waandishi kufika hapo ndani na kuhoji uongozi pamoja na wanafunzi kama mashuhuda?
Kama tatizo ni Tanesco kukatika kwa umeme hovyo hovyo nini kinakufanya uzuie?

Taarifa hizi ni za jirani ambaye mtoto wake yupo ICU mpaka sasahiv na mkuu wa shule amegoma kabisa kuonyesha ushirikiano
Wazazi ambao mpo ma watoto hapo Green Hill poleni sana ila inabidi mkuu wa shule awe responsible pamoja na mmiliki.
Mamlaka husika tunaomba mfatilie ni nini kinafichwa hapo shuleni kiasi cha mmiliki wa shule kuwa mgumu kuruhusu waandishi na uchunguzi.
Ni ipi ya secondary au primary ?
 
Back
Top Bottom