Daudi Albert Bashite sasa utaenda kumlilia nani?

Daudi Albert Bashite sasa utaenda kumlilia nani?

Wengine wametumia msemo maarufu Wa mjini wa siku hizi, "Mwana kulitafuta, mwana kulipata".

Lakini wengine wameenda mbali zaidi na kukumbuka maneno aliyoyasema Gwajima kanisani kwake kwamba "Nimemfuta Daudi Albert Bashite kwenye uongozi na siasa hapa Tanzania mpaka atakapokuwa ametubu". Hata wale ambao waliyapuuza yale maneno wameanza kuamini kumbe maneno ya mtumishi wa Mungu yanaweza kumpata mtu

Wengine wanajiuliza inawezekanaje rais atoe onyo kwamba wateule wake walidhike na nyadhifa walizopewa halafu mtu akapuuza? Kwamba imekuaje mpaka akapuuza maneno ya rais? Na kwamba labda ile laana ya Gwajima imemfanya asahau.

Wachambuzi wengine wamesema, wakati wa uongozi wake, ilikuwa akipatwa jambo anaenda kuomba kanisani wamwombee na kulia machozi huko, sio mara moja. Sasa kwa sasa ni raia wa kawaida, je ataenda kumlilia nani?

Kwako Mwalimu Kashasha.

View attachment 1508501
Naam ila usiwaamini kabisa wanasiasa Mkuu... yawezekana huyohuyo akapita kwa kishindo na akasafika vilivyo
 
Ogopa Sana kugusa watumishi wa Mungu,Ni hatari Sana kuwagusa ,utapata laana
 
Laanaa ya Gwajima inamtafunaa huyo
, MANENO yanaenda kutimia anafutwa kabisaa
 
Mwana kulitafuta, mwana kulipata ( Vijana waliozaliwa miaka ya 80s)
Mkuu, siku zote Mkulu ana ndimi mbili. Akikuambia hivi ana maana ile. Ktk wooote aliowatumbua huyu ni mtoto mpendwa na "special" kwa makusudi fulani. Wewe subiri na utakuja kuniambia.
 
Huyo Jamaa wengi wanamchukia siyo kuwa amewaudhi Bali hapati mateso wanayotarajia, wengi wao Wana kashfa Kama yake ya vyeti na wanakula msoto wanasahau kuwa jamaa upande wa pili Ni Creativity Cream, Walimu kupanda daladala bure, kuita wamama waliotelekezwa, kutengeneza Gari za Polisi chakavu.. ...........
Mimi sijampata hata theluthi, namkubali huenda kauli ya baba Yake ikawa danganya toto, Let's wait the true judge is time.
 
Mkuu, ujue hapo unamzungumzia Waziri wa Mambo ya Ndani ama Ulinzi ajaye endapo CCM itabahatika kubakia madarakani.
Siafiki ila ndio ukweli...pale wakushindana naye ni Ndungulile ambaye nadhani anajua hatoboi
 
Wabongo bado mnaamini Movie linalochezwaa na Bashite na baba yake???? Hivi mbona hamjifunzi tu hizi movie za ccm kwa kweli Mastermind anaepanga hizi Moves anatishaa sanaa..
Yaani wanaauzi jamani[emoji34] kufanywa ka majuha kila siku!!! Magu na bashite dam dam zingine sinema tu ngojeni muone.
 
Wengine wametumia msemo maarufu Wa mjini wa siku hizi, "Mwana kulitafuta, mwana kulipata".

Lakini wengine wameenda mbali zaidi na kukumbuka maneno aliyoyasema Gwajima kanisani kwake kwamba "Nimemfuta Daudi Albert Bashite kwenye uongozi na siasa hapa Tanzania mpaka atakapokuwa ametubu". Hata wale ambao waliyapuuza yale maneno wameanza kuamini kumbe maneno ya mtumishi wa Mungu yanaweza kumpata mtu

Wengine wanajiuliza inawezekanaje rais atoe onyo kwamba wateule wake walidhike na nyadhifa walizopewa halafu mtu akapuuza? Kwamba imekuaje mpaka akapuuza maneno ya rais? Na kwamba labda ile laana ya Gwajima imemfanya asahau.

Wachambuzi wengine wamesema, wakati wa uongozi wake, ilikuwa akipatwa jambo anaenda kuomba kanisani wamwombee na kulia machozi huko, sio mara moja. Sasa kwa sasa ni raia wa kawaida, je ataenda kumlilia nani?

Kwako Mwalimu Kashasha.

View attachment 1508501
Jina lake limekatwa before hajarudisha form End.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom