Waziri Mchengerwa: Kama ikifika Oktoba hamjapata muwekezaji Binafsi wa Mabasi, DART mjiuzulu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,100
49,795
Je unadhani hii itakuwa ni mwarobaini wa kero za usafiri wa Mwendokasi?

My Take
Naunga mkono hoja ila Mwekezaji awe mwenye uwezo isije kuwa kama zile treni za Wahindi za TRC

=====
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa ameielekeza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kufikia Oktoba 2024 iwe imempata mwekezaji binafsi ambaye ni mtoa huduma wa mabasi hayo ili kuleta ufanisi.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo jana Machi 18, 2024 wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi Fungu namba 56 na namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, katika ukumbi wa Anne Makinda uliopo bungeni jijini Dodoma.

“Nilishawaambia watu wa Dart wakati wanakuja kunipitisha kwenye mfumo tunaokwenda nao ikifika Oktoba wakishindwa kuhakikisha wanampata mwekezaji atakayekwenda kuhudumia njia hii wa sekta binafsi na kushindwa kuhakikisha mabasi yamepatikana waniletee barua za kujiuzulu, na tumeshakubaliana na hakuna mjadala watu wanataka huduma,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema kuwepo kwa mwekezaji binafsi mradi huo utaendeshwa kwa ufanisi kutokana na kulipa kodi kwa Serikali, na wakati huohuo atawajibika endapo atatoa huduma isiyostahili.

“Atahakikisha anatoa huduma nzuri ili kama tukileta mabasi ya kutosha watu wa Dar es Salaam wataegesha magari yao watatumia mwendokasi na tutakwenda kuokoa zaidi ya Sh300 bilioni ambayo tungeitumia kununua mabasi,” amesema Mchengerwa.

Waziri huyo ameongeza kuwa ifikapo Septemba hadi Oktoba Serikali itakuwa imepata mabasi ya kutosha ya kuendesha njia zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo sekta binafsi ili Watanzania wa Dar es Salaam wahudumiwe vizuri kabla ya kuanza kupeleka huduma ya mwendokasi kwenye majiji mengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Denis Londo amepongeza uamuzi huo na kusema kuwa maamuzi hayo yataacha alama nzuri kwa waziri aliyekuwepo kutokana na kuwa mbunifu.

Source: Mwananchi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa ameielekeza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kufikia mwezi Oktoba 2024 iwe imempata mwekezaji binafsi ambaye ni mtoa huduma wa mabasi hayo ili kuleta ufanisi.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Fungu namba 56 na Fungu namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Anne Makinda uliopo bungeni jijini Dodoma.

“Nilishawambia watu wa ‘DART’ wakati wanakuja kunipitisha kwenye mfumo tunaokwenda nao ikifika mwezi Oktoba wakishindwa kuhakikisha wanampata mwekezaji atayekwenda kuhudumia njia hii wa Private sekta na kushindwa kuhakikisha mabasi yamepatikana waniletee barua za kujiuzulu na tumeshakubaliana na hakuna mjadala watu wanataka huduma” amesema Mchengerwa

Akisisitiza hilo Mchengerwa amesema kuwepo kwa mwekezaji binafisi katika mradi huo utaendeshwa kwa ufanisi kutokana na kulipa kodi kwa serikali na wakati huohuo atawajibika endapo atatoa huduma isiyostahili.

“Atahakikisha anatoa huduma nzuri ili watu waweze kuhudumiwa na kama tukileta mabasi ya kutosha watu wa Dar es Salaam watapaki mabasi yao watatumia mwendokasi na tutakwenda kuokoa zaidi ya sh.bilioni 300 ambayo tungeitumia kununua mabasi” amesema Mohammed Mchengerwa

Hata hivyo Mchengerwa amesema ifikapo mwezi Septemba hadi Oktoba serikali itakuwa imepata mabasi ya kutosha ya kuendesha njia zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi ili watanzania wa Dar es Salaam waweze kuhudumiwa vizuri kabla ya kuanza kupeleka huduma ya mwendokasi katika majiji mengine.
 
Tatizo miradi mnawapa wanasiasa ndiyo maana wanaifirisi miradi ya serikali ,wapeni wafanyabiashara waendeshe hizo taasisi....Hivi ukimpa Bakharesa au Mo watashindwa kuziendesha? Sasa nyinyi mnampa Rizimoko/Kisena aendeshe unadhani zitafanikiwa? Hao ni wapigaji na si wafanyabiashara.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohammed Mchengerwa ameielekeza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kufikia mwezi Oktoba 2024 iwe imempata mwekezaji binafsi ambaye ni mtoa huduma wa mabasi hayo ili kuleta ufanisi.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Fungu namba 56 na Fungu namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika ukumbi wa Anne Makinda uliopo bungeni jijini Dodoma.

“Nilishawambia watu wa ‘DART’ wakati wanakuja kunipitisha kwenye mfumo tunaokwenda nao ikifika mwezi Oktoba wakishindwa kuhakikisha wanampata mwekezaji atayekwenda kuhudumia njia hii wa Private sekta na kushindwa kuhakikisha mabasi yamepatikana waniletee barua za kujiuzulu na tumeshakubaliana na hakuna mjadala watu wanataka huduma” amesema Mchengerwa

Akisisitiza hilo Mchengerwa amesema kuwepo kwa mwekezaji binafisi katika mradi huo utaendeshwa kwa ufanisi kutokana na kulipa kodi kwa serikali na wakati huohuo atawajibika endapo atatoa huduma isiyostahili.

“Atahakikisha anatoa huduma nzuri ili watu waweze kuhudumiwa na kama tukileta mabasi ya kutosha watu wa Dar es Salaam watapaki mabasi yao watatumia mwendokasi na tutakwenda kuokoa zaidi ya sh.bilioni 300 ambayo tungeitumia kununua mabasi” amesema Mohammed Mchengerwa

Hata hivyo Mchengerwa amesema ifikapo mwezi Septemba hadi Oktoba serikali itakuwa imepata mabasi ya kutosha ya kuendesha njia zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi ili watanzania wa Dar es Salaam waweze kuhudumiwa vizuri kabla ya kuanza kupeleka huduma ya mwendokasi katika majiji mengine.
Oktoba si mwaka ujao anaweka mazingira ya kwenda kuandaa familia yake ipeleke proposo!
 
Je unadhani hii itakuwa ni mwarobaini wa kero za usafiri wa Mwendokasi?

My Take
Naunga mkono hoja ila Mwekezaji awe mwenye uwezo isije kuwa kama zile treni za Wahindi za TRC

=====
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa ameielekeza Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kufikia Oktoba 2024 iwe imempata mwekezaji binafsi ambaye ni mtoa huduma wa mabasi hayo ili kuleta ufanisi.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo jana Machi 18, 2024 wakati akiwasilisha Randama ya Bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi Fungu namba 56 na namba 2 la Tume ya Utumishi wa Walimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, katika ukumbi wa Anne Makinda uliopo bungeni jijini Dodoma.

“Nilishawaambia watu wa Dart wakati wanakuja kunipitisha kwenye mfumo tunaokwenda nao ikifika Oktoba wakishindwa kuhakikisha wanampata mwekezaji atakayekwenda kuhudumia njia hii wa sekta binafsi na kushindwa kuhakikisha mabasi yamepatikana waniletee barua za kujiuzulu, na tumeshakubaliana na hakuna mjadala watu wanataka huduma,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema kuwepo kwa mwekezaji binafsi mradi huo utaendeshwa kwa ufanisi kutokana na kulipa kodi kwa Serikali, na wakati huohuo atawajibika endapo atatoa huduma isiyostahili.

“Atahakikisha anatoa huduma nzuri ili kama tukileta mabasi ya kutosha watu wa Dar es Salaam wataegesha magari yao watatumia mwendokasi na tutakwenda kuokoa zaidi ya Sh300 bilioni ambayo tungeitumia kununua mabasi,” amesema Mchengerwa.

Waziri huyo ameongeza kuwa ifikapo Septemba hadi Oktoba Serikali itakuwa imepata mabasi ya kutosha ya kuendesha njia zote kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ikiwemo sekta binafsi ili Watanzania wa Dar es Salaam wahudumiwe vizuri kabla ya kuanza kupeleka huduma ya mwendokasi kwenye majiji mengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Denis Londo amepongeza uamuzi huo na kusema kuwa maamuzi hayo yataacha alama nzuri kwa waziri aliyekuwepo kutokana na kuwa mbunifu.

Source: Mwananchi

ni mpango mujarabu wa kuanzia 🐒

but ni vizuri na ni muhimu zaid kujiandaa kuongeza uwekezaji zaid, walau kuwe na muwekezaji zaid ya moja ili kuchochea ushindani na kuongeza ufanisi na ubora wa huduma yenyewe 🐒

kwa muwekezaji moja anaweza kupunguza changamoto lakini ufanisi na ubora wa huduma ikawa ni vilevile au duni zaid na abiria kukosa chaguo 🐒
 
Pumzika kwa amani baba,kweli tunakukumbuka na ulisema haya,angekuwepo hili lingeisha zamani sana angechukua hata new force buses na kuziweka siwe mwendokasi.
Pumzika baba aaaaah!
Hukusikia zilikutwa bilioni zaidi ya 100 nyumbani kwake baada ya kufa? Lile lilikuwa jizi km majizi mengine ila alikuwa anajua kufokafoka kuwapumbaza majinga km wewe
 
Pumzika kwa amani baba,kweli tunakukumbuka na ulisema haya,angekuwepo hili lingeisha zamani sana angechukua hata new force buses na kuziweka siwe mwendokasi.
Pumzika baba aaaaah!
Mbona mpaka anakufa NIDA ilimshinda..... niambie na ukali wote ule ni lini waTanzania waliwahi pata vitambulisho vyao on time?
 
Back
Top Bottom