JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Foleni imekuwa kubwa ya abiria kusubiri mabasi, wapo ambao wamelazimika kusubiri mabasi hayo kwa saa tatu.
Upande wa Mabasi ya Mwendokasi yanayotokea Kibaha pia kulikuwa na abiria wengi kwenye vituo, mabasi ni machache na hivyo kusababisha msuguano wakati wa kuingia ndani ya usafiri huku baadhi yakipata tabu mlango kufunga kutokana na mbanano hadi kwenye milango.
Nilitamani kupiga picha nyingi ila nikashindwa baada ya kuona sura za watu zikiwa hazina matumaini, nikaona isiwe tabu ngoja nishudie kwa macho zaidi.
Wiki moja iliyopita viongozi wa Mkoa wa Dar na Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) walinukuliwa wakisema wanashughulikia changamoto hiyo ya uhaba wa magari ili isijirudie.