kupelwa
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 1,087
- 450
Hoja si kuwepo,maana ni mali ya watanzania wote,hoja yake kuwa kama taifa changa,vyema kuzingatia vipaumbele vya miradi ya kipaumbele ya walio wengi kwanza badala ya kuwana uoendeleo kimatabaka.Wazo lako ni zuri sana ila acha kuingiza uchama kwenye maendeleo off course pia hata kwenye maji wangeweza peleka huko vijijini
Lile Daraja naimani IPO siku utapita wewe ama ndugu Yako.
Tanzania yetu usambazaji maji ni 20% tu na hi ipo mijini vijijini hakuna maji,sababu bajeti yetu ni ndogo,usambazaji umeme ni 46% tu ,na hii ni kwa mijini na vijiji vya karibu na mijini,vijiji vingi bado havijafikiwana usambazaji umeme.
Nchi yetu 80% wapo vijijini na ajira kuu kwao ni kilimo,je kilimo leo inachangia kiasi gani? Ni 24% tu kutoka 65% mika ya 1967.,je kama yaifa kwann tuwekw kipaumbele kwenye sekta hiyo inayoajiri walio wengi ili kuinua kioato chao,kuinua pato la nchi,kuinua uchumiwa taifa?
Nchi kama vietnam uchumi wao unaendeshwa na uzalishaji wa zao la mpunga,na wamewekeza sana.Kwann sisi tulio na mazao zaidi ya 100 tusiwekeze huko badala ya daraja ambalo wanaopita pale ni namba ndogo sana na pia baso kuna mbafala wa barabara?
Tuna shule zetu nyingi vijijini,miundo mbinu yake zingine ni mbovu sana,madarasa yanavuja,sakafu zimezeeka,madarasa machache,walimu hawapandi amdaraja,hawana motisha,hawana nyimba wala ofisi,hawana kujiendeleza kitaaluma ,mwisho wake vijana wanafaulu kwenda sekondari hawajui kusoma nabkuandika,wakimaliza kidato cha nne 52% wanaishishi daraja la nne na zero ipi tuwekeze kwenye daraja la watu wachache wakati kuna vijana 52% hawafaulu waoatao 500000 wanabakia hawana cha kufanya na four isiyo na mpango.
Piga hesabu ya mika10 utakuwa idadi ya watu 5m hawana ujuzi,hawna ajira sitahiki na serrwkelai imewatelekeza ,je si walipa kodi?je ai watanzania kwann wasisaidiwe kwanza bafala ya daraja?