Dar na Dodoma: Wafanyabiashara walazimishwa kufunga maduka sababu ya msiba wa Hayati Magufuli

Tunakumiss mkombozi wa wanyonge
IMG_20210322_112913_905.jpg
 
sorry but kiukweli. kuna watu wasipitoka hata siku moja familia haili kabisaa.
kuna watu hali zao ni tete sipotoka watoto hawaendi chooni. so yes kuna msiba lakin kuna familia zilizo na mahitaji.

Tunarudi kwenye saving hata kama unapata 1000 jitahidi 50 usave ili kwa mambo madogo kama haya usitetereke,
 
Kwa hiyo kitendo cha polisi kupita kutangaza kwamba watu wafungue kinaashiria kwamba kulikuwapo katazo la kufungua, maana siku zote watu huwa wanafungua tu bila kusubiri tangazo la polisi
Hakukuwa na katazo ila kuna wahuni inaelekea wakivizia kuiba tu ndo walitoa hiyo taharuki na kweli maeneo ya Agrey maduka ya jumla watu wameibiwa maana mtu mwingine alikuwa hajui kama anasaidiwa au lah kumbe watu wanatoka na vitu vyake alivyoweka mpaka nje
 
Mimi Maghu sikuwa napenda kabisa,
Kifo chake kwa maoni yangu kimeiokoa Nchi na madhara zaidi.
Ila Hilo la kufunga biashara sio kweli,jana nilikuwa posts,Mwenge,kote huko biashara zilikuwa zinaendelea kuanzia Post ferry mpaka Mwenge,aliyefunga alipenda mwenyewe
 
Katika karne hii 21 taifa linaendeshwa kama enzi za ujima. watu wote tunalazimishwa kufikiri sawa, yaani wanataka woote tuhuzunike.
Kisheria siku ya sikukuu au mapumziko huruhusiwi kufungua ofisi,duka au kiwanda ni Sheria tu mkuu,labda uhamie Somalia
 
Cku moja mauzo gani??akivunjwa miguu atauza nn??funika kombe mwanaharamu apite...tutii shetia bila shuruti...mtuwache tumzike jiwe wetu kwa,amani ebooo
We mjinga hujawahi uguliwa mgonjwa wa dialysis kila wiki. Elfu ishirini tu ikiingia ina maana kubwa.

RIP MAGU
 
Katika karne hii 21 taifa linaendeshwa kama enzi za ujima. watu wote tunalazimishwa kufikiri sawa, yaani wanataka woote tuhuzunike.

Hii si sawa. watu woote hawa wamefika makazini hawajui cha kufanya baada ya kufika kazini na kuamlishwa kutawanyika. nakulilia Tanzania yangu.

mhn! nipo mita zisizozidi 400 toka tukio linapofanyika na sijafunga ofisi na wala kuona watu wakilazimishwa kufunga japo utendaji si wasikuzote hata mimi nitafunga muda si mrefu lakini si kwa kulazimishwa bali siku imekaa kimsiba msiba tu.
 
Katika harakati za kupinga pinga. Yaanini ilimradi tu ionekane kuna dosari. Hamjawahi kuweka mema,ni utopolo tu. Upumbavu tu yani.
Kwa akili yako ni sahihi maduka kufungwa? Siku ya msiba watu hawana mahitaji?
 
Mimi ni fundi computer niko kariakoo mtaa wa Lindi na Msimbaz...

Kiukweli kuna habari zilizagaa ghafla kuwa kuna askari wanapita kukamata watu eti kisa wamefungua maduka na leo ni siku ya maombolezo ya kitaifa.. ni kweli watu tumefunga maduka Kariakoo lakini mimi binafsi sikutaka kupokea tu habari bila kuona maana kila unaemuuliza hakuna anaesema amewaona askari wakikikatama wala kufunga maduka zaidi utasikia nimesikia nimesikia...

Niliamua kwenda kituo Msimbazi kupata habari kamili na nikakutana na askari wawili mle ndani nikawauliza wakaniambia hakuna kitu kama hicho na wala wao hawajapokea oda ya kufunga maduka ya watu na wala hawajakataza watu tuendelee na shughuli zetu.
ni kweli nilirudi kufuata kiatu changu nikakutana na maagizo ya askari maduka yafunguliwe
 
Back
Top Bottom