Dar es Salaam: Wakazi Kijijini Mbezi Beach B waigomea Serikali kuhusu kuhama eneo hilo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Wakazi wa eneo la Kijijini lililopo katika Kata ya Kawe, Mtaa wa Mbezi Beach B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wamekahidi kuhama eneo hilo kama ilivyoamuliwa na Serikali.

Wakazi hao walipewa siku 14 za kuhama eneo hilo kwa hiari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Matambule.

Hiyoooo.jpg

Mkuu wa Polisi Kawe (OCD) SP. Deus Shata, (wapili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Kijijini, lililoko Mbezi Beach B, kata ya Kawe, wilayani Kinondoni mwishoni mwa wiki. Wakazi wa eneo hilo walipewa siku 14 na Mkuu wa Wilaya hiyo kuondoka katika eneo hilo lakini wamekaidi. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Kawe, Husna Nondo wengine ni maofisa kutoka idara mbalimbali za Serikali.

Aidha, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kuaminika, inadaiwa kuwa, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, Maafisa kutoka TARURA na DAWASA Novemba 17, walifika katika eneo hilo na kukuta wakazi hao wakiwa hawajatekeleza agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, ambapo, Jeshi hilo liliwataka wakazi hao hadi kufika jana saa 5 asubuhi kuwa wameshahama.

Habari za ndani zinaeleza kwamba badala ya wakazi hao kuhama kwa hiari yao, wameamua kuagiza mganga wa kienyeji kutoka mkoani Mtwara ili awafanyie zindiko wasiweze kuondoka eneo hilo.
use9.jpg

Ficha 1.jpg

Ficha.jpg

use10.jpg

“Kinachoendelea kwa sasa ni wananchi hao kuanza kupimana ubavu na Serikali. Badala ya kuondoka sasa wamemuagiza mganga kutoka Mtwara ili awafanyie zindiko na wanadai kuwa huyo ni Mganga wao ambaye wamekuwa wakimtumia miaka yote,” alisema mtoa habari wetu.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mtambule, aliagiza wakazi hao kuhama eneo hilo kwa hiari ndani ya 14 kama walivyoomba, lakini hadi jana maisha yalikuwa yanaendelea kama kawaida.

Mwishoni mwa wiki Polisi walifika eneo hilo ambapo pamoja na mambo mengine walishuhudia wakazi hao wakiendelea kuishi kwenye vibanda, ambavyo wamekuwa wakitumia kufanya maovu.

Uamuzi wa Serikali kutaka wananchi hao kuhama eneo hilo unatokana na mtandao wa TimesMajira Online hivi karibuni kuibua maovu yanayofanyika katika eneo hilo dogo.

Katika eneo hilo, kuna kaya kati 30-40 ambazo zinaishi katika vibanda vya mabati, ambavyo ndiyo makazi yao ya kudumu kwa takriban miaka 30.

Makazi hayo huyatumia kama sehemu zao za kufanyia biashara haramu, ambazo wao wamezihalalisha. Biashara zinazofanyika katika eneo hilo ni uuzaji wa dawa za kulevya, bangi, pombe haramu ya gongo, pombe za kienyeji na ngono ya nipe nikupe (kununua).

Biashara ya ngono ya nipe nikupe katika eneo hilo, inahusisha wanawake na wasichana wenye umri mdogo. Kinachofanyika ni maelewano na baada ya hapo, maisha yanaendelea.

Wakati wakazi wanaoishi eneo la Kijijini wakiwa wameridhika na maisha ya eneo hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa na nyumba za kudumu jirani ya Kijijini wamezikimbia na kwenda kuishi kwingineko, kwani eneo hilo sio salama kwa malezi ya watoto na kwenye suala zima la maadili.

Mbali na hilo, pia eneo hilo limeonekana kuwa ni hatarishi kwa watoto chini ya miaka 18. Mbali na lugha chafu zinazozungumzwa na wanaofika kupata huduma, lakini kibaya zaidi watu hao wamesahau kwamba kuna vyombo vya dola.

Baada ya TimesMajira kufika eneo hilo, lilishuhudia na kujiridhisha kufanyika kwa biashara haramu na kujionea jinsi watoto wanaoishi jirani wanavyokabiliwa na tishio kubwa la kimaadili.

Chanzo: TimesMajira Online

Pia soma:
= Kijijini, Mbezi Beach eneo hatari Jijini Dar es Salaam
= Dar es Salaam: Wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B wapewa Siku 14 Wahame
= Hatimaye makazi ya baadhi ya wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B (Dar es Salaam) yavunjwa
 
Mmmh hebu ngoja kwanza.

Mtu kaishi miaka 30 ina maana umri huo kama ana mtoto ni myu mzima tayari, so huyo mtoto wa 30yrs old unampeleka wapi na kumwambia hapa ndiyo kwenu?.

Na serikali inakuwa wapi hadi jamii inaishi mazingira hayo kwa 30yrs huku wakiwa na maisha aina hiyo?

La mwisho, wanawafukuza hapo kwa sababu ipi, a) biashara wanayofanya, b) hawapo ktk mfumo mzuri wa ujenzi, c)hao waliokimbia nyumba zao?
 
Kwani Ilo eneo ni la nani hiv unaeza Jenga kibabda tu popote na kuanza kuishi duh ata sielewi
 
Hayo maeneo ni yao mbezi beach karibu yote walikuwa wanakaa wao kabla ya maeneo kuanza kuuzwa na wao kuama hiyo sehemu ndio ilikuwa imebaki lakin hayo ni maeneo yao nashangaa umpe mtu siku 14 aame kwwnye lake sababu ya mtandao fulani kuqndika maovu ya hapo kila sehemu kuna maovu hapo kuna mkubwa fulani itakuwa kashapatamani wanatake advantage
 
Serikali ndiyo inalea upumbavu huo. Yatakiwa ipitishe bull dozer
 
Wakazi wa eneo la Kijijini lililopo katika Kata ya Kawe, Mtaa wa Mbezi Beach B, Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wamekahidi kuhama eneo hilo kama ilivyoamuliwa na Serikali.

Wakazi hao walipewa siku 14 za kuhama eneo hilo kwa hiari na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Matambule.

View attachment 2819503
Mkuu wa Polisi Kawe (OCD) SP. Deus Shata, (wapili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Kijijini, lililoko Mbezi Beach B, kata ya Kawe, wilayani Kinondoni mwishoni mwa wiki. Wakazi wa eneo hilo walipewa siku 14 na Mkuu wa Wilaya hiyo kuondoka katika eneo hilo lakini wamekaidi. Wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Kawe, Husna Nondo wengine ni maofisa kutoka idara mbalimbali za Serikali.

Aidha, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kuaminika, inadaiwa kuwa, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni, Maafisa kutoka TARURA na DAWASA Novemba 17, walifika katika eneo hilo na kukuta wakazi hao wakiwa hawajatekeleza agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, ambapo, Jeshi hilo liliwataka wakazi hao hadi kufika jana saa 5 asubuhi kuwa wameshahama.

Habari za ndani zinaeleza kwamba badala ya wakazi hao kuhama kwa hiari yao, wameamua kuagiza mganga wa kienyeji kutoka mkoani Mtwara ili awafanyie zindiko wasiweze kuondoka eneo hilo.

“Kinachoendelea kwa sasa ni wananchi hao kuanza kupimana ubavu na Serikali. Badala ya kuondoka sasa wamemuagiza mganga kutoka Mtwara ili awafanyie zindiko na wanadai kuwa huyo ni Mganga wao ambaye wamekuwa wakimtumia miaka yote,” alisema mtoa habari wetu.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mtambule, aliagiza wakazi hao kuhama eneo hilo kwa hiari ndani ya 14 kama walivyoomba, lakini hadi jana maisha yalikuwa yanaendelea kama kawaida.

Mwishoni mwa wiki Polisi walifika eneo hilo ambapo pamoja na mambo mengine walishuhudia wakazi hao wakiendelea kuishi kwenye vibanda, ambavyo wamekuwa wakitumia kufanya maovu.

Uamuzi wa Serikali kutaka wananchi hao kuhama eneo hilo unatokana na mtandao wa TimesMajira Online hivi karibuni kuibua maovu yanayofanyika katika eneo hilo dogo.

Katika eneo hilo, kuna kaya kati 30-40 ambazo zinaishi katika vibanda vya mabati, ambavyo ndiyo makazi yao ya kudumu kwa takriban miaka 30.

Makazi hayo huyatumia kama sehemu zao za kufanyia biashara haramu, ambazo wao wamezihalalisha. Biashara zinazofanyika katika eneo hilo ni uuzaji wa dawa za kulevya, bangi, pombe haramu ya gongo, pombe za kienyeji na ngono ya nipe nikupe (kununua).

Biashara ya ngono ya nipe nikupe katika eneo hilo, inahusisha wanawake na wasichana wenye umri mdogo. Kinachofanyika ni maelewano na baada ya hapo, maisha yanaendelea.

Wakati wakazi wanaoishi eneo la Kijijini wakiwa wameridhika na maisha ya eneo hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa na nyumba za kudumu jirani ya Kijijini wamezikimbia na kwenda kuishi kwingineko, kwani eneo hilo sio salama kwa malezi ya watoto na kwenye suala zima la maadili.

Mbali na hilo, pia eneo hilo limeonekana kuwa ni hatarishi kwa watoto chini ya miaka 18. Mbali na lugha chafu zinazozungumzwa na wanaofika kupata huduma, lakini kibaya zaidi watu hao wamesahau kwamba kuna vyombo vya dola.

Baada ya TimesMajira kufika eneo hilo, lilishuhudia na kujiridhisha kufanyika kwa biashara haramu na kujionea jinsi watoto wanaoishi jirani wanavyokabiliwa na tishio kubwa la kimaadili.

Chanzo: TimesMajira Online

Pia soma:
= Kijijini, Mbezi Beach eneo hatari Jijini Dar es Salaam
= Dar es Salaam: Wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B wapewa Siku 14 Wahame
Mganga wao atachemsha,Mungu hapingwi na mganga!
 
Unajua media ss wenyewe we are not fare,tunaambiwa wameligeuza eneo Hilo kuwa kichaka Cha maovu for 30 yrs.Je Miaka yte hiyo serikali walikuwa vipofu,na huyu DC wa Sasa hivi ndio ana macho makubwa?Siwezi shabikia maana naweza unga mkono watoke kesho unakuta limejengwa casino.
 
Wanalipwa fidia au watajijua wenyewe 🤔🤔 wakiwaondoa hapo ndio hizo shughuli haramu watakua wame zimaliza 🤔🤔 wana uhakika gani kwamba hawata zifanya huko waendako 🤔🤔 hicho wanacho fanya ni uhalifu kwa nini wasikamatwe na kufunguliwa mashtaka 🤔🤔 serikali ilikua wapi miaka yote hiyo watu wanaishi kwenye mazingira ya ajabu kiasi hicho katikati ya jiji 🤔
 
Hao naona hawajui nguvu za serikali. Juzi kati hapa nilishuhudia serikali ikitumia nguvu kubwa ikiwa na askari wake waliojizatiti kwa silaha kali za moto kusimamia tingatinga libomoe vibanda vya wajasiriamali wadogo ikidai wamejenga kwenye hifadhi ya barabara na wanataka kuipanua. Cha ajabu kwa nini watumie ulinzi mkali wa askari polisi wenye bunduki, kwani hao wajasiriamali watabisha kuondolewa?. Sasa hao wanakiji wa mbezi bora waondoke tu kwa hiari yao wasisubiri tingatinga lije likiwa na askari wa kutosha kukabiliana nao
 
Aiseeh kweli Tanzania bado maskini Sana kwa mazingira hayo duh
Hilo eneo mbona la kitambo sana
Uswaz imepitiliza
Dar hii kuna maeneo unaweza mwambia mtu kama yapo na ukashangaa,kuna eneo mbunge,mkuu wa mkoa wenyewe hawajawahi kutia
Mguu
Watu wanaishi huko na kuna utawala wao huko
Dar kuna sehemu inaitwa sogodo huko ni hatari,uhuni wote uko huko
Maisha ni ya ovyo kupitiliza

Ova
 
Back
Top Bottom