JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Utekelezaji wa zoezi la ubomoaji ulianza mapema alfajiri ya Desemba 9, 2023 bila kujali mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, huku likitekelezwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa.
Wakati zoezi hilo likiendelea wakazi wa eneo hilo walisikika wakilia huku kukiwa kwenye hekaheka ya kujaribu kuokoa kinachowezekana bila kujali mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha alfajiri.
“Tumeponzwa na hawa viongozi uchwara, waliotuambia hatutaondoka sababu wao ndo “wenye duka (CCM)” Mkuu wa Wilaya ni msimamizi tu wa duka, sasa leo msimamizi wa duka ndio kasimamia duka, sasa hapo nani zaidi?” aliongea kwa hasira mwanaume huyo.
TimesMajira online ilishuhudia zoezi la ubomoaji likiendelea huku kukiwa na hekaheka za kuokoa vitu mbalimbali.
Katika ubomoaji huo, walikuwepo Wafanyakazi wa Halmashauri wakisimamia na kukusanya mabati na mbao na kupakia katika moja ya lori lenye namba za usajili SM12739.
Nao askari wa Jeshi la Polisi waliokuwa wakisimamia zoezi hilo walipoulizwa kuhusu mwenendo wa zoezi hilo, walisema hapakuwa na upinzani wowote, wala kizuizi chochote na kwamba wakazi hao walitoa ushirikiano kwa kukusanya wenyewe vitu vyao.
“Hakuna vurugu yoyote, hakuna upinzani wala aliyekaidi, sisi kama polisi tuko hapa kuhakikisha kuna amani na zoezi hili linakamilika bila ubishi wala kikwazo chochote” alisema mmoja wa askari ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa madai kuwa sio msemaji wa jeshi hilo.
Chanzo: Times Majira
Pia soma >
= Dar es Salaam: Wakazi wa Kijijini Mbezi Beach B wapewa Siku 14 Wahame
= Kijijini, Mbezi Beach eneo hatari Jijini Dar es Salaam
= Dar es Salaam: Wakazi Kijijini Mbezi Beach B waigomea Serikali kuhusu kuhama eneo hilo