Current four star Generals in Tanzania

Current four star Generals in Tanzania

Yaani Clinton na Gore, ambao ni Democrats, walimbagua General Colin Powell?

Haiwezekani bana. Democrats siyo wabaguzi. Wanawapenda watu weusi.
Nyani Ngabu, inawezekana sana tuu, Gen. Powell alikuwa Republican. Kwa Marekani misimamo ya Vyama vyao vina nguvu sana hata kwenye Supreme Court appointments .
 
..nakubaliana na wewe.

..na kukazia hoja yako naomba msome document ya CIA hapo chini kuhusu mabadiliko ya CoS wa Jwtz yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere.



" PRESIDENT NYERERE JULY 10 ANNOUNCED SERIES OF SHIFTS IN TANZANIAN MILITARY COMMAND, AS FOLLOWS:

BRIGADIER TUMAINIEL NDERANGUSHO KIWELU IS NAMED CHIEF OF STAFF OF TANZANIAN PEOPLE DEFENSE FORCE (TPDF), REPLACING BRIGADIER SIMON NKWERA, WHO BECOMES MANAGING DIRECTOR THE NEWLY CREATED RUFIJI DEVELOPMENT AUTHORITY.

COLONEL MIKE MARWA IS PROMOTED TO BRIGADIER AND NAMED COMMANDER OF THE TPDF SOUTHERN BRIGADE, REPLACING BRIGADIER KIWELU.

COLONEL A. SIMBA IS NAMED TANU PARTY SECRETARY OF WEST LAKE REGION (AND, IPSO FACTO, REGIONAL COMMISSIONER), REPLACING COLONEL MARWA.

MR. MOSES NNAUYE, TANU SECRETARY OF SINGIDA REGION (AND NOW CONFIDENTIAL CONFIDENTIAL
IS NAMED CHIEF POLITICAL EDUCATION OFFICER IN THE TPDF, REPLACING COLONEL SIMBA.

2. BEGIN CONFIDENTIAL.
COMMENT: BRIGADIER NKWERA HAS BEEN KICKED OUT TO A MILITARILY INCONSEQUENTIAL JOB, THUS REFLECTING AN APPARENT VICTORY FOR COMMANDER IN CHIEF MAJOR GENERAL ABDULLAH TWALIPO, WITH WHOM NKWERA HAS BEEN QUARRELING FOR SOME TIME, THOUGH WE DO NOT YET KNOW WHOLE STORY.

KIWELU IS DISTINCTLY A RISING YOUNG STAR, AND PRESUMABLY A PROTAGE OF TWALIPO. HE WAS A LIEUTENANT COLONEL COMMANDING THE FOURTH BATTALION AT NACHINGWEA WHEN HE WAS JUMP-PROMOTED TO BRIGADIER AND NAMED COMMANDER OF THE SOUTHERN BRIGADE LAST FEBRUARY 9. PREVIOUSLY HE HAD SERVED AS COMMANDER OF THE MONDULI TANU MILITARY ACADEMY.

IT IS NOT KNOWN WHY A NEW TANU SECRETARY (REGIONAL COMMISSIONER) HAS BEEN NAMED FOR WEST LAKE REGION. THIS REGION, WHICH BORDERS ON UGANDA, IS CONSIDERED MILITARILY AND POLITICALLY SENSITIVE, AND ITS LEADERS ARE CHOSEN WITH MORE THAN USUAL CARE. "

cc Nyani Ngabu, Pascal Mayalla
Thanks for this.
P
 
Elezea kwa upana, mara zote kwa tulivyo zoea nchini, yakifanyika mabadiliko ya CDF na CoS hubadilika. Na hii ni kwa kuwa Ma CoS ndio huwa CDF, kwa hiyo nafasi ya CoS huwa wazi.

...mwanzo nilikuwa sijakuelewa, ila hapa umeeleza vizuri.
 
Ahaa! Well nimekuelewa vizuri Mkorinto. Kama hutojali, naomba unipangie uzito from JWTZ to Mgambo.

Like;- JWTZ, JKT, Polisi, FFU and co.
JKT iko ndani ya JWTZ.

FFU iko ndani ya Police (ni Unit ya Police kama ilivyo Traffic police).

1. JWTZ,
2. Police, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto (level moja)
3. Mgambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Field Marshal ana nyota 5?!!?? Kwa nini rank hito Tanzania hatuna?!
Field Marshal kiuhalisia siku hizi hicho cheo ni almost hakuna, mara ya mwisho walikuwepo world war 2 huko, maana unakuta jeshi lina watu milion 4. Sasa hivi hakuna hayo mambo, na sidhani kama yatatokea
 
Naunga mkono hoja, maslahi yanafanana with tofauti ndogo
P
Nimekuelewa na kukubali, lakini naamini ilikuwa rahisi sana kwa kuwa Aliopo ndio mmoja wa Maafisa wenye elimu ya juu na mafunzo makubwa Jeshini. Lakini hiyo hiyo Elimu na Mafunzo ya juu yali mchelewesha kupendekezwa kwa nafasi za juu.
 
Nasikia JWTZ huwa hamna surprise yani wameshajipanga wenyewe na wanajua nani akistaafu CDF anakuwa nani.
 
Hujamfafanulia vizuri,
Unaposema Brigadiier Ana nyota 1 atadhani Ni moja Kama ya Luteni Usu,
Nyota mbili atadhani Ni Luten kamaili,
Nyota tatu atadhani Ni Captain.
Ingekua vizuri umwambie kuwa Brigadiier Ana alama Fulani ikiambatana na nyota kadhaa.Na kuendelea.
Tusaidie Mkuu.
Ni kweli, nilidhani anaongelea kwenye ranks za generals peke yake. Mayalla kaelezea vizuri hapo juu
 
Kwenye military organizations, hivi vyeo vya officers ni vyeo vya uongozi wa wanajeshi wenzake. Kama hauna jeshi kubwa sana, 4 star generals hawahitajiki. Jeshi letu bado dogo kwa idadi ya wanajeshi, pengine itafika siku kutakuwa na huo uhitaji.
Sio kwamba jeshi letu bado dogo,huo ni mfumo wetu wa namna ya kulifanya jeshi liwe na utii,
 
Hakuna figisu yoyote ya kumuondoa Mabeyo, cheo cha CDF kina security of tenure ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano kama alivyo Gavana wa BOT, CAG, etc, rais yoyote akija hawezi kuwaondoa na kuleta watu wake.
Hili sio tuu la hakuna Mzanzibari mwenye sifa ya kuwa CDF, kati ya ma CDF, mwenye jina la Kiislamu ni mmoja tuu, Abdallah Twalipo, na sijui ni jina tuu, au alikuwa Muislamu kweli, maana binti yake Flora, tumesoma nae primary alikuwa Mkristo.

Hili nililiulizia hapa
P
Mkuu unaweza kutusaidia elimu ya Mabeyo ?,
 
JKT iko ndani ya JWTZ.

FFU iko ndani ya Police (ni Unit ya Police kama ilivyo Traffic police).

1. JWTZ,
2. Police, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto (level moja)
3. Mgambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mgambo ni kamandi iko chini ya MMJ na kuna Brigedia ndo anaisimamia mkuu au mie nimepitwa???(RFC)

Na inashuka mpaka mikoani kote wa RC(Defence attaçhe mkoani,Mshauri wa mgambo mkoa na Wanakuwaga maMajor) na wilayani kuna Mshauri wa mgambo pale kwa DC ambaye ni mjumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama

Mgambo sema tu hawana kazi maalum wakaanza kupewa kazi za kupiga mateke sufuria za ubwabwa wa mama ntilie ndomaana tunawaona sio

Ila kipindi Fulani hapo nyuma(Nadhani hata mwanzoni kwa utawala wa Mkapa) ilikua Mgambo ni bora kuliko Polisi😂😂. Enzi zile polis wanavaa sare zina viraka na raba
 
Mtu kijana ni range ya umri gani?

Mtu akiwa luteni usu na miaka24, ukiongezea na hiyo 24 mingine uliyoitaja, by 48 au 49 anaweza akawa full general?

Mtu mwenye miaka 48 ni mzee?
Sijui utamwitaje , tunayo fahamu sisi kijana mwisho miaka 35-40.
 
Sio kwamba jeshi letu bado dogo,huo ni mfumo wetu wa namna ya kulifanya jeshi liwe na utii,
Sababu pia Jeshi ni dogo mkuu. Kamandi zenyewe ziko 6 ambazo zina askari labda 30,000 kila moja

Sio kama India, US au China ambako watu wanalinganisha sana
 
Nyani Ngabu,

..nadhani uko sahihi.

..lakini kupata uhakika zaidi tuwaite Kichuguu, Echolima, Pascal Mayalla.

..Ninavyoelewa mimi kwa, JWTZ, askari mwenye cheo cha juu kabisa, au mkuu wa majeshi, huwa na rank ya Jenerali / 4-star-general.

..Utaratibu wa Cdf kuwa 4-star-general ulianza miaka ya mwisho ya Mwalimu Nyerere, na mwanzoni mwa utawala wa Ali Hassan Mwinyi.

..wakati jeshi la wananchi limeundwa, mkuu wa majeshi wa kwanza alikuwa na cheo cha Brigadier au 1-star-General.

..baadae nadhani kutokana na jeshi kuwa kubwa zaidi mkuu wa majeshi akawa na cheo cha Major General au 2-star general.

..Utaratibu huo uliendelea mpaka wakati wa vita vya kagera, ambapo mkuu wa majeshi akawa na rank ya Lieutenant General au 3-star general.

..Wakati Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, alitoa nishani kwa maafisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama, na akawavalisha rank za 4-star-General, Abdalah Twalipo, na David Musuguri, in that order. Lakini Abdalah Twalipo alikuwa hayuko tena jeshini, Musuguri ndio alikuwa mkuu wa majeshi.

..Baada ya General Musuguri kustaafu, wakuu wote wa majeshi waliomfuatia wamekuwa na rank ya 4-star-General.

NB:

..Tumainieli Kiwelu ndiye 4-star-General pekee hapa Tanzania ambaye hajashika nafasi ya mkuu wa majeshi / cdf. Vilevile Tumainieli Kiwelu ndiye Mtanzania pekee ambaye amewahi kuwa mnadhimu mkuu / CoS chini ya Maraisi, na wakuu wa majeshi, wawili tofauti. Mara ya kwanza ilikuwa chini ya Rais Nyerere na CDF Abdalah Twalipo; mara ya pili ilikuwa chini ya Rais Mwinyi na CDF Ernest Mwita Kiaro.

..Pia Raisi Mkapa alimpandisha cheo Mkuu wa kwanza wa Jwtz, Major General Mirisho Hagai Sarakikya kuwa 4-star-general miaka kadhaa baada ya Sarakikya kuwa ameshaondoka jeshini.

Halafu Sarakikya alipata mtelemko ambao ni nadra sana kutokea. Alipandishwa cheo kutoka lieutenant mpaka brigadier na kufanywa kuwa mkuu wa majeshi. Hivyo, hakuwahi kuwa captain, major, lieutenant colonel wala colonel. Miaka hii hilo haliwezi kutokea!
 
Mkuu unaweza kutusaidia elimu ya Mabeyo ?,
Duu!, swali hili limenifanya nijitafakari sana, mimi ni Msukuma wa aina gani, kwasababu japo Mabeyo, tunatoka naye kijiji kimoja, Masanza, nyumbani kwake na kwetu ni just accros the main road, lakini huwezi amini, sijawahigi hata kujua alipandaje ghafla na kuwa generali, wala siijui CV yake, nasikia ni highly learned, and he is good!.
P
 
Yeah kwa wakati mmoja general ni mmoja ambaye anakuwa ni CDF au mkuu wa majeshi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom