Nyani Ngabu,
Nadhani uko sahihi.
Lakini kupata uhakika zaidi tuwaite
Kichuguu,
Echolima,
Pascal Mayalla.
Ninavyoelewa mimi kwa, JWTZ, askari mwenye cheo cha juu kabisa, au mkuu wa majeshi, huwa na rank ya Jenerali / 4-star-general.
Utaratibu wa Cdf kuwa 4-star-general ulianza miaka ya mwisho ya Mwalimu Nyerere, na mwanzoni mwa utawala wa Ali Hassan Mwinyi.
wakati jeshi la wananchi limeundwa, mkuu wa majeshi wa kwanza alikuwa na cheo cha Brigadier au 1-star-General.
Baadae nadhani kutokana na jeshi kuwa kubwa zaidi mkuu wa majeshi akawa na cheo cha Major General au 2-star general.
Utaratibu huo uliendelea mpaka wakati wa vita vya kagera, ambapo mkuu wa majeshi akawa na rank ya Lieutenant General au 3-star general.
Wakati Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, alitoa nishani kwa maafisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama, na akawavalisha rank za 4-star-General, Abdalah Twalipo, na David Musuguri, in that order. Lakini Abdalah Twalipo alikuwa hayuko tena jeshini, Musuguri ndio alikuwa mkuu wa majeshi.
Baada ya General Musuguri kustaafu, wakuu wote wa majeshi waliomfuatia wamekuwa na rank ya 4-star-General.
NB:
Tumainieli Kiwelu ndiye 4-star-General pekee hapa Tanzania ambaye hajashika nafasi ya mkuu wa majeshi / cdf. Vilevile Tumainieli Kiwelu ndiye Mtanzania pekee ambaye amewahi kuwa mnadhimu mkuu / CoS chini ya Maraisi, na wakuu wa majeshi, wawili tofauti. Mara ya kwanza ilikuwa chini ya Rais Nyerere na CDF Abdalah Twalipo; mara ya pili ilikuwa chini ya Rais Mwinyi na CDF Ernest Mwita Kiaro.
Pia Raisi Mkapa alimpandisha cheo Mkuu wa kwanza wa Jwtz, Major General Mirisho Hagai Sarakikya kuwa 4-star-general miaka kadhaa baada ya Sarakikya kuwa ameshaondoka jeshini.