Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,225
- 113,565
Mimi si mjeda. Sijui mengi kuhusu ujeda. Sijui mengi kuhusu mengi.
Ni mbeba maboksi tu. Wengine husema nimeishia darasa la saba. Wengine hudai nimeishia kidato cha nne.
Hivyo, sina mengi niyajuayo. Ila, ninao uungwana wa kukubali nisiyoyajua.
Na dawa ya kuyajua usiyoyajua ni kujifunza.
Kujifunza kuko kwa namna nyingi. Moja ya hizo namna ni kuuliza.
Leo nauliza hivi: Hivi kwa Tanzania huwa tuna jenerali mmoja tu kwa wakati mmoja aliye jenerali kamili, yaani yule mwenye nyota 4?
Kama sijakosea, mkuu wa majeshi ndo huwa jenerali kamili mwenye nyota 4 tu kwa wakati mmoja. Jenerali huyo akistaafu ndo mwingine [labda luteni jenerali] anapandishwa cheo na kuwa jenerali kamili halafu ndo anakuwa mkuu wa majeshi.
Kwa nini iko hivyo? Tumeiga sehemu labda?
Najua India kwa mfano, kuna four star generals zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.
Marekani currently wana four star generals 45, kama sijakosea.
Kwa mnaojua, kwa heshima na taadhima zote, naomba mnifute huu ujinga nilionao.
Shukran jazilan 🙏.