Current four star Generals in Tanzania

Current four star Generals in Tanzania

Hapa ndio mimi huanza kuchanganyikiwa! Samahani nipatie elimu...

Tanzania People's Defence Forces ndio JWTZ ambayo ndani yake ndio kuna Police Tanzania, Magereza, Fire, JKT na majeshi ya Anga, Maji na Special Forces?

Kama unaweza naomba unipatie orodha kamili ya majeshi yote na vitengo.

mkuu usichanganyikiwe.

kuna jeshi la ulinzi la wananchi(jwtz)anga,ardhi,maji.
kuna jeshi la kujenga taifa(jkt)
kuna jeshi la polisi tz(pt)
kuna jeshi la magereza(tp)

tunapotaja majeshi duniani kwa maana yake kwa ujumla basi tanzania tutataja jwtz(tpdf)na si mengine niliyoorodhesha hapo.lakini katiba yetu imeyaongeza hayo kwa makusudi ile ile ya angalau kujazia nyama kidogo just icase kimehappen,(majeshi ya akiba).
hayo si komandi wala vikosi vya jwtz ila ni akiba ya jwtz,isipokuwa jkt ambayo kwa sasa ni sehemu ya jwtz.
 
Niongezee swali hivi jenerali na meja jenerali yupi mkubwa?
Naanzia kwenye nyota
  • Luteni usu(nyota moja)
  • Luteni (nyota mbili)
  • Captain (nyota tatu)
  • Major (bibi na bwana)
  • Luteni Kanali (bibi na bwana na nyota moja)
  • Kanali (bibi na bwana na nyota mbili)
  • Brigedia jenerali (bibi na bwana, nyota moja na mkasi)
  • Major jenerali (bibi na bwana, nyota mbili na mkasi)
  • Luteni Jenerali (bibi na bwana, nyota tatu na mkasi)
  • mkuu ww majeshi (bibi na bwana, nyota nne na mkasi)
Nina amini una akili, na jibu utakuwa umelipata
 
Niongezee swali hivi jenerali na meja jenerali yupi mkubwa?
Naanzia kwenye nyota
  • Luteni usu(nyota moja)
  • Luteni (nyota mbili)
  • Captain (nyota tatu)
  • Major (bibi na bwana)
  • Luteni Kanali (bibi na bwana na nyota moja)
  • Kanali (bibi na bwana na nyota mbili)
  • Brigedia jenerali (bibi na bwana, nyota moja na mkasi)
  • Major jenerali (bibi na bwana, nyota mbili na mkasi)
  • Luteni Jenerali (bibi na bwana, nyota tatu na mkasi)
  • Jenerali - mkuu ww majeshi (bibi na bwana, nyota nne na mkasi)
 
NN kama unafuatilia vizuri kunapokuwepo na mabadiliko ya CDF huwa yanagusa CoS (Chief of staff)

Maana yake ni kumpa mteuzi nafasi ya kuteua miongoni mwa wenye sifa.

Sasa kama CoS ni Lt General halafu ukamteua mwingine kuwa CDF unadhani itakuwa na picha gani?
 
Nyani Ngabu,

..nadhani uko sahihi.

..lakini kupata uhakika zaidi tuwaite Kichuguu, Echolima, Pascal Mayalla.

..Ninavyoelewa mimi kwa, JWTZ, askari mwenye cheo cha juu kabisa, au mkuu wa majeshi, huwa na rank ya Jenerali / 4-star-general.

..Utaratibu wa Cdf kuwa 4-star-general ulianza miaka ya mwisho ya Mwalimu Nyerere, na mwanzoni mwa utawala wa Ali Hassan Mwinyi.

..wakati jeshi la wananchi limeundwa, mkuu wa majeshi wa kwanza alikuwa na cheo cha Brigadier au 1-star-General.

..baadae nadhani kutokana na jeshi kuwa kubwa zaidi mkuu wa majeshi akawa na cheo cha Major General au 2-star general.

..Utaratibu huo uliendelea mpaka wakati wa vita vya kagera, ambapo mkuu wa majeshi akawa na rank ya Lieutenant General au 3-star general.

..Wakati Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, alitoa nishani kwa maafisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama, na akawavalisha rank za 4-star-General, Abdalah Twalipo, na David Musuguri, in that order. Lakini Abdalah Twalipo alikuwa hayuko tena jeshini, Musuguri ndio alikuwa mkuu wa majeshi.

..Baada ya General Musuguri kustaafu, wakuu wote wa majeshi waliomfuatia wamekuwa na rank ya 4-star-General.

NB:

..Tumainieli Kiwelu ndiye 4-star-General pekee hapa Tanzania ambaye hajashika nafasi ya mkuu wa majeshi / cdf. Vilevile Tumainieli Kiwelu ndiye Mtanzania pekee ambaye amewahi kuwa mnadhimu mkuu / CoS chini ya Maraisi, na wakuu wa majeshi, wawili tofauti. Mara ya kwanza ilikuwa chini ya Rais Nyerere na CDF Abdalah Twalipo; mara ya pili ilikuwa chini ya Rais Mwinyi na CDF Ernest Mwita Kiaro.

..Pia Raisi Mkapa alimpandisha cheo Mkuu wa kwanza wa Jwtz, Major General Mirisho Hagai Sarakikya kuwa 4-star-general miaka kadhaa baada ya Sarakikya kuwa ameshaondoka jeshini.
👍👍
 
Ni kweli unachokisema. Ninaona unaliangalia suala hili kwa mtazamo wa US au India ambako military ni independent institution. Hapa tunazungumzia developing countries

Si lazima awe miongoni mwa hao 4 star generals lakini kumbuka kuwa uteuzi nje ya hao ni uteuzi wa chini kuwa mkubwa. Kutakuwa na chuki.

Fikiria hivi, kuna 4 star generals wanne ambao ni ''CDF in waiting''
Uteuzi wa CDF ukamchukua Luteni jenerali, hivi hawa 4 star watajisikiaje?
Kutakuwa na stability kweli ukijua hizi ni developing countries?

Ukinisoma vizuri nimesema kuna suala la 'merits na appointment'' . Appointment ni kisiasa zaidi.
Lakini Nguruvi....mara nyingi four star generals huwa ni wenye umri mkubwa. Wengi huwa wamebakiza muda mchache sana kabla ya kustaafu.

Kama waliopo kwenye active duty wote wanakaribia kustaafu, kuna ubaya gani wa kumchagua luteni jenerali aliye na umri utaomuwezesha kuhudumu kwa muda wa kutosha na kumpandisha cheo kuwa four star general?

Halafu, nadhani hata maslahi yao huwa hayatofautiani sana.

Yaani majenerali wazima wamuonee gere luteni jenerali aliyepandishwa cheo na kuwa jenerali na mkuu wa majeshi huku wao wakiwa wamebakiza muda mchache kabla ya kustaafu?

Mkuu wa majeshi ana maslahi gani ya kipekee yaliyo tofauti sana na ya majenerali wenzake?
 
Duuh ila huko marekani mkuu wa mageshi ni five star general ndio maana kuna four star generals 45 kama unavyosema hapa.
Hmm acha fiksi bana.

General Mark Milley mbona ni 4 star general...
 
NN kama unafuatilia vizuri kunapokuwepo na mabadiliko ya CDF huwa yanagusa CoS (Chief of staff)

Maana yake ni kumpa mteuzi nafasi ya kuteua miongoni mwa wenye sifa.

Sasa kama CoS ni Lt General halafu ukamteua mwingine kuwa CDF unadhani itakuwa na picha gani?
Sidhani kama italeta picha mbaya.

Naona ni sawa tu.

La sivyo, wangeweka utaratibu wa Chief of Staff kuwa ndo next in line....

Kwa sasa inafanyika hivyo kiutamaduni tu, si kisheria.
 
mkuu usichanganyikiwe.

kuna jeshi la ulinzi la wananchi(jwtz)anga,ardhi,maji.
kuna jeshi la kujenga taifa(jkt)
kuna jeshi la polisi tz(pt)
kuna jeshi la magereza(tp)

tunapotaja majeshi duniani kwa maana yake kwa ujumla basi tanzania tutataja jwtz(tpdf)na si mengine niliyoorodhesha hapo.lakini katiba yetu imeyaongeza hayo kwa makusudi ile ile ya angalau kujazia nyama kidogo just icase kimehappen,(majeshi ya akiba).
hayo si komandi wala vikosi vya jwtz ila ni akiba ya jwtz,isipokuwa jkt ambayo kwa sasa ni sehemu ya jwtz.
Ahaa! Well nimekuelewa vizuri Mkorinto. Kama hutojali, naomba unipangie uzito from JWTZ to Mgambo.

Like;- JWTZ, JKT, Polisi, FFU and co.
 
Lakini Nguruvi....mara nyingi four star generals huwa ni wenye umri mkubwa. Wengi huwa wamebakiza muda mchache sana kabla ya kustaafu.

Kama waliopo kwenye active duty wote wanakaribia kustaafu, kuna ubaya gani wa kumchagua luteni jenerali aliye na umri utaomuwezesha kuhudumu kwa muda wa kutosha na kumpandisha cheo kuwa four star general?

Halafu, nadhani hata maslahi yao huwa hayatofautiani sana.

Yaani majenerali wazima wamuonee gere luteni jenerali aliyepandishwa cheo na kuwa jenerali na mkuu wa majeshi huku wao wakiwa wamebakiza muda mchache kabla ya kustaafu?

Mkuu wa majeshi ana maslahi gani ya kipekee yaliyo tofauti sana na ya majenerali wenzake?
Kwa US ndivyo ilivyo , kwa developing countries kuna tatizo NN. Hapa kuna promotion and demotion at the same time. Kiongozi anayeteua hatakuwa comfortable kwasababu haelewi kama kuna 'reservations' katika military brass , kitu ambacho hakuna anayekitaka.

Unakumbuka Nigeria? The master mind of '' coup de tat ' kuanzia Yakub Gowon, Murtalla Muhamed etc alikuwa Sani Abacha. Mwisho akaona isiwe tabu ni zame yake!
Sidhani kama italeta picha mbaya.

Naona ni sawa tu.

La sivyo, wangeweka utaratibu wa Chief of Staff kuwa ndo next in line....

Kwa sasa inafanyika hivyo kiutamaduni tu, si kisheria.
Hakuna sheria ila kwa kiongozi yoyote ili awe na amani lazima awe na watu anaokuwa 'confortable' nao

In fact CoS ndiye the next kwa kuangalia merits lakini je, kiongozi anayefanya ''appointment' yupo comfortable?

NN unaangalia zaidi merits kama wanavyofanya huko US, lakini US mambo mengi yanafanyika katika jeshi
Kwa developing countries kuna merits na appointment. Hapa usisahau appointment ni kumpa mteuzi 'amani' ya kutafuta mtu wa kufanya naye kazi.
 
Mjeda pekee aliyekuwa Jenerali bila kuwa CDF ni Tumainieli Kiwelu
View attachment 1754602

Mimi si mjeda. Sijui mengi kuhusu ujeda. Sijui mengi kuhusu mengi.

Ni mbeba maboksi tu. Wengine husema nimeishia darasa la saba. Wengine hudai nimeishia kidato cha nne.

Hivyo, sina mengi niyajuayo. Ila, ninao uungwana wa kukubali nisiyoyajua.

Na dawa ya kuyajua usiyoyajua ni kujifunza.

Kujifunza kuko kwa namna nyingi. Moja ya hizo namna ni kuuliza.

Leo nauliza hivi: Hivi kwa Tanzania huwa tuna jenerali mmoja tu kwa wakati mmoja aliye jenerali kamili, yaani yule mwenye nyota 4?

Kama sijakosea, mkuu wa majeshi ndo huwa jenerali kamili mwenye nyota 4 tu kwa wakati mmoja. Jenerali huyo akistaafu ndo mwingine [labda luteni jenerali] anapandishwa cheo na kuwa jenerali kamili halafu ndo anakuwa mkuu wa majeshi.

Kwa nini iko hivyo? Tumeiga sehemu labda?

Najua India kwa mfano, kuna four star generals zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.

Marekani currently wana four star generals 45, kama sijakosea.

Kwa mnaojua, kwa heshima na taadhima zote, naomba mnifute huu ujinga nilionao.

Shukran jazilan .
 
Hatuna uwezo wa kuwahudumia,hao uhudumiwa mpaka siku ya mazishi.
 
Chairman of the Joints Chiefs of Staff.

View attachment 1754636
Mwamba sana Gen. Mark Milley.

Naukumbuka huu ujumbe wake wakati Nkurunzinza wenu Trump akihisiwa angelitumia jeshi kama hatua yake ya mwisho kung'anga'ania madarakani.

"We are unique among militaries. We do not take an oath to a king or a queen, a tyrant or a dictator. We do not take an oath to an individual. No, we do not take an oath to a country, a tribe or religion. We take an oath to the Constitution. And every soldier that is represented in this museum, every sailor, airman, Marine, Coast Guardsman, each of us will protect and defend that document, regardless of personal price,"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom