CPA ya Tanzania ni ya kipekee duniani

Hii kitu niliwahi bishna na mtu hadi nikampia mawe. Mbona Mainjinia, wanasheria na madaktari hawana huu ujinga
Mkuu kwenye kazi hizi ulizotaja zina hatari ndani yake(hazardous, fatal) ndio maana hakuna shortcut yake.
Ukiwa mwanasheria feki utawahukumu/kuwafunga wasio na hatia, ukiwa Daktari feki utawaua wagonjwa kwa kuwapa tiba isiyo sahihi, ukiwa Engineer feki utaangusha majengo na kuua watu.
Lakini taaluma ya mahesabu ya pesa hatari yake ni ya kukimbia na mapene tu na kula maisha mbele kwa mbele.
 
Elimu ya Tanzania haiishi vituko.

Ndio maana hatuendelei. Maana flaw kwenye mifumo yetu ya elimu ni mingi mno.

Ndio maana unashangaa, unakua na CPA ya Tanzania, ukitaka kufanya mitihani ya ACCA hupati exemptions kwa kua CPA yetu haieleweki.

Kwa wahasibu watanielewa, ni rahisi Tanzania kupata CPA hata kama wewe sio mhasibu na huna taaluma ya uhasibu, ili mradi tu ufaulu mitihani yake.

Yaani unaweza kua Certified Public Accountant huku huna academic qualification ya accountancy.

Kwa nchi nyingine kitu cha kwanza kupata CPA ni lazima uwe na academic qualifications then uombe kua certified. Nchi nyingine lazima uwe na module hours nyingi sawa na masters ili uwe eligible na CPA.

Huku mwetu unaweza kumaliza form four, ukaanza na atecs hadi CPA.

Sasa imetokea shida ofisini kwetu, wanataka senior accountant, awe na bachelor degree na CPA, aliyepo ana CPA ila hana bachelor degree, ni form four leaver, aliajiriwa kama accounts clerk.

Ikija kigezo cha CPA anayo, ikija kigezo cha bachelor degree hana. Unajiuliza mtu anakuaje certified public accountant huku hana academic qualification ya accountancy?

Ni sawa na mtu kua registered electrical engineer huku hajasoma hata certificate ya umeme. Mradi tu amelipia na amefaulu mitihani.

Certification ni profession, na ili uwe professional lazima uwe na academic qualifications kwanza. Hapa Bongo unakua certified profession without academic qualifications. Mambo ya hovyo kabisa.

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.
Totally agree, ila watatusikia??!!!
 
Japo mm ni mhasibu ila kiukweli taaluma yetu imeingiliwa. Ukiwa na pesa na muda wa kupitia past papers tayari ww ni mhasibu aliyehidhinishwa. Pia ninaye classmate yuko tanapa nilisoma naye akafeli fomu4 wakati si sisi tunaenda advanced yeye a kaanza ATEC.... Leo hii ni mhasibu mzito uko.
Taaluma pekee tz ambayo haijaanza kutiwa najisi ni taaluma ya sheria na udaktari.... Vingine ni ukanjanja tu

Umeshakutana na wanasheria na majaji wa kizazi cha sasa? Ni majanga!
Ushakitana na madaktari wetu huko mahispitalini?
Kwa kifupi taaluma zote ni najisi tu including sheria na medicine
 
Mkuu
Ndio maana nasema hii elimu ya cpa ni elimu ya kijinga, sasa kama vilaza kama wewe mnapata cpa kuna haja gani ya kua na hiyo elimu.
Kwa maelezo yako ulivyo mjinga basi zifutwe taaluma za uhasibu vyuo vikuu, maana kama unaweza kua mhasibu bila kwenda chuo kikuu, unaweka taaluma ya chuo kikuu ili iweje? Ni sawa na bodi ya uhandisi ianzishe mfumo wa mitihani, kwamba ufanye tu mitihani ufaulu hata kama hujasomea uhandisi chuo kikuu, ili mradi umefaulu mitihani basi wewe ni mhandisi, sasa kutakua na haja gani ya kua na taaluma za uhandisi vyuo vikuu.
Unaongelea kufundisha ndio unajiona mjanjaaa? Kukarili maswali ya acca na majibu yake na kufundisha vilaza wenzio ndio unajiona mjanja, hovyo kabisa.
Ndio maana nasema huu mfumo wa cpa umesababisha vilaza na wapenda shortcut kama wewe kuskip academic qualifications na kujikita kwenye kukarili maswali ya acca/ireland cpa na majibu yake kisha kufaulu na kujiita wahasibu.
Cpa ya sasa hata kama umemaliza darasa la saba, ili mradi uweze kukarili maswali na majibu ya mitihani ya cpa, ukifaulu unakua certified public accountant. Ofisini tuna wahasibu vilaza kama wewe, hawajui chochote, hata kujenga hoja tu na kufanya financial analysis hawawezi ila wana cpa, wanabaki kunigambia cpa,ucenge.
Mkuu kuna vitu unang'ang'aniza vieleweke kwa kinyume.
Na mifano yako si hai kwa mkutadha husika. Mathalani hilo la uhandisi unavyojaribu kulifananisha na mambo ya uhasibu.

Humu ndani kuna nyuzi fulani zinazonadi taasisi mbalimbali za mambo ya kusoma uhasibu ikiwemo ACCA angalia sifa wanazotaka.

Kwa baadhi ya watu kama wewe huamini ili mtu awe msomi fani fulani mnatazama sana ule mlolongo wa shule. Mkuu kwa dunia sasa watu wanatazama ni jinsi gani wanaweza kutumia muda mfupi zaidi kufikia malengo yao mojawapo ni kama hizi CPA, ACCA n.k

Ningekushauri wewe kama msomi uwe na TABIA YA KUTAFITI VITU NA SIO KUFIKIRI MTAZAMO WAKO NI SAHIHI KWENYE KILA TAALUMA.
 
Kumbe CPA ndo ipo hivyo?
Kwa taaluma zingine, ili upate professional recognition lazima uwe kwanza na ngazi fulani ya elimu - mara nyingi uwe angalau na shahada ya kwanza
Elimu ya Tanzania haiishi vituko.

Ndio maana hatuendelei. Maana flaw kwenye mifumo yetu ya elimu ni mingi mno.

Ndio maana unashangaa, unakua na CPA ya Tanzania, ukitaka kufanya mitihani ya ACCA hupati exemptions kwa kua CPA yetu haieleweki.

Kwa wahasibu watanielewa, ni rahisi Tanzania kupata CPA hata kama wewe sio mhasibu na huna taaluma ya uhasibu, ili mradi tu ufaulu mitihani yake.

Yaani unaweza kua Certified Public Accountant huku huna academic qualification ya accountancy.

Kwa nchi nyingine kitu cha kwanza kupata CPA ni lazima uwe na academic qualifications then uombe kua certified. Nchi nyingine lazima uwe na module hours nyingi sawa na masters ili uwe eligible na CPA.

Huku mwetu unaweza kumaliza form four, ukaanza na atecs hadi CPA.

Sasa imetokea shida ofisini kwetu, wanataka senior accountant, awe na bachelor degree na CPA, aliyepo ana CPA ila hana bachelor degree, ni form four leaver, aliajiriwa kama accounts clerk.

Ikija kigezo cha CPA anayo, ikija kigezo cha bachelor degree hana. Unajiuliza mtu anakuaje certified public accountant huku hana academic qualification ya accountancy?

Ni sawa na mtu kua registered electrical engineer huku hajasoma hata certificate ya umeme. Mradi tu amelipia na amefaulu mitihani.

Certification ni profession, na ili uwe professional lazima uwe na academic qualifications kwanza. Hapa Bongo unakua certified profession without academic qualifications. Mambo ya hovyo kabisa.

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.
 
Kumbe CPA ndo ipo hivyo?
Kwa taaluma zingine, ili upate professional recognition lazima uwe kwanza na ngazi fulani ya elimu - mara nyingi uwe angalau na shahada ya kwanza
Unahitaji kujua kiundani, CPA Ina stages Kama ilivyo ACCA, ili uanzie intermidiate lazima uwe Ina degree ya uhasibu au sifa linganifu, pitia website ya NBAA utaona, vinginevyo utageuka kituko hapa kwa kutoa hitimisho kwa kitu usichokijua
 
Utashangaa zaidi kwenye hz Professional bodies ni matawi ya chama. Propaganda kama zote
 
Huu mfumo wa CPA bongo ulipoingia uliwakuta wahasibu wengi wa serikali wenye certificate na diploma. Sasa wakaamua basi isiwe shida wakapigwe msasa ili wawe certified. Lengo lilikuwa kuwabeba wahasibu wa umma na kupata ada kwa wingi.
 
Baada ya kupitia hoja zote za pande mbili, nimeamua kuchukua fomu ya kujisajili (www.nbaa.go.tz). Aidha, nimefika mwenyewe ofisi za NBAA Dodoma na kuwasilisha kile nilichonacho (vyeti) na baada ya wao kuvipitia, nikatakiwa kuanzia Foundation na angalau nifanye masomo mawili ya Financial Accounting & Cost Accounting. Ngoja niicheze ngoma ili niweze kuchangia mada vizuri.

UPDATE
Level ya Foundation kwa masomo niliyotakiwa nimeikamilisha baada ya matokeo kutoka leo hii (23/12/2019), nime-pass kwa alama B kila somo. Najipanga na hatua itayofuata mwakani! Hadi niujue ukweli kwa kushiriki kikamilifu kwa vitendo.
 
Kuna kitu kimoja watu wengi hawakielewi kuhusu CPA. Unapomaliza mitihani ya CPA ni hatua ya kwanza kuelekea kuwa professional accountant. Huwa tunakosea kujiita CPA holders. Hata ukisoma kwenye cheti wameandika kabisa kuwa ni certificate of completion of CPA Exams.

CPA exams zinakuchuja ili kuhakikisha unafaa kuanza kupanda ngazi kuelekea kuwa Certified Public Accountant. Ndio maana kwa NBAA, anayemaliza mitihani anaitwa Graduate Accountant. Wala hayuko registered na bodi kama jamaa walivyojaribu kulinganisha na taaluma kama uhandisi etc.

Baada ya kumaliza mitihani unatakiwa ufanye practice kwa miaka 3 chini ya uangalizi wa registered accountant wa level ya Associate CPA na Associate CPA in Public Practice kwa auditors, huku ukijaza log book na kuhudhuria semina elekezi ambazo hazipungui masaa 32 kila mwaka (kumbuka semina moja ni kati ya masaa 2 mpaka 6).

Then kila mwisho wa mwaka unatuma report NBAA ambapo baada ya miaka 3 utahitajika kwenda kwenye panel itakayokuhoji kujiridhisha kama umeiva kweli. Na hapo ndio sasa utasajiliwa na bodi kama professional accountant kwa level ya Associate CPA au ACPA PP.

Kiukweli elimu ya CPA huwezi ilinganisha na elimu ya chuo kikuu. Suala la watu kufaulu hiyo mitihani wala lisikuumize kichwa. Yeyote anaweza kulengwa mpaka akafaulu. Ila kwa ambaye atafuata mtaala wa NBAA mwanzo mwisho, anakuwa juu saana kuliko mwenye academic degree. Japo utendaji ni kitu kingine.

So graduate accountants muache kujiita CPA holders. Kwa kifupi, ni vile tu bado mahitaji ni makubwa ndio maana GA wanahitajika. Ila soon utasikia jamaa wanataka Associates pekee. Ila hii process sio ya kitoto kama mtoa mada alivyojaribu kuifanya ionekane.
 
Yaani mkuu unalinganisha Uhasibu na Engineering? Unaijua engineering vizuri au
 
Back
Top Bottom