CPA ya Tanzania ni ya kipekee duniani

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.

Ndio maana hatuendelei. Maana flaw kwenye mifumo yetu ya elimu ni mingi mno.

Ndio maana unashangaa, unakua na CPA ya Tanzania, ukitaka kufanya mitihani ya ACCA hupati exemptions kwa kuwa CPA yetu haieleweki.

Kwa wahasibu watanielewa, ni rahisi Tanzania kupata CPA hata kama wewe sio mhasibu na huna taaluma ya uhasibu, ili mradi tu ufaulu mitihani yake.

Yaani unaweza kuwa Certified Public Accountant huku huna academic qualification ya accountancy.

Kwa nchi nyingine kitu cha kwanza kupata CPA ni lazima uwe na academic qualifications then uombe kuwa certified. Nchi nyingine lazima uwe na module hours nyingi sawa na masters ili uwe eligible na CPA.

Huku mwetu unaweza kumaliza form four, ukaanza na atecs hadi CPA.

Sasa imetokea shida ofisini kwetu, wanataka senior accountant, awe na bachelor degree na CPA, aliyepo ana CPA ila hana bachelor degree, ni form four leaver, aliajiriwa kama accounts clerk.

Ikija kigezo cha CPA anayo, ikija kigezo cha bachelor degree hana. Unajiuliza mtu anakuaje certified public accountant huku hana academic qualification ya accountancy?

Ni sawa na mtu kuwa registered electrical engineer huku hajasoma hata certificate ya umeme. Mradi tu amelipia na amefaulu mitihani.

Certification ni profession na ili uwe professional lazima uwe na academic qualifications kwanza. Hapa Bongo unakua certified profession without academic qualifications. Mambo ya hovyo kabisa.

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.
We ndio wale mnakaririshwa elimu kwani kama mm sina Bachelor ilna aanza foundation hadi napata CPA ina maana nakosa kitu gani kwenye UHASIBU??

Kuhusu huyo jamaa yako amebinywa na MUUNDO

Scheme of service ambao pia unahitaji kupitiwa upya.


SUA kulikua na PROFESSOR ambaye hajasoma secondary alimaza la 7 akasoma
cheti > diploma>bachelor >masters >PHD> Professor
 
Kuna Shemeji yake mkwe wa mama mdogo ake mjomba wa baba yangu wa kambo, kasoma PR afu ana lawyer stamp!!!
Sijui Law Skul alifaulu vipi?
Hapa umeongopa,ktk watu wapo strict ni lawschool hasa kwenye kigezo cha qualifications,sheria inatamka wazi ili u qualify kuingia lawschool ni lazma uwe umesoma municipal law kwa maana ya digrii au relevant qualification ya degree aya sheria na ktk hayo masomo yako uwe umesoma hizo municipal Law
 
Mleta mada acha kukariri, kuwa na degree haimaanishi unajua zaidi au utakuwa mfanyakazi mzuri zaidi, sehemu nyingi especially US wameshaacha kuangalia kigezo cha degree peke yake, kuna software engineers silicon valley hawana degree ila wanaandika program kuliko hata wenye PhDs, CPA holders ni pure in accounting na wanajua uhasibu kuliko degree zenu za uhasibu wa UD ,Mzumbe au IFM, kama kazini kwenu mna conflict na huyo jamaa wa CPA bila degree basi mna matatizo makubwa sana na itakuwa office ya watu ovyo sana
 
Na ni Afrika ambapo tunaona uwezo wa mtu kupitia makaratasi na si utendaji. Ukiomba kazi kampuni ya mzungu Interview yake itajikita kwenye uwezo wa kufanya ile kazi anayotaka kukupa na anaweza hata asiangalie hivyi vyeti vyako
100%, nimefanya kazi na wazungu makampuni makubwa lakini sijawahi kuambiwa onyesha cheti au kuulizwa ugali na maharage una miaka mingapi? mbongo maswali yake mawili muhimu ya kwanza ni cheti na miaka na sio kama unaweza kazi
 
Back
Top Bottom