KERO Ajira Portal kuna changamoto ya kubadili Sifa za Elimu

KERO Ajira Portal kuna changamoto ya kubadili Sifa za Elimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hongera team ya JamiiForums kwa kazi kubwa mnafanya kuhabarisha umma na jamii zote ndani na nje ya nchi hii ya Tanzania.

Ninayokero ambayo inahusiana na Sekretiati ya Ajira kwa maana ya Ajira Portal . Tunapendezwa na huduma zinatolewa na Ajira Portal lakini kuna sehemu ndogo ambayo tunaomba ifanyiwe mabadiliko ili watumiaji wa huduma hii wote wanufaike kwa pamoja.

Tunakubaliana nao kwa suala la Academic qualification kama ilivyo sasa kwamba mtu atapata ajira kulingana na kiwango cha elimu alichonacho lakini kwa maoni yangu napendekeza basi kuwepo na dirisha la kufungua ili mtu aweze kufanya mabadiliko yeye mwenyewe kuliko kama hivi tunavyopata taabu wasiliana nao na kikubali ubadilishiwe hizo accademic qualification ni ngumu sana.

Mfano; Mimi nina nimehitimu Diploma ya Pharmacy lakini sina cheti na nilijisajili Ajira Portal kwa Level ya Diploma lakini pia nina fani nyingine ya udereva ambayo nina vigezo vyote vinavyohitajika lakini nashindwa kufanya mabadiliko.

Naambiwa kuwa labda niongeza elimu ya juu zaidi wakati hata hiyo Diploma nadaiwa karibu 2m ili nipate cheti changu.

Unaishi Dar, nyumba ya kupanga na mke na mtoto utatunza kiasi gani kila mwezi kwa mshahara wa laki nne tunaolipwa huku mtaani ili nikamilishe deni wakati nina fani nyingine ambayo naweza pia kuendelea nayo tunaomba msaada sana kutusemea katika hili.

Mfano, nina Diploma ya Pharmacy nataka niweke Certificate ya Driver hapo hata ukiwasiliana bado hawataki kuondoka, lakini mimi changamoto hyo ni kwamba sina Cheti cha diploma hivyo nilitaka nitumie elimu ambayo ninavyovyeti tayari.

Ukiwa na elimu ya degree kwenda masters syo lazima uwasiliane nao mfano wenyew utakupa kazi kulingana na elimu ya juu uliyonayo, hvyo mm atanikiongeza hyo certificate mfumo hautanipa kazi kwani mwanzo kabisa nilijisajil kama diploma , hyo ndyo shida.

Ni hicho cheti cha driver ambacho kinaendana na sifa ambazo zinahitajika ambapo ni dereva daraja la pili pamoja na leseni ya daraja C au E ambapo pia nimekudhi hivo vigezo.

Cheti cha form lazima uwe nacho kwakuwa driving ni level ya certificate hvyo kama ulisajiri kwa ukaweka diploma ya fani yoyote ukija kuweka certificate huwezi kupata kwa certificate Hadi Ile diploma itoke pale
 
Back
Top Bottom