CPA ya Tanzania ni ya kipekee duniani

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.

Ndio maana hatuendelei. Maana flaw kwenye mifumo yetu ya elimu ni mingi mno.

Ndio maana unashangaa, unakua na CPA ya Tanzania, ukitaka kufanya mitihani ya ACCA hupati exemptions kwa kua CPA yetu haieleweki.

Kwa wahasibu watanielewa, ni rahisi Tanzania kupata CPA hata kama wewe sio mhasibu na huna taaluma ya uhasibu, ili mradi tu ufaulu mitihani yake.

Yaani unaweza kua Certified Public Accountant huku huna academic qualification ya accountancy.

Kwa nchi nyingine kitu cha kwanza kupata CPA ni lazima uwe na academic qualifications then uombe kua certified. Nchi nyingine lazima uwe na module hours nyingi sawa na masters ili uwe eligible na CPA.

Huku mwetu unaweza kumaliza form four, ukaanza na atecs hadi CPA.

Sasa imetokea shida ofisini kwetu, wanataka senior accountant, awe na bachelor degree na CPA, aliyepo ana CPA ila hana bachelor degree, ni form four leaver, aliajiriwa kama accounts clerk.

Ikija kigezo cha CPA anayo, ikija kigezo cha bachelor degree hana. Unajiuliza mtu anakuaje certified public accountant huku hana academic qualification ya accountancy?

Ni sawa na mtu kua registered electrical engineer huku hajasoma hata certificate ya umeme. Mradi tu amelipia na amefaulu mitihani.

Certification ni profession, na ili uwe professional lazima uwe na academic qualifications kwanza. Hapa Bongo unakua certified profession without academic qualifications. Mambo ya hovyo kabisa.

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.
Na ni Afrika ambapo tunaona uwezo wa mtu kupitia makaratasi na si utendaji. Ukiomba kazi kampuni ya mzungu Interview yake itajikita kwenye uwezo wa kufanya ile kazi anayotaka kukupa na anaweza hata asiangalie hivyi vyeti vyako
 
Mkuu hupaswi kukariri. Sisi hii elimu tumeletewa tu na wazungu. Huko kwao wanafanya hivi hivi tena ni rahisi zaidi kwa entry qualification tofauti na hapa. Udaktari na shule kama engeneering lazima ukae darasani ni too practical. Lakini hata hiyo sheria wapo watu wanaipiga kwa mitihani tu wanalamba degree nchi za wenzetu labda mnataka NBAA waanze kutoa degree kwa watu walio clear intermediate kama wanavyofanya ACCA ili kuwaridhisha watu kama nyie mnaotaka kuona cheti hicho tu. Hivi mnafikiri mtu aliyepiga professional exams ni short cut au njia rahisi? Basi kila mwenye degree si angekuwa anajibebea tu CPA? Nenda kafanye hiyo CPA uipate ndio utajifunza adabu kidogo.
Sawasawa...
 
Mifumo ya elimu ni tofauti. Sisi tunafata mfumo wa elimu ya Uingereza ndio maana kwao unaweza kufanya ACCA kama ukiwashawishi hata kwa work experience kwa kuanzia kwenye mitihani inayofanana na ATEC ukifaulu then unaanza ACCA. Ndio maana wahindi wa bongo wengi huwaoni vyuoni huko. Wakimaliza secondary wanapiga ACCA tu then kutana nae kazini uone. Marekani ndio wana mfumo tofauti wa elimu ambao ni tofauti kabisa na Uingereza. Hata ukiwa na ACCA hupati exemptions kwenye CPA ya marekani...ni mifumo tu
Acha kufananisha mifumo tofauti ndugu. Samattaaaaa
 
Kuna kitu kimoja watu wengi hawakielewi kuhusu CPA. Unapomaliza mitihani ya CPA ni hatua ya kwanza kuelekea kuwa professional accountant. Huwa tunakosea kujiita CPA holders. Hata ukisoma kwenye cheti wameandika kabisa kuwa ni certificate of completion of CPA Exams.

CPA exams zinakuchuja ili kuhakikisha unafaa kuanza kupanda ngazi kuelekea kuwa Certified Public Accountant. Ndio maana kwa NBAA, anayemaliza mitihani anaitwa Graduate Accountant. Wala hayuko registered na bodi kama jamaa walivyojaribu kulinganisha na taaluma kama uhandisi etc.

Baada ya kumaliza mitihani unatakiwa ufanye practice kwa miaka 3 chini ya uangalizi wa registered accountant wa level ya Associate CPA na Associate CPA in Public Practice kwa auditors, huku ukijaza log book na kuhudhuria semina elekezi ambazo hazipungui masaa 32 kila mwaka (kumbuka semina moja ni kati ya masaa 2 mpaka 6).

Then kila mwisho wa mwaka unatuma report NBAA ambapo baada ya miaka 3 utahitajika kwenda kwenye panel itakayokuhoji kujiridhisha kama umeiva kweli. Na hapo ndio sasa utasajiliwa na bodi kama professional accountant kwa level ya Associate CPA au ACPA PP.

Kiukweli elimu ya CPA huwezi ilinganisha na elimu ya chuo kikuu. Suala la watu kufaulu hiyo mitihani wala lisikuumize kichwa. Yeyote anaweza kulengwa mpaka akafaulu. Ila kwa ambaye atafuata mtaala wa NBAA mwanzo mwisho, anakuwa juu saana kuliko mwenye academic degree. Japo utendaji ni kitu kingine.

So graduate accountants muache kujiita CPA holders. Kwa kifupi, ni vile tu bado mahitaji ni makubwa ndio maana GA wanahitajika. Ila soon utasikia jamaa wanataka Associates pekee. Ila hii process sio ya kitoto kama mtoa mada alivyojaribu kuifanya ionekane.
Angalau nimekuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo mimi ni mhasibu ila kiukweli taaluma yetu imeingiliwa. Ukiwa na pesa na muda wa kupitia past papers tayari wewe ni mhasibu aliyehidhinishwa. Pia ninaye classmate yuko tanapa nilisoma naye akafeli form 4 wakati sisi tunaenda advanced yeye akaanza ATEC.

Leo hii ni mhasibu mzito huko.

Taaluma pekee tz ambayo haijaanza kutiwa najisi ni taaluma ya sheria na udaktari.... Vingine ni ukanjanja tu
Acha wivu
 
Well said mkuu, huyu mleta uzi atakuwa alifeli mitihani ya NBAA sasa wivu umemjaa.
Sidhani kama mwenye CPA kamili ataweza kuponda NBAA au kuongea mambo kama alioongea hapo...
CPA ni muhimu sana, Degree za accounts hazitoshi kuwa mhasibu bora.

Mhasibu kamili ni yule anayejua standards na practices
 
Na ni Africa ambapo tunaona uwezo wa mtu kupitia makaratasi na si utendaji. Ukiomba kazi kampuni ya mzungu Interview yake itajikita kwenye uwezo wa kufanya ile kazi anayotaka kukupa na anaweza hata asiangalie hivyi vyeti vyako
Wacha wewe. Mzungu wa wapi huyo? Au wa Buza kwa Mpalange?
 
Na ni Africa ambapo tunaona uwezo wa mtu kupitia makaratasi na si utendaji. Ukiomba kazi kampuni ya mzungu Interview yake itajikita kwenye uwezo wa kufanya ile kazi anayotaka kukupa na anaweza hata asiangalie hivyi vyeti vyako
CPA Bongo eti Kuna mpaka Best student?
 
Elimu ya Tanzania haiishi vituko.

Ndio maana hatuendelei. Maana flaw kwenye mifumo yetu ya elimu ni mingi mno.

Ndio maana unashangaa, unakua na CPA ya Tanzania, ukitaka kufanya mitihani ya ACCA hupati exemptions kwa kua CPA yetu haieleweki.

Kwa wahasibu watanielewa, ni rahisi Tanzania kupata CPA hata kama wewe sio mhasibu na huna taaluma ya uhasibu, ili mradi tu ufaulu mitihani yake.

Yaani unaweza kua Certified Public Accountant huku huna academic qualification ya accountancy.

Kwa nchi nyingine kitu cha kwanza kupata CPA ni lazima uwe na academic qualifications then uombe kua certified. Nchi nyingine lazima uwe na module hours nyingi sawa na masters ili uwe eligible na CPA.

Huku mwetu unaweza kumaliza form four, ukaanza na atecs hadi CPA.

Sasa imetokea shida ofisini kwetu, wanataka senior accountant, awe na bachelor degree na CPA, aliyepo ana CPA ila hana bachelor degree, ni form four leaver, aliajiriwa kama accounts clerk.

Ikija kigezo cha CPA anayo, ikija kigezo cha bachelor degree hana. Unajiuliza mtu anakuaje certified public accountant huku hana academic qualification ya accountancy?

Ni sawa na mtu kua registered electrical engineer huku hajasoma hata certificate ya umeme. Mradi tu amelipia na amefaulu mitihani.

Certification ni profession, na ili uwe professional lazima uwe na academic qualifications kwanza. Hapa Bongo unakua certified profession without academic qualifications. Mambo ya hovyo kabisa.

Elimu ya Tanzania haiishi vituko.
Uko sahihi kabisa. Hivi karibuni imeanzishwa Law School kwa ajili ya ku-certify mawakili, wale waliosoma degree za Sheria. Hii inamaanisha kuwa kama wewe huna degree ya sheria, huwezi ukasogea kwenye hiki chuo cha Law School, na huwezi hata siku moja ukaja kuwa Wakili.

Wanachofanya hawa watu wa CPA kinafanana kama vile Law School nao waanze kuwa wanatoa mitihani halafu mtu yeyote yule hata ambaye hana dgeree ya sheria, ikitokea akafanya mitihani hiyo na kufaulu, basi anakuwa certified kuwa Wakili!
 
Hhhhhh changamoto ni kuwa kama huna msingi wa law aiseee ni Ngumu kutoboa pale maana pale ni practical ya theory uliyojifunza undergraduate Sasa utawezaje kufanyaja practical ya theory ambao huijui

Ni sawa kwenye engineering how come ukapige pepa pale wakata hata theory Mona huijui?
 
Uko sahihi kabisa!
 
Back
Top Bottom