Kutofautiana kwa hoja, haina maana nabwabwaja. Mtu makini hutafakari kwanza hoja ya upande wa pili kabla naye hajabwabwaja.
Taifa linatoa takwimu zote za magonjwa mengine isipokuwa corona, je huwezi kujiuliza swali hapo. Chunguza kuna nini nyuma ya pazia.
Maamuzi ya kutotoa takwimu si ya mtu mmoja bali ni jopo la watu wenye ueledi mkubwa kwa ajili ya taifa letu. Hata wanaotulazimisha kutoa takwimu nao wana jopo lao lenye malengo yao yaliyo hasi nasi.
Je wajua ya kwamba kuna njama ya kuwangamiza watu weusi barani Afrika? Hatujui watatumia silaha gani, ni lazima tujihami.
Kwanza nikupongeze kwa kutambua kuwa takwimu za magonjwa yote hapa nchini zipo wazi kwa jamii isipokuwa kwa corona.
Pili ningependa utambue kuwa ugonjwa huu upo dunia nzima Amerika Kaskazini na kusini, Asia, Australia na hata Afrika.
Njama za kumwangamiza mwafrika kwa ugonjwa huu unaziokota wapi wakati mabara yote ni waathirika vilivyo na kote hawana mtazamo kama huo?!
Afrika penyewe hakuna nchi hata moja yenye kuona kuwa inalengwa na ugonjwa huu isipokuwa kwa serikali ya Magufuli?
Ni serikali ya Magufuli peke yake inayoona hivyo. Kumbuka mimi binafsi sioni hivyo. Tusiioona hivyo tuko wengi sana ndani ya nchi hii. Usishangae kuwa hayupo mwenye uelewa aliyeko upande wenu.
Siyo siri mlioko huko ni njaa zenu na umbumbu zaidi ndiyo unaowafanya kuendekeza kucheza ngoma uchwara hizo mnazocheza.
Hivi, Magufuli na genge lake wanapojaribu kutudanganya na hadithi zao hizi wanajaribu kufanya hivyo kwa ridhaa ya nani?
Demokrasia ni wengi wape. Kwanini tusitafute ridhaa hata kwenye kura ya maoni tu? Kwanini mnataka kutulazimisha na maoni yenu tusiyokubaliana nayo? Kwanini mnataka kutufanya kama watoto wadogo? Kwanini, ..., Kwanini, .., kwanini lakini ???
Mabibi na mabwana sisi ni taifa na kama taifa cheo ni dhamana tu. Kiongozi yeyote kwa uongozi wake ni muhimu akazingatia ukweli kuwa kwa dhamana aliyo nayo si kuwa sasa eti ndiyo anayo fursa kamili ya kufanya au hata kusema lolote kwa kuwa tu eti dhamira yake itakuwa imemtuma huko. Rais wetu...
www.jamiiforums.com
Mmejipachika eti kuwa mna weledi, hakuna lolote. Fahamuni kuwa kwa kila kifo kinachopita na ugonjwa huu upo siku mtajibu.
Kwa hakika mnatukera sana hasa hasa tunapoendelea kupoteza wapendwa wetu kila siku huu nyie ikiwa haiwahusu:
Mabibi na mabwana na tuambizane ukweli tu, kwani haisaidii kuukimbia ukweli. Pia msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Hongera Dar kwa kuanza kutupia barakoa kujaribu kujihami na kuwahami wengine japo kwa jitihada binafsi. Inatia moyo kwani mmedhihirisha "kifaranga hafunzwi kuchakura!" Ninaamini...
www.jamiiforums.com