Corona: Afrika CDC yaipa onyo Serikali ya Tanzania

Corona: Afrika CDC yaipa onyo Serikali ya Tanzania

Yako wapi "mawazo" yako nayo tuyapime!
Inawezekana mawazo yako yakawa hayana hata "mwanzo wa safari" kabisa!
Haya majibu ndio yananipa shida, unaweza kuwa na mawazo mema ila hujui kujenga hoja ikaeleweka. Sina nia ya kubishana ila kuwa na mtazamo ulio nao, ni hatari hata kwako mwenyewe.
 
Mitaani vilio kila mahali. Ukiingia status za whatsapp huwezi kosa marafiki 2/3 wenye msiba.

Leo humu jf jerrybanks kafiwa na baba, baba mkubwa na mjomba kwa wakati mmoja.

Juzi nipo hospitali nikakutana na jamaa mmoja hapa Dar kamsafirisha dada yake toka Tanga aje atibiwe, kule Tanga walishazika ndugu zao 3 wa baba mmoja mama mmoja ndani ya wiki 1.

This is public irresponsibility and masaccre kwa sirikali iliyopewa jukumu la kuhakikisha usalama wa raia wake lakini wao wanachukulia for granted huu mlipuko.

Ni kweli sisi sote hatutaki chanjo ya wazungu, lakini kwa nini sirikali haichukui japo zile basic precautions ili angalau kupunguza maambukizi?
Kati ya sisi na wao nani corona inamfyeka sana. Waache uwongo. Corona inawafyeka sana wazungu na wamerikana pamoja na lockdown zao, barakoa, social distancing na chanjo kibao. Hata mchina hafwekwi tena na corona.

Waache kutusingizia sisi. Mara ooh tunatoa takwimu za uwongo zinazoonesha corona haitufyeki zaidi yao. Tanzania tunawapa takwimu ya zero incidence. Wanakataa eti zero siyo takwimu na kwa hiyo wanatuhesabu hatuwapi takwimu kwani 0 haikubaliki. Wanataka tuandike malaki ya watu wanakufa kwa corona kila siku. Tukiandika hivyo watachekelea sana na kuanza kutuchanja kila sehemu! Mungu anawaona. Na korona hii Mungu kawapa wao kwa sababu ya machafu wanayoyafanya zaidi ya yale waliofanya wananchi wa Sodoma na Gomola enzi zile. Unakuta dume zima linajitambulisha kuwa ni mke wa mwanaume fulani. Wakiacha uchafu huo na kutubu Mwenyezi Mungu atawaondolea hiyo corona. Wakiendelea kutusakama tutamwomba Mwenyezi Mungu awatandike likorona lingine likali zaidi.
 
CDC ndio kijidudu gani tena hiki! Kiambieni kikakojoe kilale! Kama kinataka data kiombe za malaria tutampatia!
Eti tutaliweka hatarini bara la africa mfyuuuu! Kwani Tz ndio imeleta corona? Ebo!
Ukihitaji uhakika kamwulize kabudi.

Atakusifu hadharani ila mkiwa wenyewe atakwambia ulichoandika ni utopolo haswa!
 
Halafu unataka watu wamwone kiongozi wao (Rais) kuwa mtu wasiyeweza kumwamini asemacho yeye? Wamwone kuwa ni 'mwongo', wakuamini wewe kapuku, usiyekuwa na mbele wala nyuma?
😆😆😆😆😆😆. Watu wangu wanaang'amia na kuteketea kwa kukosa maarifa. Kapuku mimi naishia hapa.
 
Siku nne zilizopita pale Tarime Mama mmoja alijisikia vibaya muda wa asubuhi na kupelekwa hospitalini pale Tarime kwa matatizo ya kupumua na ilipofika mida ya saa mbili na nusu usiku siku hiyo akaaga dunia. Inasikitisha sana na huyo Mama namfahamu.
 
Kwa kutotoa uzito unaostahili, sipendi kutumia lugha hii, lakini hatuna namna, lazima tuseme:

RAIS MAGUFULI, KAMA ULICHAGULIWA AU ULIIBA KURA, HILO KWA SASA SIYO HOJA. CHA MUHIMU NI KUWA UNA WAJIBU WA KUWALINDA WATANZANIA BADALA YA KUWAANGAMIZA.

KWA KAULI ZAKO ZA UWONGO KWAMBA TANZANIA HAKUNA CORONA, NA HIVYO KUWAFANYA WATU KUAMINI KAULI ZAKO, NA KUACHA KUCHUKUA TAHADHARI, HAKIKA WEWE NI KIONGOZI MUUAJI.

Wale ambao maisha yao yangeweza kuokolewa kwa tahadhari, lakini wamekufa kutokana na uongozi wako mbaya, laana ikawr juu yako na uzao wako maana huna huruma wala chembe ya utu.

Nayaandika haya tukiwa tunasubiri mwili wa marehemu, mama wa rafiki yangu. Mimi nikiwa nimepoteza ndugu yangu hivi karibuni akiwa na dalili za kushambuliwa na covid 19, rafiki yangu, huu ni msiba wa 5 ndani ya wiki 3, wote wakiwa na dalili za kuathiriwa na Covid 19.

Ninyi mnaomshabikia Rais wakati akitenda uovu, zioneeni huruma familia zinazoomboleza kila siku kutokana na vifo vinavyosababishwa na corona.

Wakati wa majanga kama haya, we need mentally and spiritually strong leaders not muscular leadership.
Poleni sana Mkuu.
 
Mtaani kwetu,Jana wawili wamefutika katika orodha ya watu duniani,kwa matatizo ya upumuaji
 
Hizo takwimu tumtolee nani na kwa nini?

"Tumtolee nani?" Labda tuanzie hapo mkuu. Ulikuwa ukimaanisha wewe na nani?

"Kwa nini?" Kujua uelekeo wa ugonjwa ulivyo kote duniani.

Kama hali yetu ni njema zaidi basi hiyo ni la kheri zaidi. Ni sawa na dunia Ina la kujifunza kwa hilo.

Kama hali yetu inazidi kuwa mbaya zaidi, basi dunia Ione ni kwa jinsi gani tushirikiane na jamii ya kimataifa kuona maisha ya wapendwa yanalindwa kwa ubora zaidi.

Ikumbukwe ugonjwa huu ni janga la dunia. Hauna mwenyewe kama ilivyokuwa polio.

Kwa maana kuwa hali ya nchi moja ni muhimu Kwa nchi zingine.
 
Africa CDC haina mamlaka ya kuipa onyo serikali yetu, hujui kabisa ww how UN agencies and any Government zinavyofanya kazi. Kamwe Africa CDC haiwezi ipa onyo serikali yoyote ile duniani. Hivi Civics ulipata "F" kubwa sana.

Chadema mbona akili zenu hamjui mambo kabisa..
 
"Tumtolee nani" labda tuanzie hapo mkuu. Ulikuwa ukimaanisha were na nani?

"Kwa nini" kujua uelekeo wa ugonjwa ilivyo note duniani. Kama Hali yetu ni njema zaidi basic sana kujifunza.

Kama Hali yetu inazidi kuwa mbaya zaidi lions ni kwa jinsi tushirikiane na jamii ya kimataifa kuona maisha ya wapendwa yanalindwa kwa ubora zaidi.
Kujua uelekeo wa ugonjwa kote duniani?
Yapo magonjwa na mengine ambayo hali yetu ni mbaya zaidi na watu wetu wanakufa zaidi kuliko. Malaria ni mojawapo, na kama kuna jumuia ya mataifa iliwahi kukusaidia, ilikusaidia nyavu za mbu na wanaendelea kutengeneza dawa mpya za malaria ili nchi yako ibaki kuwa soko la kudumu la madawa ya malaria. Ila kwao kulishawahi kuwapo na malaria ila wao waliifuta kabisa. Kama wangekuwa na lengo la kukusaidia wangekusaidia ili uimalize kabisa hiyo malaria.

Mbona hamstuki tu?
 
Kujua uelekeo wa ugonjwa kote duniani?
Yapo magonjwa na mengine ambayo hali yetu ni mbaya zaidi na watu wetu wanakufa zaidi kuliko. Malaria ni mojawapo, na kama kuna jumuia ya mataifa iliwahi kukusaidia, ilikusaidia nyavu za mbu na wanaendelea kutengeneza dawa mpya za malaria ili nchi yako ibaki kuwa soko la kudumu la madawa ya malaria. Ila kwao kulishawahi kuwapo na malaria ila wao waliifuta kabisa. Kama wangekuwa na lengo la kukusaidia wangekusaidia ili uimalize kabisa hiyo malaria.

Mbona hamstuki tu?

Hivi serikali zetu hizi zimewahi hata kusaidia hizo neti za malaria? Achilia mbali hata kusaidia lolote zaidi ya kujikita kwenye kuwakamua watu kodi zikiwamo za mazishi, vipaimara, harusi, sherehe nk?

Hivi kwa nini kuweka siri maeneo yaliyo na mnyama mkali ili kwa watu kuchukua tahadhari?

Hivi kwa nini hamstuki mamburula nyie?
 
Kwa nini unitukane ndugu yangu? Nenda kaangalie centre for disease control ya Marekani majukumu yao na nini wanachofanya halafu angalia na majukumu ya Africa cdc. Africa CDC kazi yao kubwa ni kupigia debe vaccines na drugs za waulaya na wamerakani tu. Imekaa kama kitasisi cha PR (public relation) kwa maboss wao huko Marekani. No, huo ukoloni hatutaki.
Mkuu zimmerman ,kuna mambo ambayo kama huna uhakika nayo,bora ukae kimya.
 
hili dude lipo. ukisikia sikia tu unawezadhani ni conspiracy theories ila nina ushuhuda wa mtu naemfahamu alikuwa mzima juzi tu. juzi kwa maana ya juzi. leo yupo hospitali amekuwa diagnosed na alichonieleza kuwa 'infection mbaya kwenye mapafu'.

jana nilikuwa maeneo ya kinyerezi nikaona daladala za mbezi segerea zinajaza abiria mpaka wanabambiana.

huku na kule waziri wa afya yupo busy na maigizo ya malimao na kujifunika mablanketi.


hatari sana.
 
Back
Top Bottom