CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

The issue here is not for government to pay or Tanesco to be held responsible to pay....i object..

Hii ni kwa sababu ikilipa Tanesco tunaumia sisi na kama ikilipa serikali bado waumiaji ni sisi

Kwa nini tuumie wakati kuna majitu na familia zao yanaendelea kutanua na kututukana mitaani kwa matumbo ya jeuri za fedha yetu

Ile sheria ya uhujumu uchumi kwani si ipo (though literally najua imeuliwa mbali) na itumike basi au kama sivyo raisi atumie mamlaka yake makubwa kupitiliza aliyopewa na katibu bome kutoa kauli ya kushughulikiwa majibwa haya yaliyotuingiza kweye utapeli wa aina hii for their crave for money

Sasa kama hata hili atashindwa then basi, historia itachukua mkondo wake na kumhukumu
 
HAPO SASA.....MNAONGEA SANA NA HAMNA ACTION MUNAOCHUKUA.
MTA BRAINSTORM SANA HAPA, BUT AT THE END OF THE DAY WHAT WILL HAPPEN....??
OK TUMESHA SOMA HII, NA ZINGINE NYINGI....NOW WHAT?
MPAKA CKU MUTAKAPOAMUA KUCHUKUA HATUA......UNTIL THEN.....TUTABAKI NA AMANI YETU!! C TUNALALA NA KUAMUKA VIZURI! BANA:bored:

Nawe una tatizo.....unasema....mnaongea...mutakapoamua....yaani wewe unajiweka pembeni...ungesema...........tunaongea...tutakapoamua...au wewe huguswi?....hujui kuwa maneno huanzisha matendo?
 
Rais kaagiza hesabu zote zifike kwake mara moja kabla ya Bunge, sasa hii itaendaje? manake haijakamilika bado
 
sasa tuna kila sababu za kudai kilicho chetu toka kwa wahusika ambao no serikali.........
 
Nimefatilia ule mjadala wa Tanesco na serikali.
Mara ya kwanza TANESCO walikataa kulipa deni tena kwa kuweka vielelezo vya msingi.
But suddenly walivyopata barua kutoka kwa mkaguzi(kama sikosei) wakabadili mawazo na kukubali kulipa deni.
Swali: ni nini kilichowabadilisha Tanesco?
 
Nimefatilia ule mjadala wa Tanesco na serikali.
Mara ya kwanza TANESCO walikataa kulipa deni tena kwa kuweka vielelezo vya msingi.
But suddenly walivyopata barua kutoka kwa mkaguzi(kama sikosei) wakabadili mawazo na kukubali kulipa deni.
Swali: ni nini kilichowabadilisha Tanesco?
Kama kawaida mkuu,...ni maagizo kutoka "juu"
 
Hii hela haitakiwi kulipwa PERIOD.

Ukisoma hizi attachments inatia hasira na ni aibu kwa waliotufikisha hapa kuwa bado ni viongozi na wengine wanashikiria nyazifa katika serikali wakitafuta nafasi ya kutuingiza tena mkenge!

Ni bora wapelekwe jela, na hiyo mitambo itaifishwe!
 
kwa kweli nchii hii inalika sana....serikali ilipe deni hilo....,hapa ndipo naona mkono wa EL enzi zile alivyokuwa PM.....alilazimisha richmond ipewe zabuni hiyo...
 
k1av0.jpg

Karamagi ,tungemuuliza sasa kama bado anaamini kuwa yeye ni msafi?
 
Endapo Tanesco itaendelea kubeba mizigo ya wazembe wa serikalini. Ni kichaa tu atakayeendelea kuamani kuwa ipo siku shirika hilo litajiendesha kwa faida. Hata hii mikataba iliyombioni kelele za ukiukwaji wa taratibu zishaanza kupigwa!

Hatujifunzi kwa sababu wale wote waliosababisha hasara hizi hawakuchukuliwa hatua.

Hivi wale waliompeleka Liyumba mahakamani kwa kuisababishia serikali hasara walistahafu baada ya kesi ya Liyumba nini?
 
Bado naona kuna irreguralities nyingi sana zilitokea ktk process nzima ya contracting,na uhamishaji wa contract.Hakika deni hili linaweza epukika kama wanasheria private watalivalia njuga.

Lakini kama itabidi lilipwe,basi ni serikali nasi Tanesco wa kulipa.Hakika naanza kurudisha imani kwa watendaji wa Tanesco kwa kuwa walifuata taratibu sawasawa,na kila walichofanya waliplay safe,waliyafanya yote hayo under DURACE,siwalaumu kabisa.Serikali wabebe zigo lao, lakini no one should go unpurnished,waadhibiwe wote walioacha mambo haya yatokee,waliosign mawasiliano ya wizara kwa Tanesco.

Halafu mheshiwa invisible, sisi wananchi sasa tuanze upya ku-overhaul system, tuhakikishe wote waliokua serikalini kipindi hicho wametoka, hili ni kama tutashindwa kuiondoa serikali nzima madarakani. Tuweke serikari mpya kabisa, tuanze upya.

Walikotufikisha hawa ni aibu kwa kizazi kijacho na kizazi kijacho kitatuhukumu kwa kutochukua hatua. Afadhali tuchukue hatua, watoto wetu wataona kuwa tulichukua hatua kwa kadiri tulivyoweza.
 
Ukiwaza sana kuhusu madudu ya hawa 'Wataalamu' wa serikali, unaweza kudhani hawakusoma hata shule ya msingi.

Haiwezekani professionals waima na PhD zao wanasaini madudu bila objection za kutetea maadili ya kazi zao. Inakera sana kwa kweli.

:bored:
 
Tutaumiza vichwa bure si serikali wala Tanesco wanaotakiwa kulipa ni wale walioliingizia taifa hasara kwa makusudi kabisa wakaingia mkataba na kampuni ambayo haipo kwa kutumia mgongo wa serikali.
 
Mkuu Invisible,
Ukiweza lete documents za hayo maagizo ya wizara kwenda TANESCO ya kulazimisha hiyo mikataba tuone nani alisaini....huyo ndio atalipa au tutakufa naye...otherwise asante sana kwa kutujuza...japo umeniongeza hasira kwa hili....sikulaumu lakini
Mi ningekuwa na asili ya mashariki ya kati ningewaonyesha mfano hawa viongozi wezi.
 
Wakati umefika sasa wa bora wachache wafe wengi waishi kwa raha. Sasa ninaanza kuamini kuwa tunasumbuliwa na kikundi cha watu wachache wasiozidi 10 kama alivyosema 6


kwa wanamapinduzi hili ni pigo tuanzie hapa jf mapambano ya kweli
 
Inasikitisha sana. Yaani kwa kweli Now I understand kwa nini watu wamepoteza imani na Kikwete. Yaani barua ya huyu Mh. CAG inajieleza vyema kabisa. Kwa nini waliohusika na haya maamuzi wasifilisiwe? au tunasubiri 'ushahidi'?

Tanzania siyo kampuni ya mtu binafsi. Tanzania ni taifa letu sote. Kwa nini tunaumizana hivi jamani? Inakatisha tamaa kwa kweli.
 
Mkuu hujatoka nje ya mada; suala la gesi nalo ni suala la kuangalia, linaongeza mzigo mzito kwa TANESCO ilhali inatoka hapahapa kwetu. Inazua shaka kuwa hata tukichimba mafuta bado hali itakuwa mbaya kwa nishati hiyo Tanzania, watakaonufaika ni wachache kwa michezo yao ileile
I see where you're comming from, ni kweli haijalishi utajiri tulionao kwasababu hata tukiwabadili CCM mambo ni yale yale? Maana naona tatizo hapa ni hao wazungu?

Mbona Libya wanamafuta na nasikia wananchi walikuwa wanaishi vyema tu, sasa tusipowasikiliza hao wazungu na hizo dili zao za kimangungo hawatatutoa roho kweli bila kujali kama ni CCM ama CDM kiko madarakani?

Maana huwa najiuliza who really calls the shots.
 
Mie naona kwanza ni huyo alikuwa waziri aitwe nae aelezee kwa nini alichukÙa hatua hizo na hapo atataja nani alimtuma Tanesco etc

Duh kumbe wengi walikula pamoja sitashangaa kama raisi anajua habari hii ndani nje kabla 419 haijaanza kwa jambo hili. Tunaitaji kitu kama EFCC iliyopo Nigeria viongozi wa kona zote kwenye pesa za wananchi watajifunza
 
Back
Top Bottom