Jamani ni lini tutampata mkombozi wa nchi hii? Tukiendelea hivi mwisho wa siku hakitaeleweka!
Tumeshampata ila Dola haikumkubali, na kuna wengine pia wanatumiwa kumkataa.
Kama Dr Phd Slaa asingekataliwa na
Dola na maoni ya walio wengi yangeheshimiwa wakati wa uchaguzi uliopita leo tusingekuwa tunaongea habari hizi, habari ya Richmod/Dowans ingekuwa ilishakwisha na wahusika wapo kule wanapotakiwa kuwa.
pia mambo kama;
Kuvunja Mikataba bomu,
Kulipa wazee wa EAC,
Kuanzisha Mchakato wa katiba (baadaye kuunda Tume Huru ya Uchaguzi)
Kuondoa kero za Muungano (Hasa kuuvunja ndio dawa ya Kudumu)
Kufanya Bunge. Takukuru,Mahaka,Majeshi na Usalama wa Taifa Kuwa Vyombo Huru.
Afya bora,
Elimu bora,
Mikakati bora ya Kuinua Uchumi wa Nchi.
Kuzuia Uchakachuaji wa Mafuta,
Kuzuia uingizwaji wa Bidhaa feki,
Kudhibiti Mfumuko wa Bei
Kuboresha usafiri wa miji mikubwa (mana watu wanapoteza masaa 4 Kila siku kwenye foleni barabarani)
NK,
Yangekuwa ndio kipaumbele na nina hakika yangekuwa yameanza kufanyiwa kazi.
Tatizo Tunaongea sana, Tunalala tukiamka tunaanza kuongea na kulala tena, haitusaidii!. jamaa watazidi kula na kunywa na kusaza huku sisi na jamii zetu tukiishia kunung'unika tu. Jamani kwa mambo kama haya! Mtindo wa Tunis na Misri ndiyo suluhu kwisha, Maana kwa Mwendo huu hatutakaa tushuhudie Uchaguzi Huru na wa Uwazi na Kweli