CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

mmmmmmmmmm sina cha kuandika hapo..Labda twende kwanza kwa bibi Tabora ndo tupate mawazo mapya...Watumaliza ccm
 
Hapa dhamira si kukatishana tamaa, tunataka 'Great Thinkers' tuziangalie kwa umakini hizi nondo na kuja na hoja za kuweza kubadili hali ya nchi. I believe we can, YES we CAN!
 
Sasa kinachofuata hapa nini aise? Yani sasa naelewa kabisa haya maandamano ya Chadema.
 
Tanesco wagome kabisa kulipa hilo deni, ikiwezekana waliotuingiza kwenye huu mkataba walipe kwa fedha zao za mfukoni..
 
Tanesco wagome kabisa kulipa hilo deni, ikiwezekana waliotuingiza kwenye huu mkataba walipe kwa fedha zao za mfukoni..
Pendekezo lako linaelekea kufanana na la POAC walilotoa; serikali (si TANESCO tena) ndo ilipe gharama hizi!
 
Kazi ipo. Big up Usiyeonekana aka Invisible kwani unatuonyesha uchafu wa serikali z(y)etu. Sijui kwa nini wanatuibia hivi hawa watanzania wezetu? Ni ulafi na ubinafsi au kuna kingine zaidi?

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Shinyanga yote na Madini yake.
 
Nina mobile hapa ,sioni kilichoandikwa!
Nasikitika kuwa attachment japo si kubwa (700kb) lakini via mobile inaweza kuwa ngumu kuichukua. Ukiingia kwenye pc utaweza kusoma; ni ndefu kidogo na si maandishi bali scanned document
 
Mmh hii ndio Tanzania zaidi ya tuijuavyo kwa kweli!

Wanasiasa wetu majukwaani wakisimama wanasema wao pia wako nasi kwamba hawataki hii pesa ilipwe, confidentially CAG anasema serikali imekubali kulipa kupitia TANESCO issue pekee ni how to book it (vitabu vya tanesco or government) basi lakini kulipwa inalipwa, huku kama si kutuona wanasesere ni kitu gani? Wametuacha tuko busy tunamjadili Babu wa Loliondo wao nao wako busy kuangalia ni vp watalipa as soon as possible.

Mimi sina la kusema zaidi ya kumwomba Mungu ambaye ni mweza wa wote aingilie kati kwenye hili kwa kuwaadhibu wote wanaotaka kuwaibia watanzania maskini.
 
Hapa dhamira si kukatishana tamaa, tunataka 'Great Thinkers' tuziangalie kwa umakini hizi nondo na kuja na hoja za kuweza kubadili hali ya nchi. I believe we can, YES we CAN!

Serikali ya sasa imeshajichanganya kwa hili swala, kutegemea uchaguzi ujao nadhani tunajua kwa hali iliopo sasa si ya matumaini
Tukitegemea viongozi waliopo madarakani mi hahisi ni ngumu sana kwao, sio priority hata kidogo kwanza ni kinyume cha uelekeo wa wengi wao.

Kwa haraka, ni budi wananchi tuwaonyeshe kuwa nchi ni yetu, na tuko serious tunaitaka, na tunataka viongozi wa kututumikia sisi, sio wa kututumikisha sie.

Tunataka WOTE waliopitiwa na hii hela wote WAADHIBIWE kwa kufidia hii hela.

Hela isitoke TANESCO wala HAZINA. Hela yenyewe iko tu katika account za watu hawa hawa.

Naomba kutoka nje ya mada, hivi inakuwaje tunauziwa gesi yetu wenyewe ghali hivi, kwanini tusingechimba wenyewe labda tuweke amangement toka nje?
 
Mkuu Invisible,
Ukiweza lete documents za hayo maagizo ya wizara kwenda TANESCO ya kulazimisha hiyo mikataba tuone nani alisaini....huyo ndio atalipa au tutakufa naye...otherwise asante sana kwa kutujuza...japo umeniongeza hasira kwa hili....sikulaumu lakini
 
Back
Top Bottom