Comparing: Lowassa vs Pinda

Comparing: Lowassa vs Pinda

Jamaniee, mimi nachukia sana mafisadi, ila, kuna ishu moja hivi kila siku najiuliza, kipindi Lowasa yupo, pamoja na kwamba wanasema ni fisadi, lakini jamaa alikuwa anapiga mzigo ile mbaya, na nchi ilikuwa inachachamaa. Najua wengi watanipinga hapa, lakini wapinge wakitoa data halisi. Na kama hii thread ataisoma waziri Pinda, basi na iwe challenge kwake.

Lowassa alikuwa anahamasisha sana shule, shule zilijengwa ile mbaya, watu walikuwa hawalali au kuzubaa manake alikuwa na dictatorship akikukuta umeboronga anakuondoa kazi hapohapo. Shule zimejengwa kile mahali huko vijijini. Lakini toka huyu jamaa aingie, naona mambo yake ya polepole tu, anaongea zaidi ya kutenda ati. halafu ni mpole nashindwa kumdescribe you know.

Sio kwamba namchukia huyu Pinda au namfagilia Lowassa kutokana na madhambi yake, nahisi hii inatakiwa iwe challenge ya pinda. Semeni wenyewe, pinda amefanya nini hadi sasa ivi, mambo yake ni kuitetea selikali tu halafu anaenda kulala home kimyaa, si mtu revolutionary kabisa. Wanaomtetea walete zao, na ikumbukwe kuwa, kwenye post zangu za mwanzo, mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanzakwanza kumponda Lowassa, so, sitaki watu waseme nimetumwa na Lowassa hapa, naongea kitu ambacho nakiona. Hivi hapa TZ tunahitaji kiaongozi gani sana, mbona wote hawaleti matumaini?

Shule zimelala kabisa huko vijijini, toka Lowassa aanzishe akatoka, zikalala toka siku hiyo, mambo mengi yaliyokuwa yanaenda moto yamelala fofofo toka jamaa aachie ngazi. Yeye mwenyewe alikua kazi ilivyokuwa inapigwa ndo maana alikuwa na confidence ya kusema"naachia ngazi" because alijua watz tunamhitaji. We don't need him any more, lakini tunataka moto kama wakwake tafadhali. Shule hazina waalimu, waalimu wengi wanapanga kugoma. Pinda hafanyi chochote kile.

Naombeni mnilinde wajameni....

Ulichosema ni kweli! Simply put Pinda ni technocrat zaidi (tena siyo mzuri sana) wakati Lowassa ni Leader ndio maana anakomandi support kubwa zaidi ya Pinda ndani ya CCM.

Position ya PM inahitaji kuwa na Kiongozi anayeweza kufanya maamuzi mazito na kwa haraka kama alivyo kuwa Lowassa. Pinda as a person hana shida kabisa ni mtu mzuri tu huenda kuliko Lowassa lakini kiutendaji yuko extremely weak.

Pinda amekuwa ajitahidi sana kukwepa Lawama at any cost, mfano swala la umeme pamoja na weakness kubwa zinaonyeswa na Ngeleja na wenzake waziri mkuu ameshindwa kuingilia kati pamoja na shida zote wanazopata wananchi.
 
..serikali imeliona hili..tumelichukua, tunalifanyia kazi..naamini huu mchakato utatupa picha halisi ilisisi hapa serikalini tulifanyie kazi..haya ndo majibu ya pinduka wakati mtu kamuuliza issue ya maana, na inayoitaji majibu ya msingi
 
Ni kweli Lowasa alikuwa chapa kazi kuliko Pinda ila alikuwa mwizi mno na mbabe kupindukia! kwa mtaji huo nashindwa kubalance kwani naye Pinda kazidi kupindisha mambo kwa minajiri ya ama kuwalinda mafisadi ama kuwagwaya, yaani kazidi mno upole ama ndo hivo naye wameisha mteka kama mkuu wa Kaya!

Heri adui mwerevu kuliko rafiki mpumbavu!
 
Hivi Pinda na Lowasa nani zaidi kwa kuchapa kazi kama waziri mkuu wa Tanzania yetu?
 
pinda hana lolote kwa lowasa,isipokuwa lowasa ni fisadi
 
pinda hana lolote kwa lowasa,isipokuwa lowasa ni fisadi

Well summarised!! Kingine kinachotia doa kwa EL ni kwamba anachukua maamuzi kwa pupa, kabla hajafikiria implications za maamuzi yake
 
Pinda mwenyewe ameshasema kuwa tatizo kubwa linalozikabili nchi za Afrika ni viongozi... kwa hiyo yeye na Lowassa hakuna kitu, wote ni matatizo tu
 
Wote hawafai kwa sababu wako Chama Cha Mafisadi. Huko CCM hakuna mweama hata mmoja yote ni mifsadi papa tu.
 
LOWASSA ni sepp blatta na PINDA ni tenga! hakuna ulinganifu. upupa wa lowasa ni bora kuliko kutokufanya kitu kbs. pinda hana maamuzi....
 
Ni ishara mbaya sana kwa nchi kama viongozi wawili wanaofananishwa mmoja ni accidental prime minister na mwingine ni fisadi. Inaonyesha nchi ina upungufu wa viongozi. So sad.
 
Tunatakiwa tuwasahau wooote. We need to start afresh, hii recycling ya leadership ikome.
 
Kwa mtazamo wangu yawezekana kabisa mmoja akawa zaidi ya mwenzake kwani Kiongozi kama waziri mkuu anapimwa kwa uwezo wake wa kuchapa kazi na uwajibikaji na hasa ule uwezo wa kuthubutu.Angalia hivi vigezo halafu utajua nani kati ya hawa wawili ni zaidi ya mwenzake.

1.Uwezo wa kuchapa kazi
Kwa lowasa ni kweli mchapa kazi haswa kwani ni mambo mengi tu amelifanyia hili taifa,achilia mbali mambo yake ya ufisadi.Huyu ni kiongozi asiyependa kukaa ofisini na kungojea taarifa,huwa anapenda kufuatilia kwa ukaribu sana mambo yanayohusu uongozi wake kwa taifa.

Kwa pinda si mchapa kazi sana ila ni mtu wa kujaribu kuonyesha kama anaguswa na matatizo ya wananchi lakini huwa hana uwezo wa kuyafanyia kazi kwani ni muoga sana wa kufanya maamuzi magumu.Huwa anategemea sana msukumo kutoka nje ya nafsi yake ili atende anachoamini na hata wakati mwingine asichoamini pia.

2.Uwezo wa kuthubutu
Kwa lowasa hili halina mjadala, kwani ameshaonyesha ni kiongozi anayeweza kuthubutu kwani ameshachukua maamuzi magumu sana kwa manufaa ya taifa hili.Mfano mkataba wa City water na Pale alipoamua kujiuzulu uwaziri mkuu kwa manufaa ya taifa hili.

Kwa pinda hapa ninapata mashaka sana kwani hana ile sifa ya kuthubutu.Huyu kiongozi wetu anaweza akaishia kulia tu kwa mambo ambayo yanataka yeye kama Kiongozi mkubwa atoe uamuzi au achukue hatua.Mfano ni Mauaji ya albino na hata alipoambiwa akomeshe matumizi mabaya ya pesa za serikali aliishia kujikomesha yeye tu kuwaacha wengine wakiponda raha na magari ya kifahari.

3.Mpenda watu
Kwa lowasa ni kweli lowasa anapenda sana watu japokuwa hapa ana tatizo la kupenda sana watu kwa manufaa ya kitu fulani.Kama binadamu ana mapungufu yake katika hili lakini bado huwa anapenda sana watu wake.Ukitaka mfano mzuri nenda kwake Monduli utasimuliwa kuhusu huyu jamaa.

Kwa pinda hili halina mjadala kwa sababu pinda ni mtu wa watu na anawapenda sana na pia watu wanamkubali kwa upendo wake.Ukifika nyumbani kwao Kibaoni, utasikia sifa zake kwani yuko karibu sana na watu wake na pia watu wake wanamkubali sana.

4.Kukemea uzembe
Kwa lowasa hapa halina mjadala kabisa, huyu bwana anaweza sana kukemea wazembe.Mfano ameshawahi kuthubutu kuwafuta watendaji wabovu kazi.Pia huwa anaweza kukemea utendaji mbovu wa kazi wazi wazi.

Kwa pinda hapa pia ni tatizo sana kwake ,huwa ana tabia ya woga sana katika hili kwani anaogopa sana kulaumiwa. Hapa inategemeana na namna gani atapata msukumo kutoka nje ya nafsi yake ili aweze kutekeleza.

5.Uadilifu
Kwa lowasa hapa ndipo panakuja kuwa tatizo kubwa sana kwake,kwani huwa anapenda sana kujilimbikizia mali,hili alishawahi kuambiwa na mwalimu kuwa ana uchu sana wa kupata mali.Hili linampelekea kukosa kabisa uadilifu kwa jamii.

Kwa pinda hapa hapana sana mashaka kwani ameonyesha ni jinsi gani alivyo muadilifu kwani amefanya kazi idara nyeti za serikali na hadi sasa hana tuhuma yoyote mbaya.Nimeanza kupatwa kidogo na wasi wasi jinsi anavyopigania posho za wabunge,hapa inabidi tumuone atakavyolichukulia hili suala la posho.Tumpe muda.

HITIMISHO
Binafsi kwa kuwalinganisha hawa viongozi wawili yaani Lowasa na Pinda, mimi kwa mtazamo wangu namuona Lowasa anafaaa kuliko Pinda.Huu ni mtazamo wangu tu wana JF.
 
u
Well summarised!! Kingine kinachotia doa kwa EL ni kwamba anachukua maamuzi kwa pupa, kabla hajafikiria implications za maamuzi yake
.Huko kufikiria kwa mda mrefu ndiko kunakosababisha urasimu.Na urasimu ndio baba wa rushwa zote nchini.Lowasa ni mara 200 zaidi ya pinda bana!..
 
lowassa is handsome; Pinda is ugly.

the only thing they share in common is both worked under a lazy president.
 
Back
Top Bottom