Comparing: Lowassa vs Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Comparing: Lowassa vs Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kidzogolae, Sep 26, 2008.

 1. Kidzogolae

  Kidzogolae Senior Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaniee, mimi nachukia sana mafisadi, ila, kuna ishu moja hivi kila siku najiuliza, kipindi Lowasa yupo, pamoja na kwamba wanasema ni fisadi, lakini jamaa alikuwa anapiga mzigo ile mbaya, na nchi ilikuwa inachachamaa. Najua wengi watanipinga hapa, lakini wapinge wakitoa data halisi. Na kama hii thread ataisoma waziri Pinda, basi na iwe challenge kwake.

  Lowassa alikuwa anahamasisha sana shule, shule zilijengwa ile mbaya, watu walikuwa hawalali au kuzubaa manake alikuwa na dictatorship akikukuta umeboronga anakuondoa kazi hapohapo. Shule zimejengwa kile mahali huko vijijini. Lakini toka huyu jamaa aingie, naona mambo yake ya polepole tu, anaongea zaidi ya kutenda ati. halafu ni mpole nashindwa kumdescribe you know.

  Sio kwamba namchukia huyu Pinda au namfagilia Lowassa kutokana na madhambi yake, nahisi hii inatakiwa iwe challenge ya pinda. Semeni wenyewe, pinda amefanya nini hadi sasa ivi, mambo yake ni kuitetea selikali tu halafu anaenda kulala home kimyaa, si mtu revolutionary kabisa. Wanaomtetea walete zao, na ikumbukwe kuwa, kwenye post zangu za mwanzo, mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanzakwanza kumponda Lowassa, so, sitaki watu waseme nimetumwa na Lowassa hapa, naongea kitu ambacho nakiona. Hivi hapa TZ tunahitaji kiaongozi gani sana, mbona wote hawaleti matumaini?

  Shule zimelala kabisa huko vijijini, toka Lowassa aanzishe akatoka, zikalala toka siku hiyo, mambo mengi yaliyokuwa yanaenda moto yamelala fofofo toka jamaa aachie ngazi. Yeye mwenyewe alikua kazi ilivyokuwa inapigwa ndo maana alikuwa na confidence ya kusema"naachia ngazi" because alijua watz tunamhitaji. We don't need him any more, lakini tunataka moto kama wakwake tafadhali. Shule hazina waalimu, waalimu wengi wanapanga kugoma. Pinda hafanyi chochote kile.

  Naombeni mnilinde wajameni....
   
 2. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namshangaa JK sijui ana nini na Pombe Magufuli.Pamoja na kasoro zake lakini angepewa kazi kama hii,sasa hivi tungekuwa tunasimulia mengine kabisa.
   
 3. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mimi naona bora Lowasa mara mia. kwani pinda kafanya nini cha ziada hadi sasahivi?, hajamfikia kabisa Lowasa hata nusu tu. cha kwanza anatakiw akutilia mkazo elimu kama mwenzie alivyokuwa anafanya, aendelee kujenga shule na kuhakikisha waalimu wanapata pesa nzuri. kila siku watz wanalalama tu kuwa wakenya wamesoma kuliko wao, Lowasa hilo alikuwa analitilia mkazo sana, elimu. kusema ukweli, mimi mwenyewe kimoyomoyo namkumbuka sana yule jamaa. pamoja na kwamba wanasema fisadi, mimi sina evidence, ila naamini kuwa yukohivyo, bila evidence....lakini alikuwa anafanya mambo kwa nguvu sana, na kama tungalipata kiongozi kama yule akawa sio fisadi,kweli jamaa ni mchapakazi.
   
 4. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ukweli nimeuona.

  Japokuwa Lowasa alituhumiwa kuwa alishiriki sakata la RIchmond, Lowasa ni chapakazi. I can see the difference in short time.

  Nachukia mafisadi, lakini Nahisi Lowasa ameshajifunza. Kama ni mtu mwenye utashi na akili atakuwa makini katika maamuzi ya Tenda.

  Naomba au Nashauri apewe Unaibu Uwaziri Mkuu. Hii inawezekana. Hata Kipindi kile Mzee Ruksa alimpa Mhe Lyatonga Mrema Unaibu.

  Hapo vipi wadau
   
 5. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kujenga mashule bila walimu kazi bure ukienda sehemu nyingine shule kibao hakuna walimu na waliopo yebo yebo kuwalipa hawataki tatizo ndio hilo alitaka kuweka historia yeye alijenga shule nyingi cha msingi ni kuandaa kwanza walimu na mitaala ya elimu sio kujenga tu shule

  kwa ufuatiliaji maybe lowasa alikua anafuatilia ila kwa style ile udictator sehemu nyingine noma ili kua nafikiri baadhi ya watendaji walishukuru sana kuondoka kwake
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  difference ipo wazi wazi wakuu, unajua hawa mawaziri tumewalipa sisi watz kwa kodi zetu, kwahiyo kama mtu anakuja pale hachapi kazi, ina maana tunatakiwa kumpa warning halafu tunampiga chini. Pinda lazima achape kazi kama mwenzie alivyokuwa anafanya,kama anashindwa, alale mbele awaachie wenzie.
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Once Fisadi always Fisadi..... heri ya hiyo mizengwe uliyopinda!
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kazi anafanya,tatizo ufisadi.Inawezekana Pinda hajui kuwa yeye ni Waziri mkuu,kwa sababu alipokuwa serikali za mitaa alifanya kazi vizuri
   
 9. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hivi wewe unafikiri tz wanashindwa kuwalipa waalimu hadi kule vijijini? unafikiri wanashindwa kuwapeleka waalimu kule kwenye shule vijijini? wanaweza, ni uamuzi tu. ninachoafiki kwa huyo jamaa hapo juu ni kwamba, lowasa alijenga shule sana, in the process kwamba angeleta waalimu, akaachia ngazi, sasa waliochukua ngazi ndo wanatakiwa wapeleke waalimu kule. kupeleka waalimu kwenye shule kule vijijini kwetu, hawaendi na magari, wanaenda kwa mshahara mzuri unaolipwa promptly...wakilipa mshahara mzuri ,watu wataenda hata kama kijiji cha mwisho, maadamu inalipa. selikali inazo hizo hela, ila imeshindwa kuzipangilia tu. wakenya na waganda ndo wanazidi kupiga bao tu, sisi tunashangaa mashule matupu wakati wajinga wamejaa mtaani hawaendi kusoma..
   
 10. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unajua mkuu mimi swali hili najiuliza kila siku,kwani magufuli amemkosea nini kikwete au ni kwa sababu yuko karibu sana na che Nkapa,au inawezekana hayumo katika mtandao!Maana naona kikwete amezamilia kabisa kumpoteza,lakini mie kila siku nasema kipaji hata siku moja akipotei.Si mnaona kampeleka uvuvi kumechangamka,najua ataipa jina wizara ya uvuvi mwisho wa siku watamnyang'anya,lets wait and see.pamoja na mapungufu yake,jamaa anafaa kuwa kiongozi wa watu.
   
 11. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,782
  Likes Received: 1,961
  Trophy Points: 280
  Lowasa hakuwa mchapakazi kama baadhi ya watu wanavyojaribu kumpigia debe. Yeye ni mtu ambaye ni mlevi wa sifa, alivitumia vyombo vya habari na wanahabari wengi kumjenga kwa kumwandika na kumtangaza. Sio siri kwamba kutokana na njaa ya wanahabari wetu, waliifanya kazi hiyo na wataendelea kuifanya kwani mwenye njaa hana mwiko
   
 12. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naomba nitofautiane nawe kidogo mkuu.Kati ya shule na mwalimu nini kitangulie.Kwa tanzania yetu hii,ni bora itangulie shule kisha tutatafuta walimu.Kwangu mimi jamaa alikuwa sawa kabisa kujenga shule kwa fujo,kwa kila kitu kinaenda hatua kwa hatua.

  Nakubaliana nawe kwamba kuna sehemu lowasa alikuwa anachemka,lakini ile aina ya ufuatiliaji iliwafanya hata wavivu wafanye kazi,you can now sense the difference
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  very big difference, nafikiri kama jamaa wanavyosema,basi hata magufuri tu atie timu. but thisshould be the last resort, cha maana, Pinda ajifunze na aanze kubadilika,hii iwe challenge kwake.
   
 14. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #14
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ishu nikwamba kujenga shule kulikua kwa lazima kupita kiasi,pili hata hakukua na uwiano na kuwasomesha walimu,na strategy walio tumia ya kuchukua tu wanafunzi wa darasa la saba as walimu sijui gared gani hilo lilikua si sahihi kwa mtazamo wangu,mana wale failer woe walikua wanaenda kule sio kwa moyo wa kuwa walimu bali as source of being employed!!! ili takiwa kuwe na uwioano katika haya yote. wakuu
   
 15. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hakuna hata sehemu moja waliyochukua darasa la saba kuwa waalimu, shule tunazoongelea hapa ni shule za secondary mkuu, sio primary schools kwasababu kama ni primary schools hapa tz hatuna kabisa hili tatizo.hata kama lipo ni dogo. waalimu unaotakiwa kulalamika ni wanafunzi wanaomaliza form six, walikuwa wanaenda kuwabrush halafu wanaenda kufundisha form one na form two secondary,kitu ambacho sio cha ajabu. form six atashindwaje kumfundisha mtu wa secondary? ni mwalimu tosha anachokosa pale ni maadili ya ualimu tu, ila elimu yake inatosha kufundisha secondary. naomba kucorrect kwa namna hii.
   
 16. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ni kweli Lowasa alikuwa chapa kazi kuliko Pinda ila alikuwa mwizi mno na mbabe kupindukia! kwa mtaji huo nashindwa kubalance kwani naye Pinda kazidi kupindisha mambo kwa minajiri ya ama kuwalinda mafisadi ama kuwagwaya, yaani kazidi mno upole ama ndo hivo naye wameisha mteka kama mkuu wa Kaya!
   
 17. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,265
  Likes Received: 4,238
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Lowasa ni ufisadi but jamaa ni mchapakazi kuliko Pinda
  Huyu Pinda namuona kama ROBOT linaloendeshwa kwa remote
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unamsifia Lowassa kwa kutumia mfano wa shule tu na katika hilo, yeye ndiye aliyesababisha matatizo yaliyopo i.e amejenga shule nyingi bila kuwa na mpango wa kuongeza walimu. Matokeo yake, Pinda sasa hivi anahangaika kurekebisha makosa yaliyofanywa na Lowassa na kwa sababu makosa yalikuwa makubwa (shle zimeenea vijijini kote kama ulivyosema), itachukua muda kwa Pinda kuweza kurekebisha kasoro zote na kuanza kufanya mambo unayoyatarajia
   
 19. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bottom line, there must be ZERO TOLERANCE kwa mafisadi, no matter uwe umefanya nini. Umejenga shule nyingi kwa nguvu za wananchi fine. what about kulicost taifa 152million a day kwenye RICHMOND?.... Zingejenga shule ngapi over the course of say three years.

  Tatizo la EL ni "kilema cha ufisadi"..., sababu kama hela ya kuishi vizuri, tayari anayo nyingi tu, hata kabla ya mdudu RICHMOND.

  Tatizo kilema kile wandugu.... kitatumaliza mpaka mifupa akipata nafasi.
   
 20. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tuna 3 month before the end of the year...we need to focus kwenye personal commitment na kushauliana tumefanya nini mwaka huu na tuna panga kufanya nini next year...kwa ujumla pinda atakuwa waziri till next year...kabla muugwana hajapata moto...

  lets focus kwa wana jamii forum tushauliane what to do next..year kifamilia...kimaendeleo...etc...
   
Loading...