Comparing: Lowassa vs Pinda

Comparing: Lowassa vs Pinda

Mh.Pinda ni zaidi.Hana jazba,msikivu na msiri sana.Yeye ndio amemaliza upinzani wa CCM na CHADEMA,wanamjua ktk maswali ya papo kwa papo ni Genius huyu.Na akitia jina katika kugombe u-Rais 2015 kwa tikiti ya CCM,Dr.Slaa kwishinee.Kwanza hana kashfa toka enzi ya Mzee Kifimbo si wa mchezo huyu. Tuone 2015 atafanya nini huyu.

hacha mizaa kwenye mambo ya maana
 
Kwakweli pamoja lowasa ni fisadi hatuwezi kumfananisha na pinda, yana pinda na lowasa ni sawa na

dar to kenya.

Pinda dhaifu sana alaf hataki kujiuzulu ana penda sana rushwa ya mbuzi.
 
Mh.Pinda ni zaidi.Hana jazba,msikivu na msiri sana.Yeye ndio amemaliza upinzani wa CCM na CHADEMA,wanamjua ktk maswali ya papo kwa papo ni Genius huyu.Na akitia jina katika kugombe u-Rais 2015 kwa tikiti ya CCM,Dr.Slaa kwishinee.Kwanza hana kashfa toka enzi ya Mzee Kifimbo si wa mchezo huyu. Tuone 2015 atafanya nini huyu.

Kiatu alichovalishwa pinda nikikubwaaaaa sana kwake! Hata ukijaza makaratasi bado kitaendelea kumpwaya sana! Toka ameteuliwa haishi kwenda kwa RAISI kulalama kila siku, hana maamuzi hata ya kumwambia tunu atamke jina la Barbra kwa ufasaha! uwezo wake unaishia kutumwa zaidi na anahitaji wa kumsimamia constant...

Lowassa amedhihirisha wazi kuwa yeye ni kiongozi result oriented...Mfumo mbaya plus fitna za akina membe ndo zilizomletea shida lakini kwa kujua maana ya uwajibikaji ili kumnusuru rais na chama chake aliamua kuachia ngazi kijasiri na hakuendelea tena kulalama...Matokeo yake rais ndo alikuja kushtuka usingizini na kuanza kumsafisha kwa kuwaambia watanzania kuwa rafiki yake amepata ajali ya kisiasa!!! angekuwa muungwana angeliambia taifa kuwa deal la richmond ilikuwa ya taifa kubwa duniani USA na iliratibiwa kwa karibu na mwanae MIRAJI!!!

Tunajua hofu ya CIA ili kuwa kwa lowassa kiongozi pekee mwenye uwezo wa kusitisha mikataba ya kishenzi!!! ona land grabbers thru pinda na membe wanavyoendelea kuchukua ardhi yenye rutuba mahekta kwa mahekta! hakuna wa kuongea! Symbion walikuja kuthibitisha kuwa deal la richmond ilikuwa la USA, nani aliongea baada ya hapo? URANIUM wanachimba tena kwenye hifadhi ya taifa!!! Mkuu wa kaya kila baada ya mwezi anatakiwa kwenda kupeleka progress report USA! nani anauwezo wa kuhoji?

Pinda angekuwa na uwezo asinge ruhusu ujinga wa kuwaua wazawa kwa kisingizio cha kuwalinda wawekezaji na hofu ya serikali kupingwa!! Pinda hafai kuwa kiongozi ktk level ya kuhusisha wananchi... yeye ni wakutumwa kazi tu za ndani na zisizoonekana kama prof maji marefu...
 
lowasa kichwaaa balaaa!!!kwanza anajiamini halaf anajua anachokifanya na anakubaliana na hali halisi ispokua anajilimbikizia mali sana hapo kwenye ufisadi tuu ndio kamshinda pindaa😡
 
Haaaaaah! Pinda ni zaidi ya Lowasa: 1. ni mtaalam wa kulia hovyohovyo, 2. mtaalam wa kutoa kauli tata, 3.mtaalam wa kujibu maswali ya PUPA kwa PUPA na mengine mengi unaweza kuongeza, 4.....,5...........
 
EL aliacha pengo kubwa ktk utendaji serikalini. Miaka minne sasa ombwe la uongozi ni kubwa ajabu. Tukio la jana la kutekwa kwa Dr. Ulimboka na watu wanaodhaniwa ni maafisa wa usalama wa taifa,ni kielelezo cha uchovu wa hali ya juu serikalini na aibu kubwa kawa taifa. Imenikumbusha matukio ya Zanzibar,2001 na yale ya Arusha mwaka jana.
 
Lowassa Captain wa Jeshi mnamfananisha mtu ambae maisha yote yeye Sekretari tu
 
nimemkumbuka sana huyu baba(Lowasa)...tokea jana....
 
Lowassa moto! Na JK alimwogopa sana, ndo mana kamzamisha even if Richmond was Kikwete's mistake when Lowassa wanted to stop their contract JK called him from abroad akamwambia usiwafukuze, bomba lilipolipuka Lowassa kabeba peke yake msalaba
 
Jamaniee, mimi nachukia sana mafisadi, ila, kuna ishu moja hivi kila siku najiuliza, kipindi Lowasa yupo, pamoja na kwamba wanasema ni fisadi, lakini jamaa alikuwa anapiga mzigo ile mbaya, na nchi ilikuwa inachachamaa. Najua wengi watanipinga hapa, lakini wapinge wakitoa data halisi. Na kama hii thread ataisoma waziri Pinda, basi na iwe challenge kwake.

Lowassa alikuwa anahamasisha sana shule, shule zilijengwa ile mbaya, watu walikuwa hawalali au kuzubaa manake alikuwa na dictatorship akikukuta umeboronga anakuondoa kazi hapohapo. Shule zimejengwa kile mahali huko vijijini. Lakini toka huyu jamaa aingie, naona mambo yake ya polepole tu, anaongea zaidi ya kutenda ati. halafu ni mpole nashindwa kumdescribe you know.

Sio kwamba namchukia huyu Pinda au namfagilia Lowassa kutokana na madhambi yake, nahisi hii inatakiwa iwe challenge ya pinda. Semeni wenyewe, pinda amefanya nini hadi sasa ivi, mambo yake ni kuitetea selikali tu halafu anaenda kulala home kimyaa, si mtu revolutionary kabisa. Wanaomtetea walete zao, na ikumbukwe kuwa, kwenye post zangu za mwanzo, mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanzakwanza kumponda Lowassa, so, sitaki watu waseme nimetumwa na Lowassa hapa, naongea kitu ambacho nakiona. Hivi hapa TZ tunahitaji kiaongozi gani sana, mbona wote hawaleti matumaini?

Shule zimelala kabisa huko vijijini, toka Lowassa aanzishe akatoka, zikalala toka siku hiyo, mambo mengi yaliyokuwa yanaenda moto yamelala fofofo toka jamaa aachie ngazi. Yeye mwenyewe alikua kazi ilivyokuwa inapigwa ndo maana alikuwa na confidence ya kusema"naachia ngazi" because alijua watz tunamhitaji. We don't need him any more, lakini tunataka moto kama wakwake tafadhali. Shule hazina waalimu, waalimu wengi wanapanga kugoma. Pinda hafanyi chochote kile.

Naombeni mnilinde wajameni....
Wana jf tofauti ya lowasa na pinda ni hii,nitawaeleza kwa kutumia mfano.Kama Pinda au Lowasa mmojawapo amekuta duka la radio linaungua,Lowasa atachukua maamuzi yafuatayo,haraka ataita watu wa kuzima moto huku akiwa ameandaa watu wa kusaidi kutoa radio ambazo hazijaungua,wakati wanatoa atawaambia wasaidizi wake kuwa kila wakitoa radio kumi basi moja iingizwe kwenye gari lake na hiyo itaenda kwake. Juhudi zake zitaokoa baadhi ya radio ingawaje kiasi cha radio ataondoka nacho.Sasa Pinda atakapokuta the same situation,kwanza atapenda kabla ya kuanza kuokoa watafute mtaalamu wa kutoa definition ya moto,aina ya moto,chanzo chake,pia atataka kujua ndani kuna nini,cha thamani gani,mwenye nacho ni nani,huwa analipa kodi au la. Mwisho duka linateketea,alafu anasema aaaaaaaah liwalo na liwe.To me lowasa is the best.
 
mnafananisha usiku na mchana?
Hata mimi nashangaa ni sawa na kumfananisha huyu Makamba na Kamanda Mnyika, yaani kilaza na kipanga! Wapi na wapi bana!! Labda wangesema tu mmoja ni nweupe na ana nywele nyeupe na mwingine ni mweusi na ana nywele nyeusi!
 
Inastaajibasha kuona kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda hakutoa kauli yoyote
wakati huu ambao taifa linapita katika majaribu magumu Kama Kuuliwa kwa RPC wa Mkoa wa Mwanza, Kuchomwa kwa makanisa huko mbagala, kupigwa bomu kwa Katibu wa BAKWATA Arusha, Kutangazwa kwa baa la Njaa Mkoa wa Tanga nk! Taifa linapitia wakati Mgumu na kibaya zaidi ni kuwa Serikali imekuwa kama haina Waziri Mkuu. Amani imetoweka. Hofu katika mioyo ya wananchi imetamalaki. Wananchi wanaishi katika wasiwasi mkubwa huku kanisa likilia machozi! Kwa tishio kubwa kwa
amani ya nchi kama hili waziri mkuu kuwa kimya na kuonekana kama hayupo haliwezi kunyamaziwa hata kidogo!


Msomaji mmoja kutoka Njiro, Arusha akaniandikia, alisema “Umesema kweli mwalimu mkuu wa watu, Pinda siyo kama hayupo ni hayupo kabisaa! Mimi naona serikali yote haipo. Nchi imewashinda sasa wanyonge hatumwoni wakumshika mkono! Pamoja na yote Edward Lowassa ndo waziri mkuu pekee angalau alifanya kazi! Yaani haingii akilini mpaka sasa Pinda hajasema chochote, ama ni mgonjwa wametuficha?”

Rais Kikwete, Pinda lazima aliliwe hata kama mbingu zitaanguka kwasababu alipoteuliwa kuwa waziri mkuu aliwapa matumaini makubwa wananchi ingawa yeye mwenyewe hakujua! Wananchi walijawa na matumaini makubwa kwasababu Mizengo Pinda wakati hila za kutafuta madaraka zilipokuwa zikifanywa na baadhi ya viongozi waliopo madarakani hivi sasa yeye hakuwa mmoja wao! Hivyo wananchi walidhani angekuwa na nafasi nzuri ya kuwa upande wao kwa maana wametelekezwa! Yeye hakuwa katika
majadiliano na wafanya vurugu wa sasa! Hawamdai kitu chochote. Kama vile haitoshi, serikali imetangaza balaa la njaa! Ukimya huu wa mtendaji mkuu ukiendelea unadhani nini kitatokea? Siyo kwakutaka kwetu bali tunalazimishwa kukumbuka balaa la njaa lililopita.

Tulishuhudia Waziri mkuu Edward Lowassa alivyokuwa wakihaha nchi nzima kuhakikisha maisha ya Watanzania hayapotei kwa sababu ya njaa. Nani asiyekumbuka ziara ya Waziri mkuu Edward Lowassa kule Same? Njaa imeshika kasi, wananchi wanataabika kwa njaa, mkurugenzi kakaa na mahindi ya njaa
ofisini! Eti Same yote hakukuwa na mtu mwenye uwezo wa kuyasafirisha. Mtu huyu hakuwa na kile wadhaifu wanaita maamuzi magumu. Aliamua mahindi yagawiwe kwa wananchi akiwepo! Wakati wakuondoka kurudi Dar es salaam akaondoka na mkurugenzi; kazi ya mkurugenzi ikawa imeisha.

Mwangwi wake ukaenea katika masikio ya wakurugenzi wote nchi nzima! Nani ataichezea serikali kwa kuwatesa wananchi? Kungekuwa na ukimya kama huu kule Same wangekufa wananchi wangapi?
Lazima Waziri mkuu atokeze aseme na wananchi wanaoishi kwa wasiwasi katika nchi yao. Atokeze awajibu Maaskofu wanaolia! Asimame akemee ugaidi huu! Maaskofu wanahoji, “Watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamuue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa Taifa letu?” Ni nini hiki wanachosema Maaskofu kuwa, “Katika mateso haya kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana?”


Labda Pinda anakuiga wewe Rais ulieahirisha safari ya kwenda nje kutokana na kifo cha mwigizaji wa michezo huku ukitoa ubani wa milioni kumi halafu ukaenda Oman wakati mauti yamemfika Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow? Au Labda ni Utamaduni wa Serikali yote ya awamu ya nne- Serikali ya Tanzani ni Muungano wa Visiwa Vya Zanzibar na Zimbabwe


PASCHALLY MAYEGA: KIPANDE CHA MAKALA GAZETI LA TANZANIA DAIMA 10-24-2012
TEL 0713334239
 
HAPA nawakumbuka marehemu wawili wote maarufu japokuwa umaarufu wao unatofautiana lkn wote wametoa wosia mbalimbali kwa taifa letu. ktk hoja hii ntamtumia marehemu DR Remmy Ongala alipoimba kipande cha maneno haya; niseme nini? niseme nini? sina la kusemaa na mwingine MWL NYERERE aliwashauri watanzania tumvumilie rais wetu wa awamu ya pili amalize muda wake,[tumvumilie Pinda amalize muda wake] maana jamaa karidhika na uwaziri mkuu hana cha kupotezaamekwisha sema hagombei tena hivyo hana kiu.
 
aiseeeeeee babaangu nasikia uchungu sana hapa ndipo ambapo naamini ikulu iliusika kumteka ulimboka pinda alikuwa mstari wa mbele kupinga akifwata na jk sasa mbona haya majanga yanayotokea yupo kimya au hayopo nchini
 
Back
Top Bottom