Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

serikali yetu inafungua tu magazeti yanayo elemisha kama vile ----------- na mwananchi na kusahau vyombo vingine vya habari vianavyo tanagaza anasa tupu kila kukicha kama vile EATV, CLOUDS FM NA TV, MAGAZETI YOTE YA UDAKU, ndiyo maana taifa hili haliwezi kuendelea angalia nchi kama china hakuna vyombo vya habari uchwara kama hapa kwetu...mfano magazeti ya udaku kila siku ni habari ya wema na diomond jamani taifa lina mambo mengi ya kuzungumzia....
 
Nilianzisha uzi kama huu mwaka jana kwenye kipindi hiki hiki, NI AIBU KUBWA

Mbeeeee! Yesuuuuuuuuu, Kumbe udhalilishaji huu ulianza muda mrefu hivyo? Sasa serikali iko wapi isiukomeshe? Ina maana TCRAwapo likizo au wana masilahi binafsi na udhalilishaji huu? How the hell can this particular discrimination persist for such a long time without any corrective action being taken? Hivi kweli kuna utawala katika nchi hii au hii ni nchi ya mahayawani? Nina hasira sana--ningekuwa gaidi leo hii ningejifunga mabomu niende kuilipua Clouds TV!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:

Ndiyo maana Jamii yetu imeharika si mdogo wa si mkubwa maana tumefika mahali tumekubali kila kitu nisawa.

Ebu pima na jifikirishe Bibi kumtongoza kijana mdogo ,hili linatupa elimu gani kwa vijana wadogo 2-12yrs . Naamini hiyo ni Elimu inatosha miaka mitatu mbele vijana tena wadogo watakuwa wakiwachangamkia Vibibi tena bila kusahau hawana cha kwenda Mwezi/wala Mimba hapo Upo?

Mie simo huu ushauri tu kuwa nivizuri kuepuka mambo haya!

Mkuu, asante kwa mchango wako. Kuna mjinga mmoja humu alidai kwamba sio lazima kila kipindi kielimishe. Sasa sijui haoni kama hiki kipindi cha BIBI BOMBA kinamomonyoa maadili ya jamii!
 
TCRA wako blinded na matukio ya clouds tv sababu inafanya kazi on interest za CCM na wao wako chini ya CCM na sio INDEPENDENT INSTITUTION
 
Kwa mara nyingine tena nimechukua jukumu la kuripoti huu udhalilishaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto, TAMWA, TAWLA, LHCR na TCRA (kwa mara nyinine tena, maana mara ya kwanza nimewatumia lakini sikupata feedback yoyote). Kama hata Wizara ya Maendeleo ya wanawake, wakigoma kuwachukulia hatua hawa akina Ruge basi tujue kwamba wameishaitia serikali mfukoni. Silaha pekee itakayokuwa imebaki, ni maandamano ya wananchi ili kupinga ukatili huu:
================================================================================================

Me
To dg@tcra.go.tztawla.information@gmail.comlhrc@humanrights.or.t and 2 More...
Today at 12:26 AM
Ndugu watanzania,

Clouds TV wamekuwa wakiwadhalilisha bibi zetu kupitia kipindi chake cha BIBI BOMBA kwa muda mrefu sasa. Nadhani sasa imefika wakati wahusika mchukue hatua ya kusitisha kipindi kile, kuwalipisha faini wahusika au kuwaelekeza namna nzuri ya kutangaza kile kipindi bila kudhalilisha wale watu wazima hadharani. Watu wengi hawapendezwi na udhalilishaji ule lakini hawana namna ya kufanya kuuzuia. Nchi inaendelea kupata laana mbalimbali kwa sababu ya udhalilishwaji wa wanaofanyiwa watu wazima kama wale, na bahati mbaya ni kwamba udhalilishwaji huu hufanywa na vijana wadogo kabisa kwa kisingizio cha kwamba wanawashindanisha (sijui kwa kitu gani).

Hata kama hawa bibi wanatoka kwenye familia masikini kiiwe kigezo cha kudhalilishwa hivyo. Elewa kwamba nao ni watu wanaostahili kuheshimiwa kama raia wengine katika nchi hii. Sidhani kama serikali haioni udhalilishaji huu au kama nyie mnaona ni sawa kipindi hiki kiendelee kuruka hewani. Hivi kweli ina maana hamjawahi kuona kipindi hiki? Kama bado hamjawahi kukiona basi nendeni pale Clouds TV muwaambie wawape ile mikanda waliowapiga wale kina bibi halafu muipitie muone kama kweli inakidhi vigezo vya TCRA. Kama miongoni mwenu hakuna anayeweza kukemea au kutoa adhabu kwa makosa kama haya, naomba suala hili mlipeleke kwenye kitengo kinachohusika ili Clouds TV wachukuliwe hatua zinazofaa kwa kuwadhalilisha bibi zetu bila sababu za msingi.

Asante kwa kunielewa na kwa kuchukua hatua zinazofaa dhidi ya ukiukaji huu mkubwa wa haki za binadamu.

Reply, Reply All or Forward | More
====================================================================================================

Hiyo hapo juu ni barua niliyowapelekea nikitatajia kwamba wataifanyia kazi. Nimetimiza wajibu wangu kama raia mwema ambaye nisingependa kuona bibi zetu wakidhalilishwa.
 
Last edited by a moderator:
Kama uongozi wa Clouds utatumia maoni yaliyotolewa katika uzi huu kwa lengo la kukiboresha kipindi hicho,itakuwa ni jambo muafaka sana.Ni muhimu kubuni vipindi vitakavyoijenga jamii na ndo maana vituo vya habari hulazimika kufanya utafiti ili kukidhi mahitaji.Lengo la kipindi cha Bibi Bomba liwe ni kuelimisha kwanza kwa sababu udhalilishaji wa kundi lolote ktk jamii ni kinyume cha maadili.
 
Yatoka kwa Mdau


SERIKALI IANGALIE UDHALILISHAJI UNAOFANYWA NA CLOUDSTV KUPITIA KIPINDI CHA BIBI BOMBA
Posted on May 19th


Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo–havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha ‘BIBI BOMBA' kinachorushwa na TV hiyo. Nimehuzunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.
Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa ‘Biology', akajibu ‘ndiyo'. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.
Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Kama kweli kinachofanyika katika kipindi kile ni kuwajali bibi wale kwa maana ya kuwapatia pesa wakishinda hebu wanaoendesha kipindi kile siku moja wawalete bibi zao na wawahoji maswali yale ya kishenzi tuone kama itakuwa sawa kwao, kwanini pesa iwe kigezo cha kudhalilisha watu wazima? Tena wanadhalilishwa na vijana wadogo wasio na chembe ya maadili? Hivi kweli kumwambia bibi mtu mzima amtongoze kijana mdogo halafu mbele ya skrini kila watu wa rika tofauti wanatazama wakiwemo watoto hapo tunafundisha maadili gani kwa jamii?
Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu–tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki
 
Inasikitisha sana kuangalia uzalilishaji wa namna ile! Serikali ichukue hatua mara moja!


Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
hayo ndo madhara ya kucopy kutoka Uzunguni. yani ni kweli wanawadhalilisha haomabibi. kwanza jina lenyewehalifai hilo ndipo walipokisea. wapuuzi hao waendesha kipindi
 
Yatoka kwa Mdau


SERIKALI IANGALIE UDHALILISHAJI UNAOFANYWA NA CLOUDSTV KUPITIA KIPINDI CHA BIBI BOMBA
Posted on May 19th


Mimi sio mtazamaji mzuri wa Clouds TV kwa kuwa vipindi vyake vingi ni vya ovyo–havina mvuto wala mafundisho ya maana. Jana, kwa bahati mbaya, nilitazama kipindi cha ‘BIBI BOMBA’ kinachorushwa na TV hiyo. Nimehuzunishwa sana kuona jinsi bibi na mama zetu wanavyodhalilishwa hadharani. Bibi zetu huulizwa maswali ya kidhalilishaji.
Bibi mmoja aliulizwa kama aliwahi kula mboga inayoitwa ‘Biology’, akajibu ‘ndiyo’. Hili ni swali linalohusu ufahamu na kwa wabibi wale ambao hawakwenda shule, hawajui biology ni nini. Si hivyo tu, hata wale walioishia la saba hawajui biology ni kitu gani. Kuwauliza mabibi swali kama hili ni kuwadhalilisha kitaaluma kwa kuwa tu hawakwenda shule.
Bibi mwingine aliombwa amtongoze kijana yule anayewauliza maswali hadi amkubali. Bibi akatekeleza agizo hilo laivu mbele ya skrini ya TV! Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Kama kweli kinachofanyika katika kipindi kile ni kuwajali bibi wale kwa maana ya kuwapatia pesa wakishinda hebu wanaoendesha kipindi kile siku moja wawalete bibi zao na wawahoji maswali yale ya kishenzi tuone kama itakuwa sawa kwao, kwanini pesa iwe kigezo cha kudhalilisha watu wazima? Tena wanadhalilishwa na vijana wadogo wasio na chembe ya maadili? Hivi kweli kumwambia bibi mtu mzima amtongoze kijana mdogo halafu mbele ya skrini kila watu wa rika tofauti wanatazama wakiwemo watoto hapo tunafundisha maadili gani kwa jamii?
Wizara ya jinsia inapaswa kukataza udhalilishaji huu wa kijinsia. Nasi wananchi tuache kushabikia upumbavu huu–tukatae kuwapigia kura bibi wanaoshiriki




SERIKALI IANGALIE UDHALILISHAJI UNAOFANYWA NA CLOUDSTV KUPITIA KIPINDI CHA BIBI BOMBA|Mtizamo Huru
Ukitaka kutazama hiyo tv au kusikiliza hiyo redio ya unatakiwa uwe mvuta bangi mnywa viroba na uwe umelelewa na wahuni ndo utaiona nzuri.Hawa watu ni majanga tena hawafai hata kwa matumizi ya binadamu hawana adabu wana nidhamu!!
 
Ile radio/tv huwa wanachukua tu watu ilimradi aweze kuongea ongea anapewa kipindi. Kulikuwa na namna nyingi za kuendesha hilo shindano, mfano bibi anayetunza zaidi tamaduni zetu za kitanzania, labda bibi mshauri mzuri kwa mjukuu mwenye matatizo, analetwa mtu mwenye tatizo liwe la ukweli au la bibi anaambiwa amsaidie hilo tatizo, lakini wao wanaendekeza udhalilishaji tu.
Usitegemee serikali kuikemea hiyo TV, labda kama ingekuwa inamilikiwa na watu wa Tanzania Daima.
 
nchi inaongozwa na majuha.. kwao kila kitu sawa tu.. kuna kipindi kipya wataanzisha kinaitwa "madada poa" kaa mkao wa kula..kiko jikoni
 
Mabadiliko yafanywe na sisi wenyewe watanzani!!
Kwa kua mwishon hua kunakua na maoni au ushaur kuhusu kipind husika kama wakiona kila atoae maoe hapendi ule ujinga wao mi naamin wataacha,,,,,,
Siipend clouds ndo mana hata vipind vyake sivitambui
 
yah nikweli mimi mwenyewe naonaga aibu kuangalia kile kipindi cha kihuni na akina mantiki.mamlaka husika waliangalie upya swala hilo.
 
Back
Top Bottom