Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

Clouds TV acheni kuwadhalilisha bibi, mama zetu!

kwa kweli naiomba serikali iiangalie clouds kwa jicho pana kuhusu hii bibi bomba ingekuwa na maudhui mengine ningeisapoti ila kwa hili naomba nitoe shilingi yangu...huu ni udhalilishaji wa wazee wetu halafu kwa kujua hilo wanalala kwenye mgongo wa ccm ili wasibugudhiwe....ngojea rais ajae tuone kama hawaja rudi enzi zao za disco vumbi
 
udhalilishaji wanaofanyiwa hawa wabibi haukubaliki duniani wala mbinguni. ngoja hao wachumia tumbo waendelee tu kudhalilisha watu lakini ipo siku moto utawawakia.

ukitaka kufannya uhalifu na usiguswe na mtu yeyote ktk nchi hii, basi egemea mgongoni mwa ccm na serikali yake--hata ukiwavua watu nguo hadharani hakuna atakayekugusa. nchi hii imeoza tangu nchani hadi shinani.

wanachokifanya clouds ni matokeo ya utawala goigoi usioweza kuwatetea wananchi wake.

lakini ipo siku uhuru wa wanyonge kama hawa 'bibi bomba' utapatikana bila shuruti. freedom and respect to common citizens' humanity & dignity is around the corner!
 
Hili tatizo nimeliripoti kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, TAMWA, TCRA, TAWLA, LHCRA na kila mahali lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyechukua hatua. Hata hawa TAMWA juzi tuliona wakiandamana kuwatetea wasichana wa Nigeria waliotekwa na Boko Haram, lakini hatujawahi kuwasikia wakiwatetea hawa mabibi zetu wanaodhalilishwa hadharani kama nyumbu wa Serengeti.

Nadhani Clouds TV wana ubia na CCM na serikali yake ndio maana wanavunja haki za binadamu bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria. Bw Asa Mwambene (Mkurugenzi wa Habari, Maelezo) anajua kufungia vyombo vya habari kwa maelekezo ya wanasiasa tu. Sidhani kama ana meno ya kuweza kuwazuia Clouds TV waache udhalilishajiwao huu. Mwaka wa jana tumeshuhudia Radio Clouds wakipigwa faini ndogo ya Tsh 5M huki Radio Imaan FM wakipigwa faini na kufungiwa kwa miezi 6 kwa makosa yanayofanana. Sababu ya Clouds kupigwa faini peke yake bila kufungiwa huku Imaan wakipata adhabu zote mbili kwa kosa lilelile wanazijua serikali ya CCM na mafisadi wake.

Nashangaa kwanini viongozi wa nchi hii wameamua kuziba masikio na kuvaa miwani ya mbao kwa matatizo yanayowasibu wanyonge. Nadhani kama ingekuwa bibi zao ndio wanaodhalilishwa kama hivi wasingekubali. Haya yote yanatokea kwa sababu ya utawala dhaifu wa serikali ya kifisadi ya CCM; na inaonyesha ni jinsi gani serikali ya CCM isipojali matatizo ya wanyonge. Lakini ipo siku ukombozi utapatikana na udhalilishaji kama huu utafikia kikomo. Tuombe Mungu atusaidie kuufutilia mabali utawala huu kengeufu na usiojali kero za walalahoi.
 
Du Jf ni kiboko wana jamii Ruge salam zimemfikia angalia milardayo tv akijijieleza
 
kwa kweli naiomba serikali iiangalie clouds kwa jicho pana kuhusu hii bibi bomba ingekuwa na maudhui mengine ningeisapoti ila kwa hili naomba nitoe shilingi yangu...huu ni udhalilishaji wa wazee wetu halafu kwa kujua hilo wanalala kwenye mgongo wa ccm ili wasibugudhiwe....ngojea rais ajae tuone kama hawaja rudi enzi zao za disco vumbi
wazo zuri... je hiyo serikali unayoomba iangalie kwa jicho pana ina macho??
 
clouds wamekosa ishu,ule n udhalilishaji mkubwa sana wa bibi zetu.serikali wakifunge hcho kipind.
 
Kwa kweli hata mimi nilishangaa sana nililovyoona hiki kipindi. Kuna siku bibi aliambiwa wacheze mziki. Bibi akaanza kukatika maskini. Dah nikijisikia vibaya sana. Utasema watangazaji hawana mama! Wao wangekubali mama zao wafanyiwe vile?
 
Ikiwa serikali hiyohiyo ndio hukitumia kituo hichohicho kwa propaganda chafu, ni vigumu sana ikachukua hatua,

Jamii kwaujumla ndio yenye dhamana ya kupaza sauti na kukemea haya.
 
Hili tatizo nimeliripoti kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, TAMWA, TCRA, TAWLA, LHCRA na kila mahali lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyechukua hatua. Hata hawa TAMWA juzi tuliona wakiandamana kuwatetea wasichana wa Nigeria waliotekwa na Boko Haram, lakini hatujawahi kuwasikia wakiwatetea hawa mabibi zetu wanaodhalilishwa hadharani kama nyumbu wa Serengeti.

Nadhani Clouds TV wana ubia na CCM na serikali yake ndio maana wanavunja haki za binadamu bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria. Bw Asa Mwambene (Mkurugenzi wa Habari, Maelezo) anajua kufungia vyombo vya habari kwa maelekezo ya wanasiasa tu. Sidhani kama ana meno ya kuweza kuwazuia Clouds TV waache udhalilishajiwao huu. Mwaka wa jana tumeshuhudia Radio Clouds wakipigwa faini ndogo ya Tsh 5M huki Radio Imaan FM wakipigwa faini na kufungiwa kwa miezi 6 kwa makosa yanayofanana. Sababu ya Clouds kupigwa faini peke yake bila kufungiwa huku Imaan wakipata adhabu zote mbili kwa kosa lilelile wanazijua serikali ya CCM na mafisadi wake.

Nashangaa kwanini viongozi wa nchi hii wameamua kuziba masikio na kuvaa miwani ya mbao kwa matatizo yanayowasibu wanyonge. Nadhani kama ingekuwa bibi zao ndio wanaodhalilishwa kama hivi wasingekubali. Haya yote yanatokea kwa sababu ya utawala dhaifu wa serikali ya kifisadi ya CCM; na inaonyesha ni jinsi gani serikali ya CCM isipojali matatizo ya wanyonge. Lakini ipo siku ukombozi utapatikana na udhalilishaji kama huu utafikia kikomo. Tuombe Mungu atusaidie kuufutilia mabali utawala huu kengeufu na usiojali kero za walalahoi.

hawajachukua hatua yoyote kwasababu hakuna sheria yoyote iliovunjwa. tunachokiona mimi na wewe ni udhalilishaji kwa wengine ni burudani ndio maana hiki kipindi kina watazamaji wengi na wadhamini ambao labda unatumia huduma zao na kwa kufanya hivyo unachangia udhalilishaji huu.

cha kufanya ni kususia huduma za wadhamini wa vipindi kama hivi,tena mnaweka wazi anaedhamini kipindi hiki huduma zake hatutumii wataacha kudhamini na kipindi kitaondolewa hewani, na nimeona kuwa hii ni SEASON 3 inaonyesha ni kipindi kinachopendwa.
 
Angalau hapa umeweka vijistop stop kwa mbaali.
Acha unapanic? Slow down....
Hiyo Ni Staili Yangu Na Nimeanza Nayo Na Nitamaliza Nayo Na Huna Huwezo Wa Kunibadilisha. Ungekuwa Na Akili Ungekuwa Unajibu Hoja Na Kuwa Na Tabia Za Kike Kike Na Za Kishoga. Na Pia Huwa Sipendi Sana Kujibizana Na Senior Member Kama Wewe Humu JF Bali Nabishana au Najenga Hoja Na Tunaolingana Kiupeo Humu JF na Ambao Ni Wengi Sana. Tafuta Wa Saizi Yako Na Usitafute KIKI Kupitia GENTAMYCINE. Mbwiga Mkubwa Weye................... USILETE VITA YA MAWE na MIMI WAKATI UNAISHI KTK NYUMBA YA VIOO na Bahati Mbaya AU Nzuri Nimeiga Utaratibu Wa KIYAHUDI Ambapo Ukijamba tu Mimi Naharisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mimi nilikuaga mfuatiliaji mzuri sana wa vipindi vya clouds , lakini kipindi kama kile cha saa kumi cha kina kibonde kilinifanya niachane kabisaa na hiii radio, watu w azima kazi kuongea upuuzi na kucheka ovyo kama mashoga, yani wanaudhi sana, upuuzi ni mwingi sana kwenye vipindi vyao.

Mkuu umenena! Hivi Kibonde ni mzima kweli? nimeichukia sana radio kwa vipindi vyao pia , ni upuuzi mtupu.
 
Clouds TV (Ruge na team yake) mlipoanzisha shindano hili la BIBI BOMBA nilifikiri wanataka kuwatumia bibi hawa kwa ajili ya kutukuza uTanzania wetu, utamaduni wetu na mchango wao ili kufanya vijana wafahamu utamaduni wetu ambao unaanza kusahaulika katika jamii. Lakini tunachokishuhudia hivi sasa ni kinyume chake. Ni udhalilishaji usiovumilika wanaofanyiwa bibi na mama zetu. Haingii akilini kumuimbisha bibi wa miaka 65- 70 nyimbo za muziki wa kizazi kipya au kumvalisha suruali wakati tunazo nyimbo zetu za kabila mbalimbali na pia tunafahamu kabisa katika maisha ya kawaida bibi hao hawavai hivyo!

Ruge umekosea sana(wewe ndiye msimamizi wa TV yako kufanya marekebisho. Jipe muda fuaitili shindano hilo uone kama kuna lolote la maana jamiiinajifunza. Badili maramoja; itapendeza na kuleta maana zaidi kama bibi hawa watashidanishwa kwa mambo yenye maadili na kudumisha utamaduni wetu Watanzania

EJL
Ni kweli unachokisema, TV one wanakipindi huleta kutoka Nigeria kinaitwa Pamper your mum. wangefanya kitu kama hicho tungewasifu sana na hata tungechangia. Wanachokifanya sasa hivi hakileti picha nzuri.
 
Niliangalia siku moja hicho kipindi kweli nilikipenda ila hiki cha Clouds aisee wajipange upya, kipindi chao kinadhalilisha sana hawa wamama na bibi zetu
 
Back
Top Bottom