CIA walimuua Bob Marley?

Bob nyimbo zake nyingi ni haki kwa wote na ni muimbaji aliekubalika kwa watu wapenda haki.

Wimbo wa Bob- Zimbabwe ni marufuku kwa Mugabe na Iron Lion Zion huwezi kuusikia nchi za kiarabu lakini album zote zipo mpaka picha zake unaziona kwenye maduka mengi tu na sio marufuku, wanaopinga hawajui maana na maudhui yake alipokuwa anafikisha ujumbe
 
Asante mkuu umetoa maelezoo mazuri yaliyinyooka..nikitaka kupitia hiyoo short history ya Walter Rodney ntaipata kweny kitabu kipi kwa mfano mkuu..??
 
Mh sawa bwana,nasisi tis wako vizuri,ila kuna mwenye hadith ya jinsi hugo chaves alivyo tegewa mpaka ku uawa na hao jamaa??
Hugo Chaves Alibana Sana Venezuela Kiasi Cha Mataifa Makubwa Kushindwa Kuiba Nchini Kwake.
Alikuwa Anapenda Sana Wananchi Wa Chini Na Aliisaidia Sana Venezuela Kupiga Hatua.
 
Yan mie huwa nasema hivi km hujui kitu nyamaza kimya tu!...maana hakuna unachoelewa mkuu!.sikiliza nyimbo zote za bob marley kwa umakini,km huelewi bora uulize!..hyo nyimbo aliyoimba kuhusu shetan ni ipii? aiseee acha hizo mkuu km hujui bora usichangie tu! maana hakuna kitu
 
Napata ugumu wa kuelewa maana ya michango yako kabisa!...eti nyimbo zinasifu shetani hyo kitu haipo mkuu ndo maana soma vitabu vinavyomuelezea bob marley ...listen to roots reggae utapata ukweli!...nyimbo nyingi za ukombozi huimbwa kwa hisia kali kumaanisha kinachoimbwa!...acha kuandika usichojua! sasa hivi wakongwe wa reggae wanatembea na maiki zao kabisaa hawataki kufa kifo km cha Culture na wengineo!...
 
Wakati mwingine, vitu vingine ni vigumu kumeza, japo ndo ukweli wenyewe.vitu vingi tunavyoviona na kuviamini viko kinyume na sio wote wanaoweza kutambua hilo, kwa hiyo si shangai sana.
 
Mkuu hapo mwisho umeniacha kidogo. Huyo Culture uliyemtaja ni solo artist au? Unaweza kutaja moja ya nyimbo zake? Kama ni Culture kama kundi la muziki wa reggae basi hilo bado halijafa.
 
Mkuu hapo mwisho umeniacha kidogo. Huyo Culture uliyemtaja ni solo artist au? Unaweza kutaja moja ya nyimbo zake? Kama ni Culture kama kundi la muziki wa reggae basi hilo bado halijafa.
mkuu huyu Culture ni solo artist ambaye alifia stejini nchini ujerumani na hao hao jamaa walihusika ktk kifo chake! ananyimbo nyingi sana baadhi ni Jah alone a christian,money girl,one stone,pay day.
 
mkuu huyu Culture ni solo artist ambaye alifia stejini nchini ujerumani na hao hao jamaa walihusika ktk kifo chake! ananyimbo nyingi sana baadhi ni Jah alone a christian,money girl,one stone,pay day.
Baada ya kupata maelezo hayo sasa nimekupata mkuu. Ila ni hivi huyo aliyefia nchini Ujerumani ni Joseph Hill ambaye alikuwa ni mwimbaji kiongozi katika kundi liitwalo Culture. Na nyimbo ulizotaja ni za Culture kama kundi.

Pengine kutokana na Joseph Hill kuimba nyimbo nyingi katika kundi hilo ndiyo kukafanya watu kudhani kwamba jina Culture ni la mtu mmoja kama solo artist wakati sivyo. Hivyo kundi la Culture bado lipo na mmoja wa wanamuziki walio katika kundi hilo hadi sasa ni mtoto wa marehemu Joseph Hill aitwae Kenyatta Hill.
 

Kifo cha Bruce kilichangiwa na mambo mengi yote hayakuwa na uhusiano wowote na masuala ya CIA, kitu cha kwanza ni utumiaji wake mkubwa wa cannabis aliwahi kuonywa na Daktari wake alipo patwa na ugonjwa wa kifafa ghafla akiwa kwenye studio yake aki-dub film, alikaa hosptalini kwa muda baadae akaruhusiwa na kupewa mashariti ya kumeza dawa kila siku ili kudhibiti kifafa kisijitokeze tena, akaonywa kwa mara nyingine kwamba asiwe anatumia/vitu bhangi na dawa za kulevya haionyeshi kama alizingatia mashariti ya madaktari wake!!

Kitu kingine Bruce alikuwa anafanya mazoezi ya viuongo ambayo mengine yalikuwa hatarishi mfano: kutumia umeme kustimulate misuli, wakati fulani aliwahi kuhumiza mgongo wake akiwa mazoezini nadhani alikuwa yuko kwenye zoezi la kunyanyua vyuma kama nakumbuka vizuri, injuries alizo sustain madaktari wake walifikiri hataweza tena kusimama vizuri au kwendelea na michezo/mashindano ya Kung-Fung lakini wapi bwana Bruce bounced back, lakini akawa anaendelea kutumia dawa za kupunguza maumivu ya mgongo - tukiweka maanani idadi ya madawa aliyokuwa anameza kila siku - namely: Dawa za kudhiti kifafa, dawa za kupunguza maumivu ya mgongo na uvutaji/ulaji wa aina fulani ya bhangi yote hayo anayameza kila siku - mtu ungetegemea long term abuse ya nadawa hayo yangeleta nadhala gani eventually.

Kitu kingine Bruce alikuwa anapenda wanawake sana, kifo chake kilitokea akiwa nyumba ndogo, sasa tabia hii ni rahisi sana washindani wako kibiashala kuwatumia wanawake kukudhulu, Bruce alijua kwamba Studio yake na Raymond iliyokuwa inajulikana kama Golden Harvest ilikuwa na ushindani mkubwa na Studio za manyangumi wa Hong Hong wa familia ya Run Run Shaw (sijui kama jina nimepepatia) familia hiyo ilikuwa haipendi jinsi Studio za Raymond Chow na Bruce Lee zilivyo kuwa zimekuja juu kibiashara - wote tunajua Wachina walivyo vicious, wanaweza kufanya lolote kuondoa ushindani.

Now a million dollar question - Vitu gani vilichangia kifo cha ghafla Cha Bruce Lee?

* Binafsi nafikiri sababu ya kwanza inaweza kutokana na utumiaji wake wa madawa mengi kwa wakati mmoja, actually wanasena dawa aliyo pewa (Super Asprin) na mpenzi wake kuzuia maumivu ya kichwa ndio ilichangia kufanya ubongo wake uvimbe na kumsababishia kifo.

* Sababu ya pili, mpenzi wake anaweza kuwa ametumiwa na Kampuni ya Studio za Run Run Shaw kumuua Bruce baada ya kulipwa hela ndefu - kwa nini nasema hivyo: alipo hojiwa na Polisi baada ya kifo cha ghafla cha Bruce, mwanamke huyo majibu yake yalikuwa yenye utata sana, walimuhoji kwa nini Bruce alifia nyumbani kwa binti huyo kwenye kitanda chake - akajibu kwamba Bruce alipitia nyumbani kwangu akanambia anaunwa kichwa nikampatia Super Asprin ameze baadae nikampeleka chumba changu cha kulala nikampumzisha, baada ya hapo akwenda kumwangalia hali yake inaedeleaje mpaka masaa nane yakapita - alidai baadae kabisa alikwenda chumbani kwake akajaribu kumwamusha Bruce bila mafanikio, badala ya kuwasaliana ni mke wa Bruce alawasiliana na Raymond Chow ambae alikuwa ni Business partner wa Bruce, binti huyo hakutaka mkewe wa Bruce afahanu ukweli wa kile kilicho jiri - ndio maana alikimbiza mahiti Hospitalini!! Je hili lilikuwa jambo la kawaida kweli - I don't think so?
 
Siku zake zilikuwa zimefika,hayo mambo ya kufirika ni kwa wale wanaoamini hivyo,kwa kipi CIA wamtegee Bob ,alikuwa na athari gani kwa Marekani ,sijawahikusikia kuwa virusi vya kansa vinawekwa kwenye kiatu yaani vikaishi kwenye ukavu.
 
Naomba niulize hivi mbona wanaharakati wengi wa magharibi huwa ni waislam na hata kama walikua wakristo then huwa wana change kuwa waislam
 
Bwana @Bukyanagand kama story uliyoeleza ni sahihi, hata huyo mwanamke alikua sahihi. Kwa hali ya kawaida akijifaham kuwa yeye anaiba penzi la mtu asingeweza kumtaarifu mwenye mali kuwa mumewe kafia kwake. Ni bora alivyojisalimisha police.
 
Siku zake zilikuwa zimefika,hayo mambo ya kufirika ni kwa wale wanaoamini hivyo,kwa kipi CIA wamtegee Bob ,alikuwa na athari gani kwa Marekani ,sijawahikusikia kuwa virusi vya kansa vinawekwa kwenye kiatu yaani vikaishi kwenye ukavu.
.....hujawahi? Ndo usikie sasa
 
Walimuua ili iweje kuna nn aliwauzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…