Chuo Chetu Kimeanza Kufundisha Kiswahili

Chuo Chetu Kimeanza Kufundisha Kiswahili

Natamani sana kujifunza kikamilifu kichina. Nawezaje kupata scholarship mkuu? Njia rahisi kabisa ya kufanikisha hilo.
Kichina ni rahisi sana mkuu. Kama ukitaka kujifunza basi njoo hapa China na serikali itakupa scolarship
 
Kichina ni rahisi sana mkuu. Kama ukitaka kujifunza basi njoo hapa China na serikali itakupa scolarship
Inabidi kupata kwanza scholarship ndo uweze kuenda China,maana shule ndo inakupatia viza.
 
Mpumbavu ni yule anae shobokea comment isiyo muhusu.. Anzisha thread yako unijibu... Mind your own business bi*ch
Kwa maana hiyo wewe ndiyo umeanzisha hii thread ndiyo maanda unaandika utakavyo? You're a devil[emoji48] indeed!

Jifunze kuelewa wenzio siyo kuropoka hovyo Kama uko kwenye sungusungu
 
kwahiyo we mchina unataka kutufundisha misamiati sisi wamiliki wa hii lugha? jiangalie ohoooooo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwam ameanza madoido kuthibitishia kuwa keshaota mapembe ( kaitawala lugha)!
 
Bakari nina swali. Hivi ni nyoka yupi anaefaa kuliwa? Wale wenye sumu mnaitoa vipi sumu yao?
 
na ng'e na chura. JE wachina wote wanakula hao wanyama?
Bakari nina swali. Hivi ni nyoka yupi anaefaa kuliwa? Wale wenye sumu mnaitoa vipi sumu yao?
Alaa...hawali nyoka wenye sumu......
kwa kawaida sisi hula kuku, ng'ombe, kondoo, mbuzi, bata, samaki, ng*****(samahani ikiwa wewe ni mwislim) n.k Pia nilisikia kuwa wachache wanakula panya, tandu, nge, nyoka,paka......
 
Alaa...hawali nyoka wenye sumu......
kwa kawaida sisi hula kuku, ng'ombe, kondoo, mbuzi, bata, samaki, ng*****(samahani ikiwa wewe ni mwislim) n.k Pia nilisikia kuwa wachache wanakula panya, tandu, nge, nyoka,paka......
Muislamu [emoji106][emoji106][emoji106]

Mwislim [emoji107][emoji107][emoji107]
 
Sasa mimi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Lugha na Taaluma za Kimataifa cha Shanghai(yaani Chuo Kikuu cha Shanghai International Studies University). Mwaka jana chuo chetu kimeanza kusomesha lugha hii, mimi ni mmojawapo kati ya wanafunzi wa mwanzoni. Tuna walimu watatu, wawili ni Wachina na mwingine Mwl. Bosire anatoka Kenya na anakuja kutufundisha lugha hii.
Nimechagua chuo hiki kwa sababu ninapenda lugha(nilipokuwa sekondarini nilipenda sanasana Kiingereza). Wakati nilipoingia chuoni, Kiswahili ni lugha mpya kwangu, lakini sasa naona Kiswahili ni rahisi sana.
Mwaka kesho nitakwenda UDSM kwa muda mrefu. Natumai kupata maendeleo makubwa huko.
Kabla ya kujifunza Kiswahili sikuelewa Tanzania hata Afrika ya Mashariki, lakini sasa hivi ninaelewa historia na jiografia ya Afrika ya Mashariki. Pia ningependa kufanya urafiki na watu wa Tanzania. Baaya ya kuhitimu nitafanya kazi nchini Tanzania kwa ajili ya kujenga urafiki wa China na Tanzania.
Vyuo vinne vinasomesha lugha hii, yaani: Chuo Kikuu cha Idhaa na Lugha ,Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing, Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Tianjin, Chuo Kikuu cha Lugha na Taaluma za Kimataifa cha Shanghai. Vyuo vingine vya lugha vitaanza kufundisha lugha hii miaka ijayo baadaye. “Kiswahili duniani” ni kweli kabisa.
Asante sana
Hivi inakuwaje mkenya anafundisha kiswahili na ukirejea kenya kwa asilimia kubwa wanazungumza English na hata kiswahili chao ni broken sana na sio fasaha.

Mnaachaje kuchukua walimu kutoka Tanzania ambao wengi wao ni fluent swahili speakers na hii kwao ni official language plus Tanzanians ni 100% majority swahili speakers......?!

Hebu niambie we bakari mchina..... Kwanini hampo makini katika kutafuta walimu wa kiswahili?!
 
Katika kipindi chetu cha kwanza mwalimu wetu Dada Upendo(Mchina) alichagua majina yetu ya Kiswahili. Alifikiri kuwa kutuita majina ya Kiswahili ni bora zaidi kuliko kutuita majina ya Kichina.
Sasa huyo mwalimu kakosea majina ya kiswahili inabidi upate yale ya kijijini. Sasa ukiitwa bakari utaonekana ustadhi au ukiitwa Frank utaonekana mfarisayo. Ila nadhani ungeuliza majina ya kiswahili yenye ubantu ndani yake kama, Tumwine, Boke, Lung'wecha, Nyangero, Lukuvi, Chibulunje, kikwete, Kachweka, Kapanga, Mwanjali, Mwakabonga....
 
najifunza Kiswahili kwa kusudi la kukuza urafiki kati ya Tanzania na China wala si kukuibia[emoji35]sisi Wachina tunapenda amani na urafiki. Watu wa Tanzania ni marafiki zetu wakubwa sana
Mbona mnakuja wanaume tu, me natarajia mngetanguliza wanawake hao ndio tungejenga nao urafiki kwanza maana nyie wanaume sasa huo urafiki daaaaah mbon ni nyie tu mtakuwa mnakula dada zetu....
 
Back
Top Bottom