Chuo cha Uhasibu Arusha chadaiwa kudahili Wanafunzi wengi kuliko uwezo wake, wengine wasomea na kuishi Hoteli ya Ngurdoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
1.jpg

Chuo cha Uhasibu Arusha – Institute of Accountancy Arusha (IAA) kimedaiwa kufanya udahili kwa idadi kubwa ya wananafunzi kuzidi uwezo wake, jambo linalosababisha uongozi wa chuo kuhamishia wanafunzi wa baadhi ya kozi katika hoteli ya Ngurdoto.

Baadhi ya Wanafunzi hao ambao wamepelekwa Ngurdoto kusoma na kuishi ni kutoka katika kozi za:
•Bachelor in Business Management (BBM)
•Basic Technician Certificate in Business Management (BTCBM)
•Ordinary Diploma in Business Management (ODBM) mwaka wa 1
•Bachelor of Accountancy (BA) mwaka wa 1 & 2
•Basic Technician Certificate In Accountancy (BTCA)
•Ordinary Diploma In Accountancy (ODA) mwaka wa 1 & 2

Baadhi ya Wanafunzi wamelalamikia suala la kupelekwa Hotelini kwani awali waliomba kusomea Main Campus ambapo walishakodi vyumba karibu na chuo na kununua mahitaji ya kujikimu kama vile magodoro, majiko nk.

Wamesema sasa wanalazimika kulipa kiasi cha Tsh. 400,000 kama malipo ya Hosteli (huko hotelini).

“Kama chuo kimejaa kwanini wanachukua idadi ambayo wao hawawezi kumudu na kuanza kutusumbua wakati tumeomba main campus?” amehoji mwanafunzi mmoja.

Wanafunzi wameomba kama Idadi imezidi ni bora baadhi ya Wanafunzi wahamishiwe Vyuo vingine.
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati, kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha, imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi! Kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
Wanakodishwa kwa kiasi gani? Je, mkataba wao unasemaje?
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania .
Tunajenga miundombinu kwanza ya taifa ikifeli imefeli kivyake tu
 
THIS is purely mismanagement, The gvt has nothing to do with the failures and never ending internal conflicts within the family of the late Mrema.

Ni kweli serikali hii ina makosa katika baadhi ya mambo ila tusiisingizie uongo kila mara kama huu wa kusema ooh serikali uchumi wa Kati.

Lawama zote kwa Mrema mwenyewe alishindwa kuweka mifumo ya kuendesha mali hizi sasa kila mtu ni kambale nani ataenda kulala sehemu yenye migogoro?

FAMILIA ya Mrema ilaumiwe kwa kushindwa Kusimamia mali nyingi kiasi kile wanaanza kuumana kila uchao.
 
THIS is purely mismanagement, The gvt has nothing to do with the failures and never ending internal conflicts within the family of the late Mrema.

Lawama zote kwa Mrema mwenyewe alishindwa kuweka mifumo ya kuendesha mali hizi sasa kila mtu ni kambale nani ataenda kulala sehemu yenye migogoro??
Blame shift lawama ni kwa serikali.
 
Hii ndio taarifa ya sasa na ya kushangaza inayozunguka Tanzania mpya yenye uchumi wa kati , kwamba Hotel ya nyota 5 iliyo kwenye kitovu cha utalii Arusha , imefikia makubaliano na uongozi wa chuo cha Uhasibu ili kufanywa malazi ya wanafunzi ! kiukweli hili jambo linafikirisha haswa .

Nakulilia Tanzania.
Duh! Mkuu Erythrocyte , asante kwa taarifa hii⁩, kwanza naomba ku declare interest, mimi ni mdau wa hotel za Mzee huyu. Kampuni yangu ya PPR, ndio ilikuwa ikiwatengenezea matangazo ya biashara, na kila mikutano mikubwa tukiitwa kuitangaza, na ni Mkutano fulani uliofanyikia Ngurdoto, ukanifanya waandishi wa Arusha niwavulie kofia, kwa kuwaheshimu kwa umoja!.

Comming back to Hotels, my favourite ni Impala na ndio makao makuu. The boss mchana kutwa anashinda kwenye usimamizi, anaingia kazini saa 5 usiku, hadi saa 12:00 asubuhi, daily, hakuna kulala na hakuna Jumamosi, Jumapili wala Sikukuu.

Kutokana na ratiba hii, sijui chakula cha nyumbani alikuwa anakula saa ngapi, lakini kwa wahudumu wa hotel na walivyo warembo, ilikuwa ni kazi na dawa!.

Kupitia ukaribu huo, kwanza ndio nikajua kumbe ni huyu jamaa huwa anaamua Mbunge wa Arusha awe nani, ni yeye aliyekuwa akimfund Lema japo ni mwana CCM, kama yule tajiri wa Dar alivyokuwa aki i fund Chadema japo yeye ni CCM, na angekuwa hai, CCM ingepigwa mweleka Arusha.

Kwa sisi wanye economic eye, the money ilitumika as capital kujenga hiyo business empire yake, sio income from the hotels only, alikuwa na side business ya big bucks changing hands usiku kucha. Kwa vile na mimi nafanya editing usiku kucha, ndio unaona people's movements with trunks full of $. This side business ndio inaingiza good money, mke, watoto hawajui na hawawezi na wazee wengine kwa sababu walikuwa wanajua the risks associated, hivyo they opted to keep the family away.

Alipoitwa kwenye makao yake ya milele, no one else knew how to go about. Na japo jamaa alikuwa ni Mchaga, lakini alikuwa na genes za Kisukuma za kupenda vi spring chickens vyeupe, na kupenda watoto, hivyo he had many with warembo na kuna mahali, alma nusra ningemvunjia heshima, ila after learning ni pumziko la Boss, I just said no, kwa heshima tuu, hata kama Boss hata jua!, the lady insisted nisiogope, kwasababu the boss picks every good tasty meals!. Hizo ni tabia za Kisukuma za wanawake wengi, watoto wengi na openly!.

Uzuri wa huyu Mzee, akikukubali, any price you tell anakulipa bila kusema punguza kidogo!. Mimi na team yangu ni kula bure, kulala bure!. He was more than boss, na baada ya kujikuta tunafanana tabia, tukatokea kuwa marafiki, jamaa anaongea na presidents!. Hizo connections ndizo zilikuwa zinafanya hotel zijae. Ameondoka na connections zake!.
RIP Don Mrema!.

P
 
Back
Top Bottom