Gemu mpaka dakika hii haijanivutia kabisa. Dk ya 38 bila bila. Namuana Baba Vieira naye yupo, pembeni yupo na 'kakitu kake' duh..walah pesa inavuta vitu vizuri wajameni.
Acha Ukware mazee....umetoa mimacho kwa kakitu ka mwenzio?
Carra anapata taabu sana kwa Drogba!
Ku-acknowledge uumbaji wa Mola wetu tangu lini ni ukware? Au ukware siku hizi umebadilishwa maana?
Ukikutana na kakitu kama hako mitaa ya kati lazima uteme neno!
Hapana kiongozi, nitafumba macho kuomba dua ya shukran kwa uumbaji maridhawa.
BTW, game vipi naona imedoda ni vurugumechi tu hamna ufundi wowote. Dalili ya goli siioni.
Kipindi cha kwanza sijakiona lakini natarajia vijana wa KOP watazinduka dk hizi 45 za mwisho
Hahahahahh
Mechi hii iko very tactical ukiweka ulufundi mnaweza jikuta mnaenda kuanza kati chuma ndani!
Tatizo linachangiwa kwa kiasi kikubwa na uoga wa Benitez wa kuchezesha straika mmoja. Chelsea naona ndio likely kufunga ktk mechi hii kuliko KOP.