Mashabiki wengi wa Chelsea na football kwa ujumla Wana mu underrate sana Pedro Neto tuna wasifia wachezaji wengine kama Palmer, Caicedo n.k tunamuacha huyu jamaa lakini asikuambie mtu moja kati ya wachezaji muhimu ni huyu jamaa ndio maana makocha wengi huwa wanampenda baada ya ujio wa Estevao wengi waliona atapigwa benchi dhidi ya huyu lakini haikuwa hivyo.
Pedro Neto anapendwa na makocha wengi kwasababu Pedro Neto ana workrate kubwa uwanjani kuliko mawinga wengi mafundi, ana kasi alafu ni mzuri sana kwenye kufanya majukumu ya ukabaji. Kwa aina ya mfumo wa Alonso wa mabeki watatu nawaambia ukweli Pedro Neto atakuwa first choice ya Winger ,wa pili atakuwa Quenda na mwisho ni Estevao yeye ndio anakizi nafasi ya Wing back na Quenda kwa Estevao hafit ila kama mfumo utakuwa wa mabeki wanne.