Huu ni uuzwaji wa lazima lakini ni mchungu
Ni wa lazima kwa sababu Chelsea lazima iuze wachezaji wenye bei sokoni ili isikumbwe na shoka la FFP na pia iweze kufuata masharti ya UEFA kwenye A-list waliyopewa tangu msimu uliopita kwa miaka minne. mMasharti ya UEFA inasema ili Chelsea isajili wachezaji wa A-list ni lazima iuze wachezaji.
Ni lazima pia kwa sababu Chelsea msimu ujao haina mechi nyingi za kucheza. Kama Santos alifanikiwa kucheza mechi 13 tu msimu uliopita je msimu ujao bila UEFA anaweza asicheze kabis ana ndio maana mchezaji mwenye alilazimisha kuuzwa.
Sio nzuri na ni uuzwaji mchungu kwa sababu Santo ni kiungo bora sana aina ya Casemiro. Ni mzuri kwa ukabaji, anasoma mchezo vizuri na anaweza pia kufanya mashambulizi. Ni mzuri sana kwenye mfumo uliopangika kama wa Xabi Alonso ila sasa Alonso inaelekea atawatumia zaidi Caicedo na Enzo Fernandez kuliko Santos.
Kumbuka pia tuna Valentin Barco na Reece James anaweza pia kutumika sana kwenye DM ili kumpunguzia mzigo wa majeruhi na kwa ujio wa Marco Palestra na Giovani Quenda na uwepo wa Malo Gusto unaweza kuwa ni mkakati wa kutompa majukumu mengi James kwenye RWB ambayo Alonso anaweza kuutumia sana
Kwa hiyo ni halali kusema kuwa Chelsea ina viungo wafuatao hata asiponunuliwa mwingine
- Moises Caicedo
- Enzo Fernadez
- Valentin Barco
- Dario Esugo
- Reece James
RB/RWB
- Reece James
- Marco Palestra
- Giovani Quenda
- Malo Gusto
- Josh Asheampong