TANGAZO RASMI LA KLABU YA CHELSEA KUHUSU ENZO MARESCA
“Klabu ya Chelsea inatambua kwamba msimu wa 2025/26 ulikuwa wa huzuni kubwa mno kwa Klabu na wapenzi wake wote. Sababu kuu ilikuwa machafuko makubwa yaliyotokana na mabadiliko ambayo Klabu ililazimika kufanya katika nafasi ya Head Coach wakati wa Krismasi.”
“Kutokana na mambo mapya yaliyojitokeza, tunaona ni muhimu kuwafafanulia wapenzi wetu yaliyotokea na kwa nini former Head Coach wetu aliondoka Klabuni tarehe 1 Januari 2026.”
“Mwaka jana katika vuli, Klabu iliarifiwa na former Head Coach wetu kwamba kunaweza kuwa na opportunity kwake kurithi nafasi ya Pep Guardiola mwishoni mwa season.”
“Ilikuwa wazi kwetu kwamba moyo wake ulikuwa umeegemea sana kutaka succeed Guardiola, na alikuwa amejitolea kabisa kufuata hiyo opportunity, ijapokuwa alikuwa chini ya mkataba wa muda mrefu ambao hakuwa na haki ya kuivunja.”
“Mwishoni mwa mwezi wa Desemba 2025, kocha mkuu wetu alijiuzulu ghafla na bila kutarajiwa. Tulihisi kuachwa, kwani ilikuwa dhahiri kuwa moyo na akili yake vilikuwa vimeelekea klabu nyingine na fursa nyingine, licha ya kuwa alikuwa amefika Chelsea mwaka mmoja tu uliopita.”
“Hakuna klabu inayotaka kubadilisha Head Coach wake katikati ya msimu. Hata hivyo, kwa kuzingatia uamuzi wake wa kutotimiza majukumu yake hadi mwisho wa msimu, Klabu haikuwa na njia nyingine ila kulinda wachezaji wetu, wapenzi wetu, na Beji yetu, na kukubali resignation yake.”
“Katika hali hii na kwa heshima ya pande zote kati ya maklabu, confidential settlement imefikiwa na Manchester City, ambayo inajumuisha payment ya compensation. Confidential settlement pia imefikiwa na kocha wa zamani, ambapo yeye atalipa compensation.”