Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Enzo Fernández akachukua usukani, akamchezesha Malo Gusto kwa ustadi, Gusto akamtengenezea João Pedro mpira wa kumalizia kwa tapping maridadi. Na kweli, yule Enzo wa enzi za Pochettino ameonekana kurudi uwanjani—mwenye ubunifu, utulivu na ushawishi mkubwa kwenye mchezo.

Aston Villa 1 -1 Chelsea

 
João Pedro alimchezesha Cole Palmer, akampasia Reece James pembeni naye James akamimina krosi ambayo kipa Martinez hakuweza kuimudu akapangua na mpira kumfikia Palmer ambaye hakufanya ajizi bali akamalizia kwa bao maridadi kabisa.

Aston Villa 1 -3 Chelsea

 
Cole Palmer alimpasia pasi murua Alejandro Garnacho, ambaye alimfungulia João Pedro, na Pedro akakamilisha hat-trick yake ya kwanza na Chelsea kwa ustadi mkubwa.

Aston Villa 1 -4 Chelsea

 
Alejandro Garnacho alipenyeza mpira kwa Enzo Fernández, ambaye alimsogezea João Pedro kwa ujanja mwingi, na Pedro akamalizia kwa bao lake la pili—moja ya mabao bora ya timu kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.
Aston Villa 1 -2 Chelsea

 
João Pedro chini ya Liam Rosenior:

→ Mechi 12
→ Magoli 10
→ Asisti 4
1772789449760.png
 
Niliwahi kusema sehemu fulani kwamba Chelsea wana wachezaji wazuri sana.
Kwa mfano hawa wachezaji walisemwa sana kuwa ni wabovu ila mimi nasema:
  • Garnacho ni mzuri
  • Gittens ni mzuri
  • Hato ni mzuri
Tatizo si ubora wa wachezaji mmoja mmoja. Kilichowafanya washindwe “kukiwashe” ni ubovu wa timu katika idara nyingi—hawachezi kama timu.

Mfano mzuri kabisa ni Strasbourg. Ukiwaangalia, utaelewa ninachomaanisha:

1) Wanacheza kama timu

Hakuna uchoyo, wanapeana pasi, wanafuatilia pasi, na hakuna mchezaji anayebaki isolated. Mfumo wao unamfanya karibu kila mchezaji aonekane mzuri. Ndio maana karibu kila mchezaji akien da pale anaonekan ni mzuri.

2) Wanachukua risk kwa kupigiana pasi kila sehemu ya uwanja

Wanacheza:
  • back passes
  • sideways passes
  • vertical passes
  • long balls
  • transitions
  • short passes
Ni fursa ya kwenye mchezo wakati huo ndio inaamua aina ya gani ya pasi, si woga. Huu ni uchezaji wenye ujasiri na maamuzi ya haraka.

3) Work rate iko juu
Kila mchezaji anafanya kazi. Hakuna aliyesimama kama mlingoti. Movement ipo, presha ipo, na intensity iko juu.

Sasa turudi Chelsea

Ukiweka pembeni mechi ya jana dhidi ya Aston Villa, Chelsea wana talanta kubwa kuliko Strasbourg, tena kwa mbali. Lakini hawana zile sifa tatu muhimu:
  • Hawajitumi vya kutosha
  • Wachezaji wa mbele wanabaki isolated
  • Hawatake risk
  • Wanacheza back na sideways passes nyingi
  • Movement ni ndogo, hakuna kukimbia kwenye nafasi
Matokeo yake, hata mchezaji mzuri akipata mpira, anaonekana dhaifu kwa sababu hana support wala structure. mchezaji akipewea mpira akawa kwenye presure hakuna msaada, ufuatiliaji ili aweze kuupasi huo mpira bila ya kuupoteza.

Lakini jana dhidi ya Aston Villa…

Idara zote zilifanya kazi.
Nimeona:
  • uchezaji kama timu
  • risk-taking, pasi za hatari zilichezwa kila sehemu ya uwanja
  • movement nzuri has aya viungo an washambuliaji
  • intensity na presisng nzuri
  • na coordination ambayo imewafanya wa-outperform Aston Villa kabisa.
Na ukitaka uthibitisho, angalia tu takwimu za Garnacho:

Garnacho vs Aston Villa
  • 100% passes completed (27/27)
  • 12 touches in the opposition box
  • 7 duels won
  • 6 chances created
  • 4 tackles
  • 3 shots
  • 3 fouls won
  • 1 assist
 
Chelsea wamegundua namna mpya ya kuwashinda opponent zao kisaikolojia na kiakili, angalia hii hapa

 
FA Cup 5th round
Wrexham vs Chelsea

3-4-2-1

--Delap--

Garnacho ------ Neto

Hato--Santos --- Lavia — Acheampong

— Sarr--Badiashile — Tosin

--Sanchez--

Bench
  • Sharman-lowe
  • James
  • Gusto
  • Cucurella
  • Esugo
  • Lavia
  • Derry
  • Joao Pedro
  • Guiu

#CFC | #WRECHE
 
Badiashile ana pass moja tu kila akipewa mpira yeye ni kurudisha kwa kipa, hata kama yupo katikati ya uwanja. mamaee chezaji kama hili lanini?
 
FA Cup 5th round
Wrexham vs Chelsea

3-4-2-1

--Delap--

Garnacho ------ Neto

Hato--Santos --- Lavia — Acheampong

— Sarr--Badiashile — Tosin

--Sanchez--

Bench
  • Sharman-lowe
  • James
  • Gusto
  • Cucurella
  • Esugo
  • Lavia
  • Derry
  • Joao Pedro
  • Guiu

#CFC | #WRECHE
Chelsea imewaanzisha wachezaji wawili tu wa kwenye XI ambao ni Neto na Sanchez (Ambaye sasa sio starter tena wa Chelsea)
Sub iliyofanyika ni wachezaji watatu tu ndio wanaoanza kwenye timu kuu ambao ni Gusto, Joao Pedro na Cucurella aliyetokea majeruhi
 
Tutawezaje kuwafunga kwa mchezo mchafu kama huu. Unamkamata mchezaji ili asiruke, asimove. Ni mchezo wa mieleka peke yake ndio inachezwa bila kuruka wala kusogea.Davids Raya kaonekana shujaa wa Arszenal kwa sababu mabeki wao wako busy kuwakamata wachezaji wa Chelsea walio kuwa kwenye mkao wa kuruka na kufunga magoli. Nadhani hii ni tactoics aliyowapa wachezaji huyo kocha mchafu Arteta kwa sababu ni kila mchezaji wa Chelsea kamata kamata na refa naye legend wa Arsenal
View attachment 3552161
Cry more bro😅
 
Wee Mmarekani na Muisrael wakikusikia unawataja hao Late Ayatollah Khamenei na Osama watakujumuisha kwenye Vita Yao!!💀💀🤪🤣
 
Kwa wale mnaoangalia mpira kwa kutumia PC au browser please tumia hii link, wanaonyesha full HD very clear bure. Ukipenda kuwachnagia ila sio lazima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom