Si bado mechi moja anafikisha mechi nane
Rosenior bado anapata matokeo, lakini kiwango cha uchezaji hakiridhishi. Nilisema huko nyuma na narudia tena.
Huenda wachezaji bado hawajamuelewa kikamilifu.
Huenda pia safu ya ulinzi inamuangusha.
Huenda pia kushuka kwa ubora wa Caicedo, Palmer, James kunamuathiri sana — hawa wachezaji hawako kwenye viwango vyao. Hata Pedro Neto hayupo kwenye ubora wake tena. Hata Cucurella kabla ya mechi ya jana alikuwa hachezi vizuri ila jana alipotokea benchi ndipo aliingia na moto.
Hata wachezaji wachanga kama Garnacho, Gittens, Delap na Hato waliokuwa wanaonyesha kuimarika kipindi cha Enzo maresca, sasa wamepotea. Ni kama wamerudi mwanzo kabisa.
Nampenda Liam Rosenior kama kocha — ni mtu positive, anaongea sana na wachezaji — lakini nimeona udhaifu ambao ukiachwa ukae muda mrefu unaweza kumzuia kufika kiwango cha juu zaidi.
1) Anawaaonea huruma sana wachezaji.
Huwezi kuwaonea huruma wachezaji wasiojituma na kucheza vizuri mara kwa mara kama Disasi, Badiashile na wengineo. Mchezaji akishindwa kucheza vizuri, tupa nje atakuja kukufuzisha kibarua.
2) Hana ile nguvu ya ku-command kama alivyokuwa nayo Enzo Maresca.
Hiyo authority ndiyo iliyomsaidia Maresca kuwafanya hawa vijana wafuate maelekezo yake na kucheza vizuri na kutwaa makombe mawili ya haraka haraka. Rosenior anatakiwa kuweka msimamo: wachezaji wajue anataka nini, na wasipofuata maelekezo, wapigwe benchi hata kama ni wachezaji muhimu.
3) Anakuwa mkarimu kupita kiasi kwenye muda wa kucheza.
Anafanya rotation kubwa kupita kiasi na kuwapa dakika wachezaji ambao hawajastahili. Gittens, Garnacho, Delap na wengine hawapaswi kuanza mechi labda zile za umuhimu mdogo au kucheza dakika 45 hadi wakomae kiakili na kujua kufanya maamuzi sahihi ya kiume wanapokuwa uwanjani.