Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Mbaga Jr 😂😂
Leo wamekuponda na nyundo
IMG_4854.jpeg
 
Emanuel Emegha ni mnyama wa nguvu—ana misuli, kasi, na uwezo wa kujipanga kwenye nafasi hatari za kufunga. Akipata nafasi safi, anafunga bila kusita. Hapa ndipo anapomzidi Nicolas Jackson: ni mfungaji wa uhakika, hana haja ya nafasi nyingi kufunga bao moja.

Lakini udhaifu wake mdogo ni ubinafsi. Si kwamba hii ni mbaya sana kwa sababu striker wengi wakubwa ni wachoyo, ila anacheza kwa mtazamo wa “mimi kwanza.” Haunganishi na viungo, haangalii wachezaji walioko kwenye nafasi bora, na mara nyingi huchagua kupiga badala ya kupasa. Anaonekana kama anacheza peke yake.

Jackson, kwa upande mwingine, ni mshambuliaji wa timu. Anashuka kusaidia, anapasi vizuri, anashirikiana na wenzake, na anajua kuunda nafasi kwa wengine. Ingawa hana ukali wa Emegha katika kumalizia, mchango wake kwa timu ni mkubwa zaidi. Ana akili ya mpira, anajua kusoma mchezo, na anafanya timu icheze vizuri.

Chelsea tayari wameamua—Jackson atauzwa mwaka 2026, hata kama Bayern hawatamsajili. Lakini kwa timu inayotaka mshambuliaji anayejenga ushirikiano, anayesoma mchezo, na anayefanya wengine kung’ara, Jackson ni bora zaidi. Emegha anaweza kufunga zaidi, lakini Jackson anafanya timu kuwa bora.
1758154916611.png
 
Huyu Mgosi ashauza mechi mpuuzi huyu, Gusto wa nini?!!
Mna beki line mbovu kuliko kitu chchte kile....yule Chalobah na Tosin ni wafanyakazi hewa wale...nyny kila siku mnasajili mawinga....ila mabeki hamshuhuliki kabisa....mtadundwa sana msimu huu
 
Lakini pia kumbuka katoa assist ya Cole Palmer sisi mchezaji anayetuangusha ni huyo Enzo Fernandez huyu ameshakuwa mzigo kwenye team
Nawakumbusha tu majirani mpo nafasi ya 32 mpk sasa kwny msimamo....mdogomdogo mtafika tu msijali
 
huwa nawambia hapa kila siku kwamba huyo jamaa ni takataka lakini mnakaza fuvu. Sasa naona mnaanza kuelewa
Lakini pia kumbuka katoa assist ya Cole Palmer sisi mchezaji anayetuangusha ni huyo Enzo Fernandez huyu ameshakuwa mzigo kwenye team
 
Leo ngoja niwambie ukweli mchungu.

Kila alie shabiki na mpenzi wa Chelsea FC asome hili andiko. Klabu yetu ya Chelsea ni ya kawaida sana wala msijidanganye kuwa tuna ukali wowote ule. Ata ile FIFA Club World Cup tulibahatisha tu.

Klabu yetu haina uwezo wa kupamba na klabu kama Liverpool, Arsenal, Bayern Munich, Real Madrid, Barcelona, PSG, Inter Milan, Man City, Napoli na nyingine kwenye mashindano yoyote yale, tutaishia kushiriki tu. Kwa sasa level zenu ni Conference League huko, bado hatujawa na uwezo wa kuleta upinzani kwenye UEFA na UEFA Europa League. Huo ndio ukweli ukubali ama ukatae huo ndio uhalisia.

Huwezi kwenda kwenye mashindano makubwa kama UEFA wakati huo huo una lundo la wachezaji ambao ni matakataka tu. Wenzako wana silaha kweli kweli mfano, Harry Kane, Mohammed Sarah, Lamine Yamal, Mbappe Haaland na wengine wengi kuwaandikia wote sito weza. Wakati huo sisi tuna matakataka akina Enzo Maresca, Sanchez, Enzo Fernandez, Liam Delap, Jamie Gittens, Romeo Lavia, Facundo Buonanotte, Malo Gusto, Jorrel Hato na matakataka mengine.

Huwa nashangaa sana unakuta mtu hapa jukuani ana kaza mshipa kabisa eti kwa hilo lundo la matakataka kuna mahala watatufikisha, kwa kweli inasikitisha sana. Inapaswa tuelewe na tukubali wanao tuhalibia timu ni hawa wapuuzi walio uziwa hii timu. Hizi sajili za hovyo hovyo alafu wakati huo tukitaka matokeo chanja ni sawa na kuokota embe chini ya mnazi.

Klabu nyingine zinafanya sajili za maana eti sisi tunaenda kusajili watu kama Liam Delap, Jamie Gittens alafu unategemea upate matokeo chanya tunaacha wachezaji wazuri wa kutupa hiyo chanya tunakimbilia matakataka ambao ata hawajulikani walikuwa wanafanya nini hapo kabla.

Hapa hamna timu ya kuleta upinzani kwenye UEFA na EPL, level zetu saizi ni kina Sunderland, West Ham, Wolves, Leeds na wengine kama hao. Huwezi fika level za ukubwa wakati huohuo una lundo la matakataka.

Huo ndio ukweli mchungu, ukubali ama ukatae ila tambua huo ndio uhalisia wenyewe. Mtu anae fahamu na mpenzi wa mpira hawezi pingana na huu ukweli. Tizama kuanzia kikosi tulicho nacho na uchezaji tunao cheza kisha tathmini tunaweza kuwa bora mbele ya hao miamba. Sisi bado sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom