Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Mimi nina mtizamo chanya msimu ujao na Chelsea (Mabingwa wa Dunia) itakuwa timu itakayoogopwa na timu nyingi sana. Msimu uliopita hatukuwa na timu nzuri, wewe fikiria msimu mzima tuna striker anayeitwa Nicolas Jackson na winga anayeitwa Noni Madueke na winga wa kulia tulimtegema sana Sancho na George kmidogo. Winga peke aliyekuwa mzuri japo sio world class alikuwa ni Pedro Neto. Sasa tunaenda kuanza msimu na Fowards 9 na wote wakali. Niambie nani atapona na hawa washambuliaji. Hapo bado sijaweka Andrey Santos na Enzo Fernandez.
  1. Xavi Simons – Central Attacking Midfielder (CAM)
  2. Cole Palmer –Central Attacking Midfielder (CAM)/ Right Winger
  3. Jamie Gittens – Left Winger
  4. Alejandro Garnacho – Left Winger
  5. Pedro Neto – Right / Left Winger
  6. Estevão Willian – Right Winger / No. 10
  7. Liam Delap – Striker
  8. João Pedro – Striker / No. 10 / Left Winger
  9. Nicolas Jackson – Striker
 
Yani ninyi mashabiki mnataka mchezaji akipata majeraha tu auzwe?, Kwa hiyo James angeuzwa kisa majeraha,Lavia auzwe kisa majeraha,palmer akipata majeraha auzwe!!!, sa hiyo itakuwa timu au kikundi cha wahuni!!!?.

Yani timu ikuthamini ukiwa mzima tu basi sio, ni nani ambaye huwa haumwi au kupata changamoto katika kazi anayofanya awe ameajiliwa akiumwa basi aachishwe kazi au mnahisi wanajivunja ili wapumzike?, hakuna timu ya hivyo dunia isiyovumilia majeruhi ya mchezaji na haitatokea wachezaji wasipate majeruhi iwe ya mda mfupi ama mrefu,hivyo tuwe mashabiki wa kusupport pande zote mchezaji anapokuwa ndani ya uwanja na nje ya uwanja kwa sababu ambazo hajazisababisha kwa kusudio.
 
Mm nimeuliza lavia ameisaidia nn timu, watu wanaishia kusema jamaa anajua Ila majeraha ndo yanamrudisha nyuma 😂 nabaki kucheka tuu
Lavia ni injury prone that is true lakini huwa akiwa Hana majeraha huwa anaonesha kiwango kikubwa ni Kama James akirudi tu uwanjani huwa anakiwasha Kama vile hajatoka kwenye majeraha ndio maana watu hawamlalamikii kivile ila tulikuwa na wachezaji Kama Madueke na huyu mwenzake Jackson huwa hawana injury lakini viwwngo vyao uwanjani vinaongeza ugonjwa wa kisukari
 
Ebu leo tuwataje watu wakubwa na macelebrity ambao ni mahsabiki wa Chelsea

Bill Clinton
Beyonce
Taja wengine**
 
🗣️ Rúben Amorim alizungumza na BBC kuhusu hali ya Alejandro Garnacho katika Manchester United, akisema:

"Garnacho ni mvulana mwenye kipaji... lakini wakati mwingine mambo hayaendi sawa. Huwezi kueleza hasa ni nini. Ni wazi anataka jambo tofauti katika uongozi tofauti".

Kauli hii inaonyesha kuwa kuna mgawanyiko wa maono kati ya mchezaji na kocha. Garnacho ameondolewa kwenye kikosi cha ziara ya kabla ya msimu, na ripoti zinaonyesha kuwa anatafuta klabu mpya—Chelsea ikiwa miongoni mwa kloabu inayovutiwa na mchezaji huyo.

Amorim pia alisisitiza kuwa si suala la nani ni mzuri au mbaya, bali ni mchezaji kutaka changamoto mpya. Hali hii inaonyesha mabadiliko makubwa ndani ya United chini ya uongozi wake.

Kwa maelezo haya inaonyesha wazi kuwa Man United hasa kocha Amorim alikuwa anmhitaji ila Garnacho amekataa anataka kujaribu changamoto mpya.

Taarifa zingine zinadai kuwa Garnacho anatamani sana kucheza UCL kitu ambacho man United hawana wala haionyeshi wataipata miaka ya hivi karibuni

1754226572898.png
 
Yani ninyi mashabiki mnataka mchezaji akipata majeraha tu auzwe?, Kwa hiyo James angeuzwa kisa majeraha,Lavia auzwe kisa majeraha,palmer akipata majeraha auzwe!!!, sa hiyo itakuwa timu au kikundi cha wahuni!!!?.

Yani timu ikuthamini ukiwa mzima tu basi sio, ni nani ambaye huwa haumwi au kupata changamoto katika kazi anayofanya awe ameajiliwa akiumwa basi aachishwe kazi au mnahisi wanajivunja ili wapumzike?, hakuna timu ya hivyo dunia isiyovumilia majeruhi ya mchezaji na haitatokea wachezaji wasipate majeruhi iwe ya mda mfupi ama mrefu,hivyo tuwe mashabiki wa kusupport pande zote mchezaji anapokuwa ndani ya uwanja na nje ya uwanja kwa sababu ambazo hajazisababisha kwa kusudio.
Ni ww sasa umepata House girl mchapa kazi, umekaa nae mwaka mzima kila siku yeye nikuumwa, ukipiga hesabu siku alizifanya kazi ni kama mwezi mmoja miezi yote yupo kitandani, utaendelea kukaa nae? Kuumwa kupo ila kukizidi sana pia ni tatizo.
 
Vipi kuhusu wachezaji ambao hawana injury Kama Madueke na Jackson alafu na viwango wanavyoonesha uwanjani
 
Vipi kuhusu wachezaji ambao hawana injury Kama Madueke na Jackson alafu na viwango wanavyoonesha uwanjani
Ndio mana wote ni wa kuuza hawana faida kwnye timu, wanajaza tu nafasi wanazuia wachezaji wenye uwezo kununuliwa.
 
Estevão Willian na wenzake waripoti leo kwenye Chelsea kuanza maandalizi ya msimu mpya.
Leo, wachezaji wapya wanaripoti rasmi Cobham, huku mazoezi ya pamoja yakitarajiwa kuanza kesho. Taarifa zinaonyesha kuwa Estevão tayari amewasili London na ataanza mazoezi na timu Jumatatu hii. Wiki nzima itahusu kujenga mawasiliano ya awali, kufahamiana na wachezaji wenzake wapya, na kuanza safari ya kurekebisha muundo wa kikosi kwa msimu ujao.

1754229898952.png
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom