lembu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 19,383
- 25,490
Chelsea inahitaji kuongeza mauzo ya zaidi ya £60m ili kuhakikisha wachezaji wapya wanaweza kucheza kwenye mashindano ya Uefa baada ya kukiuka sheria za kifedha za bodi.
Faini alizopigwa Chelsea ni hizi hapa:Kapigwa fine yote hiyo kwa kosa gani, maana nilipokutana nalo tu nikalitupia hapa chap chap.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
| 🏟️ Timu | 💶 Kiasi cha Faini | 📝 Sababu ya Adhabu |
|---|---|---|
| Chelsea (England) | €31 milioni | Kukiuka kanuni za usawa wa mapato na matumizi ya kikosi; mauzo ya mali za ndani ya hoteli na uuzwaji wa timu ya wanawake yenye utata |
| Barcelona (Spain) | €15 milioni | Hasara kubwa kifedha; taarifa zisizo sahihi kuhusu mapato |
| Aston Villa (England) | €11 milioni | Matumizi ya kupindukia wakati wa mashindano ya Conference League |
| Lyon (France) | €12.5 milioni | Ukosefu wa uthabiti wa kifedha; tishio la kutengwa kwenye mashindano ya UEFA |
Wachezaji wa Chelsea walioripotiwa kuwa wanaweza kuuzwa katika dirisha la majira ya joto 2025, pamoja na makadirio ya thamani zao za soko ni:Faini alizopigwa Chelsea ni hizi hapa:
Faini ya Uro milioni 20 kwa kuvunja Sheria ya Ufuatiliaji wa Kifedha ya UEFA (UEFA Financial Monitoring Rule)
Faini ya Uro milioni 11 kwa kuvunja Sheria ya gharama ya Kikosi ya UEFA (UEFA Squad cost rule)
Jumla ni Uro milioni 31 au sawaswa na pauni mil 27
Sheria ya Ufuatiliaji wa Kifedha ya UEFA
Chelsea imetumia zaid ya kiwango kinachotakiwa na UEFA katika miaka mitatu iliyopita
Pia mauzo ya hoteli na timu ya wanawake haikubailiki na sheria za kifedha za UEFA kama ni mapato halali kwa sababu miamala ilifanyika kwenye makampuni tanzu ya BLUECO ambayo ndie mmiliki wa Chelsea
Sheria ya gharama ya Kikosi ya UEFA
Sheria ya UEFA inasema timu inatakiwa itumie sio zaidi ya 80% kwenye gharama za usajili na mishahara ya wachezaji lakini Chelsea wao wametumia zaidi ya 80% ambayo ni kati ya 80-90%
Hitimisho
Kwa sakata lote hili Chelsea na Aston Villa ambao ndio waliokumbwa na panga hili la UEFA safari hii kwa EPL wamekjubali makosa na pia watalipa hiyo faini
Pia Chelsea imekubali kutowasajili wachezaji wapya kwenye A-list ya UEFA hadi watakapotimiza masharti ya mauzo ya wachezaji. Kwa hili Chelsea inatakiwa kuuza wacheza angalau sio chini ya pauni milioni 60 ili waruhusuiwe kwuasajili wachezaji wapya kama akina:
Vilabu Vilivyoadhibiwa na UEFA (2024–2025)
- Liam Delap
- João Pedro
- Dário Essugo
- Mamadou Sarr
- Jamie Gittens
🏟️ Timu 💶 Kiasi cha Faini 📝 Sababu ya Adhabu Chelsea (England) €31 milioni Kukiuka kanuni za usawa wa mapato na matumizi ya kikosi; mauzo ya mali za ndani ya hoteli na uuzwaji wa timu ya wanawake yenye utata Barcelona (Spain) €15 milioni Hasara kubwa kifedha; taarifa zisizo sahihi kuhusu mapato Aston Villa (England) €11 milioni Matumizi ya kupindukia wakati wa mashindano ya Conference League Lyon (France) €12.5 milioni Ukosefu wa uthabiti wa kifedha; tishio la kutengwa kwenye mashindano ya UEFA
Timu ya kuuza na kununua kma biashara ya nyanya sokoniWachezaji wa Chelsea walioripotiwa kuwa wanaweza kuuzwa katika dirisha la majira ya joto 2025, pamoja na makadirio ya thamani zao za soko ni:
💰 Jumla: €247 milioni
- Nicolas Jackson - €50 milioni
- Noni Madueke - €40 milioni
- Christopher Nkunku - €35 milioni
- Raheem Sterling - €10 milioni
- Ben Chilwell - €15 milioni
- Axel Disasi - €22 milioni
- Carney Chukwuemeka - €18 milioni
- Renato Veiga - €25 milioni
- Armando Broja - €12 milioni
- Djordje Petrovic - €20 milioni
Ndio maana nilikwambia sera ya kusajili wachezaji wengi kwa wakati mmoja angalia madhara yake ndio hayaWachezaji wa Chelsea walioripotiwa kuwa wanaweza kuuzwa katika dirisha la majira ya joto 2025, pamoja na makadirio ya thamani zao za soko ni:
💰 Jumla: €247 milioni
- Nicolas Jackson - €50 milioni
- Noni Madueke - €40 milioni
- Christopher Nkunku - €35 milioni
- Raheem Sterling - €10 milioni
- Ben Chilwell - €15 milioni
- Axel Disasi - €22 milioni
- Carney Chukwuemeka - €18 milioni
- Renato Veiga - €25 milioni
- Armando Broja - €12 milioni
- Djordje Petrovic - €20 milioni
Madhara yako wapi?Ndio maana nilikwambia sera ya kusajili wachezaji kwa wakati mmoja angalia madhara yake ndio haya
Si ndio Kama tunakutana financial fair playMadhara yako wapi?
Hapana na unajua hilo halipoWachezaji wa THE BLUES wamekaa kimauzo mauzo. Sitashangaa dirisha hili tukiuza wachezaji muhimu ili kutengeneza faida wa wamiliki
Hii ni ajali kazini, huu msimu unaokuja ndio mtaona faida ya hizi sajiliSi ndio Kama tunakutana financial fair play
Hata hivyo hatuna hasara, kanuni za UEFA ni tight mbona za FA hatukukiuka!Si ndio Kama tunakutana financial fair play
Timu imemaliza top 4Hapana mkui labda useme hawa wachezaji wangeingia kwenye mikono ya Enrique. Maresca mikono yake inatetemeka.
Hizo pooints 69 EPL hazipatikani kwa urahisi nndg. Hata akina Arsenal Man city ni mbinde mbinde. Timu kwa ujumla bado ilikuwa changa na haijazoeana kisawa sawa. Natumaini sasa hivi wamezoeana na uchezaji wa msimu ujao hautakuwa kama huu ulioishaMaresca ameshindwa kurekebisha madhaifu kama timu ikishafunga bao la kwanza inasema good night, bao likisawazishwa na opponent, timu inasema good morning.
Mashabiki tunacheki game roho mkononi, kutangulia bao 1 au 2 kwetu sio salama kabisa.
Udhaifu wa 2 kwenye selection ya kikosi. Hana uhakika na kikosi anachokipanga. Akishafungwa ndio anaanza kuhaha kama mbwa koko kufanya sub za kuokoa jahazi.
Kiufupi Maresca amekuwa na maamuzi ya ovyo kwenye selection ya wachezaji, kuwapanga kwenye nafasi za kucheza, maamuzi ya kumng'ang'ania pazia Sanchez.
Maresca anatuaminisha ni world class coach kumbe ni mbarara
Wamarekani hawatofautiani kabisa na Wahindi kibiashara na kiubahili, tutakinywea sana kikombe wana Chelsea wenzangu 😩Wachezaji wa THE BLUES wamekaa kimauzo mauzo. Sitashangaa dirisha hili tukiuza wachezaji muhimu ili kutengeneza faida wa wamiliki
Bado Maresca ni average Coach na timu ni kubwa mno kwake.Hizo pooints 69 EPL hazipatikani kwa urahisi nndg. Hata akina Arsenal Man city ni mbinde mbinde. Timu kwa ujumla bado ilikuwa changa na haijazoeana kisawa sawa. Natumaini sasa hivi wamezoeana na uchezaji wa msimu ujao hautakuwa kama huu ulioisha
Maamuzi ya hovyo ni sawa ila natumaini anajifunza kwa sababu naye ni mgeni kapewa mzigo mkubwa
Kitu unachoshindwa kuelewa ambacho wengi wanamlaumu Maresca ni namna anavyo approach mchezo. Poch alikua na wachezaji wa kawaida sana tofauti na Enzo lakini tulifanikiwa kumaliza top four. Huyu Poch mtamdharau ila sielewi aliwakosea nini. Enzo game na Palmeiras unaona kabisa mbinu hana, ligi kuu karibia kila top four katufunga, walau Poch alikua anajitahidi tunatoa sare.Finali alizoshindwa Mauricio Pochettino. Tungekuwa naye hata UECL angeshindwa mbele ya Real Beatis
View attachment 3397245
- 2015 League Cup Final
- 2019 Champions League Final
- 2024 EFL Cup Final
- 2025 CONCACAF Gold Cup Final
Pochettino anamikosi na fainal tangu akiwa Spurs, PSG, Chelsea na sasa USMNTKitu unachoshindwa kuelewa ambacho wengi wanamlaumu Maresca ni namna anavyo approach mchezo. Poch alikua na wachezaji wa kawaida sana tofauti na Enzo lakini tulifanikiwa kumaliza top four. Huyu Poch mtamdharau ila sielewi aliwakosea nini. Enzo game na Palmeiras unaona kabisa mbinu hana, ligi kuu karibia kila top four katufunga, walau Poch alikua anajitahidi tunatoa sare.
Yapo mambo mengi ambayo Poch kamuacha mbali sana Maresca ila tusifike huko. Muhimu tuangalie kama coach ana mchango gani kwa rasilimali (wachezaji) zilizopo kuweza kutufikisha nchi ya ahadi.
MaduekeHapana na unajua hilo halipo
Uuzwaji wa wachezaji unaendana na mahitaji ya kocha
Falsafa ya hawa wamiliki wapya ni kununua wachezaji wengi na wachanga ili katika hao kocha awe na pool nzuri ya kuchagua
Kocha akishawachagua wachezaji wake hao wengine wanauzwa iwe kwa profit au kwa hasara
Lengo kuu ni kukwepa kuendelea kwuannunua wachezaji kama akina Sterling ambao ni bei ghali na wanakuja na mahitaji ya mishahara mikubwa.
Hawa wachezaji wachanga wananunuliwa bei chee, mashahara mdogo hata baadaye wakitakiwa kuuzwa ni rahisi
Case study nyingine ni kwamba kusubiri wachezaji wanaswe na timu kama Benfica, Dortmund au Brighton wanakuja kuuzwa wakiwa wachanag kwa bei ghali. Mimi naona huu mfumo unafaida hata wasipouzwa kwa faid kwa sababu timu inakuwa imekwepa kutumia pesa nyingi kwa wachezaji wazuri.
Wee fikiria mchezaji kama
Andrey Santos
Estevao Willian
wangeangukia kwenye mikono ya Brighton au Benfica wangeuzwa shilingi ngapi baada ya mwaka mmoja
Commitment ya hawa wamiliki hata kama wamefanya makosa mengi huko nyuma bado ni nzuri ukitofautisha na timu zingine kubwa. Wamjitoa sana kuwanunua wachezaji bora
Nataka niwahakikishie kuwa mchezaji akishaingia mikononi mwa Maresca na akiwa na amani naye hakuna mmiliki atalazimisha wauzwe. Kama wapo nipe hata mmoja