Umri hauchezi acha mbwembwe huwezi kuwa na shida na kombe ukawa na Jackson..
Unajua ukikuta mtu anabishia umri wa Nicolas Jackson na uchezaji wake inabidi kumuacha tu.
Umri ni factor kubwa ya decision making kwenye vitu vyote wala sio mpira tu.
Kuwa kiongonzi popote lazima ukomae kiumri ili usije fanya maamuzi eratic ukaangamiza watu au mali.
Kuoa au kuolewa sio tu mpaka ubalehe, utahitajika ku undergo some maturity ya ubongo ili uwe kwenye nafasi ya kufanya sound decisions kwa mke au mume wa mtu.
Ndio maana umri wa miaka 10-20 wakaita foolish age kwa sababu vijana wengi wa huo umri wanafanya maamuzi ya kijinga sana
Maamuzi sahihi ya Jackson ya kushindwa kupiga mpira kwa haraka na kufunga goli kwa sehemu kubwa ni umri wake mdogo na sio kwamba Jackson ni mchezaji mbaya. Mimi na wengine wengi tunaamini udhaifu huo ni wa muda mfupi tu na utaisha na Jackson atabaki kuwa ni mmoja wa wafungaji wakubwa EPL, kama sio 2025 ni 2026.
Kocha anayemkochi anakiri ni mchezaji mzuri na SD aliyemsajili anasema ni mchezaji mzuri. Wamiliki wamerizishwa na ubora wake wakamboreshea mkataba na wakamuongezea mshahara mnono hadi 2033.
Mashabiki nearly 70% wa Chelsea wanamkubali Jackson
Basi tu anabakia kalaghabao mmoja au wawili wa pale Manzese Uzuri au Kariakoo wanasema Jackson sio mchezaji mzuri kisa tu damu yake haimpendi
Mtabakia kuwa kalaghabao ila mwenzenu kapewa mkataba bora zaidi na mshahara mnono kwa sababu alikuwa the second best player after Cole Palmer msimu uliopita wa 2023/24, huu ni ukweli na utabisha na utabaki na ubishi wako hadi Moyo wako upanuke mara 10