Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Katika wachezaji walioorodheshwa hapo wa kuondoka sijaelewa yule dogo Petrovic anashida gani mpaka naye aondoke. Alifanya vizuri sana msimu uliopita kipindi Sanchez kaumia sasa naona kocha naye hamuhitaji.
Labda damu yake Kipa Petrovick haijaivana na damu ya Kocha Mkuu, kama zile enzi za Shevchenko na Drogber, nani ajuaye?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Kiukweli ni jambo linanishangaza na kuniumiza. Huyu dogo ni potential kubwa hii timu sijui imekuaje
Umenikumbusha Bonge la Kipa la Mwantesa Utd "Van Der Sir" alivyostaafu soka kwa sababu ya inshu za kifamilia ilihali alikuwa bora sana kiuwezo.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Enzo Maresco kumhusu Noni Madueke -

"Nilisema tangu siku ya kwanza yeye ni aina ya winga ninayempenda sana".

"Jambo muhimu zaidi kutoka kwa Noni leo ni kurudi nyuma kulinda shambulio la kaunta katika dakika ya 90".

"Tunaweza tu kuepuka mpira wa adhabu alioutoa kabla ya muda wa mapumziko."

@FabrizioRomano
 
Katika wachezaji walioorodheshwa hapo wa kuondoka sijaelewa yule dogo Petrovic anashida gani mpaka naye aondoke. Alifanya vizuri sana msimu uliopita kipindi Sanchez kaumia sasa naona kocha naye hamuhitaji.
Maresca alisema tangu mwanzoni kuwa Petrovic haingii kwenye mfumo wake. Hatakuwepo kwenye squad. Kwa hiyo naye atauzwa au kutolewa mkopo
 
Kiukweli ni jambo linanishangaza na kuniumiza. Huyu dogo ni potential kubwa hii timu sijui imekuaje
Djordje Petrovic anaondoka kwa sababu kwa umri wake (24yrs) na kwa profile aliyonayo hatakubali kuwa namba 3
Marseca chaguo lake la kwanza ni Robert Sanchez wa pili ni Filip Jorgensen na Marcus. Bettinelli anakuwa backup GK
 
Labda damu yake Kipa Petrovick haijaivana na damu ya Kocha Mkuu, kama zile enzi za Shevchenko na Drogber, nani ajuaye?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Hapana, Perovic hawezi kuucheza mpira, foot-work yake haifikii standard anayotaka Maresca
 
Ebu angalia jinsi Neto anavyokimbia kutafuta nafasi, world class
Ebu pia fuatili mtangazaji wa kiarabu, wa bongo haoni ndani

View attachment 3079056
Tukisema akili ya mpira ndio hiyo sasa, world class assist and world class finish. Mchezaji anapick mfungaji. Sio mbugila lenu hapo angepiga tu golini mara paap! yanakua magoli mnamsifia. Magoli ya papatu papatu.

Chelsea wanaendelea kuimarika japo defence bado hatupo vizuri, kuna timu zisipokuja kwa kutuheshimu watakula si chini ya goli 10. Na pia defence ikiendelea hivi kuna mechi tutaoga mvua y magoli.
 
Unachosema Mhoti ni sawa, kwa standard Neto amemuacha mbali Madueke ila kumbuka pia uchezaji unatofautiana sana mchezaji kwa mchezaji na hii ndio asset kubwa itakayofanya Chelsea ishinde mechi nyingi msimu huu
Defense zingine zinahitaji uchezaji wa Madueke na zingine huu wa Neto.
Muhimu ni Chelsea ipate point 3 kila mechi possible.
 
Binafsi nadhani wafungaji watakuwa wengi hivyo itakuwa ni vigumu kwa mchezaji mmoja kufikisha 20+ goals maana Mudueke, Palmer, Neto, Felix, Nkunku, Jackson, Mudryk watagawana dk za kucheza. Pale mbele ni Palmer tu ana uhakika wa kucheza almost kila mechi
Maoni ya ajabu: Ikiwa Noni Madueke atapata dakika za kutosha msimu huu chini ya Maresca na aina hii ya uchezaji, atafunga mabao 20+. Nini maoni yako
Fs
 
Hapana, Perovic hawezi kuucheza mpira, foot-work yake haifikii standard anayotaka Maresca
Hafikii kwamba hafundishiki au anaweza kidogo? Unadhani kuna Kipa ambaye ana compliment sets zote katika ubora bila mapungufu yoyote?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Maresca alisema tangu mwanzoni kuwa Petrovic haingii kwenye mfumo wake. Hatakuwepo kwenye squad. Kwa hiyo naye atauzwa au kutolewa mkopo
Ngoja tusubiri maajabu yake maana sio kwa fagio hilo.

Hivi sera ya Chelsea inasema nini juu ya vijana wanaozalishwa kwenye academy. Tutaanza kupoteza potential nzuri baadaye
 
Djordje Petrovic anaondoka kwa sababu kwa umri wake (24yrs) na kwa profile aliyonayo hatakubali kuwa namba 3
Marseca chaguo lake la kwanza ni Robert Sanchez wa pili ni Filip Jorgensen na Marcus. Bettinelli anakuwa backup GK
Huyu Bettineli anakula tu mshahara wa bure. Sanchez kwa upuuzi wake anafaa sana kuwa namba 3 basi tu
 
Kipa wa umri mdogo hawezi kukaa benchi mkuu. Timu zote huwatumia makipa wazee kama backup. Sachez akifanywa namba tatu atatafuta timu ataondoka, This is football mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom