Michi ya pre season inaweza isiwe kipimo bora cha uchezaji bora kwa sababu wachezaji wengi wanaocheza sio wa first team hupewa fursa za kuonyesha uwezo wao.
Celtic iliishinda City, msizime data hapa.
Hii timu iliyocheza haiwezi kuonyesha Chelsea halisi, tuseme ukweli hapa, Fofana hajacheza kwa misimu miwili, atahitaji nusu msimu mpaka awe fiti.
Badisahile amekuwa mzembe kabisa tangu enzi za Pochettino.
Gusto na James hawafai kucheza kiungo kama Cucurella.
Lavia pia atahitaji mechi kadhaa ili awe fiti kabisa.
Wachezaji wanaoamua mechi hiyo hawapo uwanjani, kama Cole Palmer, Marc Cucurella, Moises Caicedo, Enzo Fernandez, Conor Gallagher, na Nico Jackson.
Hakuna Chalobah kwenye safu ya nyuma, angalau Tosin akiingia kipindi cha pili atatuliza dhoruba kwani alicheza vyema katika mechi iliyopita.