Nimeangalia mechi yote asubuhi ya leo
Tumeweka wachezaji wengi wapya
Tumebadilisha timu 90% kipindi cha pili
Wachezaji muhimu wengi hawakuwepo
Nilichokiona, kubadilisha kocha kuna gharama, tumerudi square one
Hadi msimu uishe ndipo wachezaji watakuwa wameuelewa mfumo nam mbinu za kocha
Badi wachezaji wanavutwa na uchezaji wa Pochettino, mchezaji akipata mpira anabaki nao muda mrefu kabla hajampasia mwenzake wakati Enzo hataki mchezaji akae na mpira sana
Madueke hafai mfumo wa Maresca na ni mchoyo wa kutoa pasi, Angelo ni bora kuliko Madueke.
Josh Acheapong bado ana maeneo mengi ya kuboresha sana au hajiamini, Chalobah ni bora zaidi kuliko yeye.
Badiashile ni sikio la kufa
Armando Broja auzwe tena chap chap, atatupotezea muda zaidi
Lavia, George, Nkunku na Marc Guiu wameonyesha uwezo mkubwa sana
Sachez pia kacheza vizuri
Colwill mzalendo wa kweli
Wachezaji muhimu ambao hawakuwepo
- Cucurella
- Caicedo
- Enzo
- Jackson
- Palmer
Baada ya preseason kuisha nadhani ndio tutapata picha halisi
Ila ule uchezaji wa Leicester city sijaona leo