Lakini mwanzoni si mlisema hawa wachezaji ni matakataka? wakati kocha ndie alitaka kuwafanya waonekane takataka.
Anyway, Poche akiendelea alichokivumbua katika mechi za mwishoni hakuna mshabiki ataendelea kumtupia mawe na ndio maana mimi nasema hata kama simkubali, nitampa msimu ujao kuona kama hatavuruga timu tena kama alivyofanya sehemu ya kwanza ya msimu huu.
I will give him time to prove me wrong
Vitu ambayo nimeona Poche anaweza kuwa bora msimu ujao ni:
- Kusema hataendelea kusema tena kuwa wachezaji ni wachanga na wasio na uzoefu
- Hataendelea kusema kutrust the process
- Sasa anakiri Chelsea inatakiwa kushindania makombe msimu ujao
- Ijumaa hii ya tarehe 17 April 2024 alikuwa na dinner na Tod Boehly ambaye ndie anayetaka afukuzwe pale klabuni, na nadhani wameongea mengi mema na wameshamaliza tofauti zao kwa sasa.
- Alikiri kuwa hata tukimaliza na 5 na Chelsea ikashiriki michuano ya Ulaya haitoshi kwa wamiliki, kwa Sporting directo, kwa wachezaji na kwa mashabiki wote
- Amedai kuwa amefurahia sehemu ya mwisho wa ligi, ila hatashangilia kwa sababu ya historia ya Chelsea inahitaji zaidi
- Kwa sababu wachezaji wanampenda na wako tayari kumpigania uwanjani
- Kwa sababu ni wazi ameweza kuinua viwango vya Palmer, Madueke, Gallagher, Jackson, Malo, Chalobah na Cucurella
- Ameweza pia kumtumia vizuri Cucurella kwenye inverted LB
- Enzo anakiri kuwa alipokuja kwenye klabu, kulikuwa shagalabagala na sasa Pochettin o ameweka utaratibu na utambulisho, na maadili na nidhamu ya kazi umeimarika
- Sio chuki binafsi hapa, ni kweli Pochettino anawazidi makocha wengi kwenye kumanage wachezaji hasa wa calibre hii ya Chelsea. Mfano mzuri ni jinsi anavyokwenda sambamba na Madueke. Kwa kocha mwingine Madueke wala asingecheza mechi mbili pale Chelsea
- Baada ya kukutana na Boehly Ijumaa, Pochettino anawasiwasi kama kikao cha kumtadhmini kitakuwepo tena, anadai wasaidizi wake wataondoka kwenda likizo na yeye atakuwepo kwa siku chache kabla hajaondoka kwenda likizo. Hii ni dalili kuwa uongozi sasa wameshamkubali na hawana haja ya kumtadhmini