Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Hayo yite unayoyasema ila stil tumecheza vizuri na chances tukatengeneza kama sio uzembe wa jackson enzo alikuwa anaondoka na assist leo,

Siwez mlaumj Poch kwa leo.
Enzo hakucheza vizuri, anatakiwa apewe dakika chache hadi atakapofanyiwa operation ya hernia yake inayomsumbua. Poche bado anaforce wachezaji fulani kucheza hata kama wamelemewa. Rotation ni filosofia nzuri ya kuwapumzisha wachezaji muhimu na pia kuwapa wale wasiopata nafasi muda wa kuonyesha makali yao.
Mimi bado naamini Gallagher angecheza nyuma na Caicedo na Sterling angepata nafasi jana tungeongeza fursa za kufunga mabao
 
Kuna maamuzi ya Chilwell ambae ni Experience player na ni Vice Captain sehem ya kupiga square pass kwa sterling yeye anaweka extra touch
Ila niliipenda sana ile run ya Chilwell, Cucurella hawezi hiyo. Aliharibu tu alipochelewa kurelease mpira
 
Pamoja na misses zote bado yeye ndie kacheza vizuri kuliko wengine jana
Akiweza tu kuboresha clinicalityy kwenye kuweka mipira wavuni. wote tuliokuwa tunamuita takataka tutatubu kwake
1713679639032.png
 
Handball ya wazi kabisa, hawa marefa wa EPL wanaudhi sana

View attachment 2969657
Achana na hizo penalties za kupewa, kuna Umbwa mnayoifuga hapo darajani inaitwa Jackson hio ndio iliyowakosesha kwenda fainali, hio Umbwa imekosa clear chances zaidi ya 3 na kutusababishia sisi Man United matatizo makubwa sana kwenye final.

#Poor Wacko Jacko
#Poor wavaa blauz wote
tapatalk_-294146578_524x556.jpg
 
Ndg Jackson wala hafananii hata kidogo Havertz. Havertz yuko clinical zaidi ya Jackson ila Jackson anajua kucheza mpira kuliko Havertz. Hao ni watu wawili tofauti kabisa
Kai anamaliza msimu na goal 7 unasemaje ni clinical kuliko Jackson tena Jackson huu ni msimu wake wa kwanza Flano yupo sahihi
 
Jackson huwa ana nini ambacho mimi huwa sikioni?
Anajua kuhold mpira, ana kasi msumbufu kwa mabeki na anasaidia katengeneza nafasi kwa wenzake kitu moja tu anakosa ni kutakuwa clinical kwenye goal, kulingana na hizo sifa nyingine nilizokutajia ndio inapelekea kuanza kila game
 
Ngoja niwachambue wachezaji walivyocheza jana
Ujumla
Wachezaji wetu karibia wote hawawezi kuruka, Ake pamoja na kuwa mfupi lakini anaweza kumnyang'anya mpira wa juu Disasi ambaye kamzidi urefu. Kocha anatakiwa agundue hilo la kulifanyia kazi

Petrovic
Huyu bana alituokolea mikwaji mingi sana japo upanguaji wake wa mikwaju bado sio mzuri sana

Chalobah
Jana alicheza vizuri sana, yuko sharp sana

Silva
Japo alikuwa shacky na baadhi ya passi kutoenda salama ila overall katumia vyema uzoefu wake kucheza vizuri na daima pivot ya Silva na Chaloba inakuwa nzuri. Kocha angebakia na hii pivot, Disasi na Badiashile wasugue bench kidogo

Gusto
Pamoja na mazuri yake mengi sana kwenye kushambulia ila Gusto hana speed. Inapokuja confrontation ya 1X1 huwa mara nyingi anazidiwa pace na speed. Aliweza kuwadhibiti akina KDB, Alvarez na Grealish vizuri sana

Cucurella
Cucu bado hatumii akili japo jana alitumia juhudi sana, aliweza kupress na kuwathibiti akina Silva na Walker vizuri sana wasilete madhara golini mwa Chelsea. Angekuwa na akili kama ya Chilwell au James angekuwa bonge la full back

Caicedo
Anajitahidi ila bado ana utoto sana hasa kwenye maamuzi, anajua kujenga build up vizuri sana ila inapokuja kwenye kufanya maamuzi sahihi ndipo alipotuangusha jana. Bado pia alifanya madhambi ya kiuzembe kwenye maeneo ya hatari na kuiweka Chelsea kwenye presure kubwa

Enzo
Pamoja na kutengeneza nafasi nzuri kwa Jackson akashindwa kufunga ila uwezo wake wa kucheza vizurii bado unazidi kudorora sio kama alivyoanza miezi sita yake ya kwanza. Passi zake nyingi zinaharibika. Pia inawezekana Hernia aliyonayo inamuadhiri kwenye kucheza vizuri. Nadhani baada ya operation atarudia ubora wake

Gallagher
Sikuona shida yake jana, ameendela kuwa mtibuaji wa movement za opponent na pasi zake zilikuwa bora jana. Muhimu alicheza nafasi ya LW na kaitendea haki vizuri

Palmer
Palmer jana hakuwa kwenye form yake nzuri japo aliweza kumthibiti Rodri asilete madhara kwenye lango la Chelsea. Kila wakati alikuwa naye kumnyima raha ya kucheza. Bado yeye ni mfano wa kuigwa kwenye maamuzi sahihi akiwa na mpira

Madueke
Akiwa na mpira ni hatari japo mbinafsio sana na mashuti yake yalikuwa hayana akili

Disasi
Kacheza vizuri kwa muda mfupi alioingia japo madhara ya city yalitokea upande wake

Chilwell
Kaonyesha uwezo wake wa kukimbia na kuoverload final third ya adui japo jana alifanya uamuzi wa kujinga kuchelewesha kutoa pasi kwa Sterling dakika ya 90 na hivyo kutukosehsa fursa ya kupata bao la kusawazisha

Mudryk
Anacho kitu ambacho bado kimefichwa. Alipoingia hakuwa na impack yeyote

Kama ni kuwataja wachezaji watatu waliocheza vizuri jana zaidi ya wengine
  1. Gallagher
  2. Cucurella
  3. Chalobah
 
Kai anamaliza msimu na goal 7 unasemaje ni clinical kuliko Jackson tena Jackson huu ni msimu wake wa kwanza Flano yupo sahihi
Clinicality inaangaliwa na Chances ulizokosa na sio magoli ya kufunga, hili naona liko wazi mno
 
Hayo yite unayoyasema ila stil tumecheza vizuri na chances tukatengeneza kama sio uzembe wa jackson enzo alikuwa anaondoka na assist leo,

Siwez mlaumj Poch kwa leo.
Poche Leo alikuwa kwenye ubora wake nimpumbavu tu anayeweza kumlaumu hoja ya kwamba kwanini asingemuanzisha Enzo ni kwasababu lembu hukuangalia mpira vizuri Enzo alicheza vizuri sana pass zake zilikuwa ni hatari amepiga key pass nyingi ikiwemo chance ya Jackson aliyokosa pass ilitoka kwa Enzo pia alikuwa anarahisisha mpira na movement ya mchezo kwenda smooth.Binafsi sikupenda Enzo, Gallagher na Caicedo waanze pamoja baada ya kucheki mpira vizuri niliona Kocha alikuwa sahihi kwa asilimia zote plan ilitiki aliyetuangusha ni kosakosa za Jackson. Kuhusu sub ya kuingia Disasi na kumtoa Agusto ni kwasababu Agusto alishaumia hakutaka aumie zaidi kama taadhari.
 
Jackson kumbe ni Kai mweusi tu
Jackson kamzidi kai mkuu mlinganisho wako sio sahihi pamoja na kosakosa zake ana 10 na assist 7 tena ni msimu wake wa kwanza, anajua kuhold, ana kasi, nguvu, pace na dribble huwezi kumcompare na yule goi goi kai
 
Ila ni upumbavu pia kusema kuwa Enzo kacheza vizuri kwa sababu ya pasi moja nzuri kwenda kwa Jackson. Pasi nyingi zilipotea, alikuwa too Shacky and sloppy, uwezo wake wa long balls umefall. Hapo alipo anaumwa hernia. Kwanini kocha amlazimishe kucheza?
 
Ukiachana na uduanzi wake kwenye finishing, bado ana faida kwenu jamaa. Unadhani hizo nafasi anazokosa zinamkuta kwa bahati mbaya?
Yaani wewe umeona ambao wengi hawaoni. Angekuwa ni fala wala hizo nafasi za kukosa asingezipata. Jackson anajua kujiposition ili apewe mpira, Siku hili pepo la kuogopa goli likiisha, Jackson atafunga magoli kama Didie Drogba hadi mtampigia magoti ninyi mnaomuita takataka
 
Nipe tofauti ya Jackson na Mzize. Wote wanajua kuhold mipira, kukimbia ila ni zero kwenye finishing. Wote wazuri kutokea pembeni at least mwingine anakua bora akicheza kama mshambuliaji wa pili.

Jackson anayo nafasi ya kufanya vizuri kama atarekebisha finishing yake anapokua golini ila mpaka sasa ni very poor japokua na magoli yake 10 PL.
 
Mimi sioni kama ni kurekebisha, huyo bado mtoto. Ndio anakulia kujua mpira
Drogba japo alikuja Chelsea akiwa na miaka kama 25 hivi lakini season yake ya kwanza alikuwa na poor finishing za kizembe hivi hivi kama Jackson. Jackosn atakuja kuwa bonge la mchezaji akifikisha miaka 24 au 25 hivi
Tumvumilie kijana wetu
Uongozi unatakiwa tu umtafute striker mzoefu wa kucheza hiyo nafasi msimu ujao ili kama Jackson atapata dakiak acheze winga au namba 10
 
Jackson kamzidi kai mkuu mlinganisho wako sio sahihi pamoja na kosakosa zake ana 10 na assist 7 tena ni msimu wake wa kwanza, anajua kuhold, ana kasi, nguvu, pace na dribble huwezi kumcompare na yule goi goi kai
Nilikuwa naongelea ukosaji wake wa magoli wa kijinga mno alioonyesha jana. Hata hivyo, hata hivyo vingine unavyosema amemzidi Kai sidhani kama ni kwa asilimia kubwa. Ni kwamba tu Kai ukimtazama sura yake amekaa kiboya boya huku Jackson ana sura ya kazi kazi hivyo watu wakiwaangalia hao wawili wanamuona Kai mbovu zaidi.
 
Kai nafasi kama zile asingekosa labda chache sana
Ubovu wa Kai uko sehemu kama tatu hivi
  1. Hajui kujiposition kama Jackson
  2. Hawezi kuhold mpira na kusesereka nao kwa kufanya dribling kama anavyofanya Jakcosn
  3. PIa Kai uwezo wake wa ball recovery na disposesion ni mdogo kuliko wa Jackson. Na ndio maana wachambuzi wanaojua mpira wanadai Jackson anazo potentials nyingi ambazo akikomaa (ndani ya mwaka au miwili) atakuwa bonge la forward
Tukumbuke pia kuwa Kai ni mzuri sana hewani wakati Jackson sio mzuri kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom