Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Wachezaji wa Chelsea sasa wanajipanga uwanjani kama watoto wa mitaani tu waliokotwa kucheza mpira
 
Madueke kasababisha penalti na kaipiga vizuri sana, yeye ndie kaleta uhai mbele baada ya HT
 
Hizi game za kushinda ushindi wa papatu papatu ndio zinawafanya waone waendelee kumpa muda ila kama wangekuwa wanaangalia performance huyu hakufaa hata game inayo kuwepo ilikuwa tu kesho asubuhi mnatupia virago

Sijawah kuona kocha mbishi kama huyu
 
Baadaye kidogo utaona
  1. Anavuruga upangaji wa timu
  2. Anafuga uzembe wa wachezaji
  3. Sub zake hazina manufaa kwa timu
  4. Kwaweka benchi wachezaji bila sababu,
kocha anaye stick na XI ile ile ni yule mwenye timu nzuri sasa yeye wachezaji wanafanya uzembe ule ule na anaendelea kuwapa nafasi huku wengine wakiozea benchi
Ukiona ivyo ujue hakuna mchezaji wa maana anayeweza kumchallenge yule anayefanya madudu
 
Ukiona ivyo ujue hakuna mchezaji wa maana anayeweza kumchallenge yule anayefanya madudu
Pochetino mvuta bangi mbichi mbichi kabisa una muwekaje benchi Madueke na Maatsen LB anacheza LW huu ni ukichaa,huyu kocha hajui kutumia wachezaji,angeendelea na upuuzi alio anza nao wa kumchezesha Maatsen LW na Madueke akae benchi kama tungepata goli la pili.
 
HONGERENI SANA THE BLUES KWA USHINDI.

Sikubahatika kuangalia mechi ila kwa highlights za magoli nilizoona, kwa kasi walizonazo GUSTO & MUDYK ni mtaji tosha kwa kocha kimbinu.

Nafasi ya 10 inasema THE BLUES popote ulipo tupo.
Na pia baada ya kuingia Lavia kaleta utulivu mkubwa pale kati alikuwa kwenye ubora
 
hii timu imeshakuwa gari la mkaa trip shamba trip gereji, mechi inayofuata tunapoteza maisha yanaendelea
 
Pochetino mvuta bangi mbichi mbichi kabisa una muwekaje benchi Madueke na Maatsen LB anacheza LW huu ni ukichaa,huyu kocha hajui kutumia wachezaji,angeendelea na upuuzi alio anza nao wa kumchezesha Maatsen LW na Madueke akae benchi kama tungepata goli la pili.
Lakini ni mara ngapi anawachezesha hawa wachezaji kwenye position zao na nini kilitokea? Ju,i kati kawachezesha Broja na Jackson kwa pamoja nini kinatokea? Wakati mwingine anafanya kubet tu aone wanaweza leta maajabu gani lakini inakua ngumu. Hakuna timu ilitotengeneza nafasi nyingi za kufunga kama Chelsea unataka Poch aingie yeye akafunge? Kina Jackson wanaruka ruka tu.

Spirit ya upambanaji hamna kabisa. Tukishafungwa mechi moja inayofuata ndio wanajua lazima wapambane
 
Mkuu angalia game ya carabao cup baada ya Gusto na Matsen kuingia na kucheza kama RB n LB hali ilikuweje na uangalie wakat wanacheza Disasi na Colwil
Kiukweli kabisa ninaouona Colwill, Disasi na Gallagher hawa ndio wachezaji nawaona wanacheza kwa spirit ya hali ya juu muda wote wakiwa uwanjani. Pengine hiyo ndio sababu wanaanza zaidi.
 
Spirit ya upambanaji match after match inaandaliwaje au inatengenezajwe au inapatikana vipi kwa wachezaji?

Nani mwenye jukumu la kuandaa hiyo sprit

Mchezaji mwenyewe?
Captain?
Kocha?
Mashabiki?
Slogan ya timu?

Case study - Liverpool
Mkuu spirit ya upambanaji haiandaliwi na mtu au kundi moja la watu. Hiyo inakuja kwa mjumuisho wa mambo mengi kama usajili mzuri, maslahi mazuri, benchi bora la ufundi na hata historia inachangia kuleta spirit ya mchezaji kuipambania timu. Sasa kinachobaki ni hulka ya mchezaji mmoja mmoja ndio inapelekea leo hii mnamlaumu kocha. Unadhani ni kocha gani atakuja kubadilisha hii hali? Hakuna kocha ataweza ila kinachobaki aendelee kupewa nguvu then yeye ndio ataona ni wachezaji gani hawamfai atawaondoa. Hawa kina Madueke mnaowasifia leo mtawakataa mechi 3 zijazo.

Wachezaji wetu wengi hawajielewi. Atakuja kocha mwingine wataperform vizuri mechi 4 kinachofuata watarudi kwenye normal default setting.
 
Ni kweli unachosema Mkuu. Nakumbuka ile spirit ya mashindano ya UEFA 2021 ilikuwa ya hali ya juu.

Kama unavyosema spirit inachangiwa na mambo mengi kama muunganiko mzuri wa kocha na wachezaji, wachezaji kwa wachezaji.

Mfano kwenye ucaptain THE BLUES tunafanya masihara sana msimu huu.

James - amepewa ucaptain mchezaji ambaye anacheza mechi chache sana kwa msimu, timu imekosa kiongozi wa kudumu uwanjani. Hata akiwepo kwenye baadhi ya mechi huoni ule ucaptain

Chillwell - ambaye ni captain msaidizi ndio walewale mechi chache.

Gallagher - anavaa tuu kile kitamba kama fashion au ili ajitume zaidi lakini hafanyi majukumu ya ucaptain, poor communication na wachezaji wenzake uwanjani.
Hiki ndio kinatufelisha pia. Ila kiuhalisia nani atavaa kitambaa tofauti na hao? Kwa hiyo hatuna budi kwa hao wenye u afadhali
 
Lakini ni mara ngapi anawachezesha hawa wachezaji kwenye position zao na nini kilitokea? Ju,i kati kawachezesha Broja na Jackson kwa pamoja nini kinatokea? Wakati mwingine anafanya kubet tu aone wanaweza leta maajabu gani lakini inakua ngumu. Hakuna timu ilitotengeneza nafasi nyingi za kufunga kama Chelsea unataka Poch aingie yeye akafunge? Kina Jackson wanaruka ruka tu.

Spirit ya upambanaji hamna kabisa. Tukishafungwa mechi moja inayofuata ndio wanajua lazima wapambane
Kwa sasa Pochetino anabahatisha tu sio lazima ufunge magoli mengi ushinde mechi,team haina balance ndio maana tunapoteza mechi,kiufupi sioni chelsea tukitoa 0-0 tutafungwa tu kama tusipofunga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom