Mkuu
juan david baada ya kupitia comments nyingi hapa haswa za kwako na
lembu, juu mjadala unaondelea kuhusu poor performance ya timu.
Kuna ambao mnasema kocha ni tatizo na kuna ambao tunasema wachezaji ni tatizo, na wote tuna hoja zenye mashiko, kulingana na mitazamo.

Hapa inawezekana kuna mitazamo 2 ya kufanyia maamuzi.
1. Poche ni kocha mzuri inawezekana wachezaji waliopo hawafit kwenye style/mbinu/mifumo yake. Zaidi labda Poche sio kocha wa kubadilika kiuchezaji kulingana na wachezaji waliopo, labda ni muumini wa style moja tuu ya uchezaji na inayohitaji aina flani flani ya wachezaji.
SOLUTION:- Asajiliwe wachezaji wachache ambao yeye ataona wakiingia kwenye kikosi chake watabadilisha hali ya mambo na timu itacheza kama anavyotaka hence matokeo chanya.
2. Kama uongozi timu unadhani wachezaji waliosajiliwa ni wazuri sana na wanajitosheleza kila idara na still wameshindwa kumatch na Poche na kuwaondoa kusajili watakaomatch na Poche itakuwa gharama zaidi au kubomoa timu.
SOLUTION:- Uongozi umuondoe Poche wamlete Kocha mwingine ambaye mifumo/Mbinu zake zitaleta performance kubwa kwa wachezaji waliopo hence matokeo chanya.

Kwahiyo hapo uongozi utapima SOLUTION ya haraka ni ipi ili kuinusuru timu kuendelea kupata matokeo mabovu na ya muda mrefu.